webnovel

Nani????!!!

Watu wote muhimu walikuwepo.Kwenye kiti cha kifalme alikuwepo Mesel mwenwtwewe.

"Jamani ningependa kutowapotezea muda wenu hapa.Leo nimewaita hapa ili niwatambulishe kuwa nimeowa binti kutokea Atlas,Alicia.Ningependa kumtambulisha kwenu.Alicia njoo mbele tafadhali."

Akasema Mesel.Alicia akatabasamu na kumsogelea Mesel taratibu.

"Nipatie taji la kimalkia." Akaagiza Mesel.

Taji likaletwa haraka.Alicia akapiga magoti tayari kwa kuveshwa taji halisi la umalkia.Avrie,yule mwanamke aliyekutana na Alicia kule chumbani akapiga hatua za haraka haraka kumsogelea Mesel.

"Nini unachonionyesha Mesel?" Akauliza Avrie kwa mshangao mkubwa mno.

"Umewezaje kwenda kuowa ilhali mimi na wewe ni mke na mume?Mimi ni mkeo usijisahaulishe"

Akasema Avie akilia.Alicia akasimama na kumtazama Avrie.

"Nani?????!!!!!" Akauliza Alicia kwa mshangao.

"Alicia..." Akaita Mesel kwa upole.

"Usiseme kuwa unapenda kunishangaza tena Mesel "Akasema Alicia kwa hasira.Hakuna jambo alilokuwa akilichukia kama kuolewa mke mwenza.Akakimbia kutoka pale kwa hasira akilia pia.

Mesel akamgeukia Avrie na kumtazama kwa hasira.

"Ndio umefanya nini sasa Avrie?"

Akauliza Mesel kwa ukali mno.

"Ukitaka kusikia mlio wa ngoma lazma ujue kuucheza pia"Akajibu Avrie na kuondoka kwa nyodo.

~ Animas sasa~

Ecca...!" Nora sasa akaenda kumuona Ecca.Nyumba ilitulia mno na kumfanya Nora ajiulize kwanini. Ghafla akasikia sauti ya kilio kutokea bafuni.Kwa mwendo wa taratibu akausogelea mlango wa bafuni na kuufungua.