webnovel

Welcome to create on WEBNOVEL

WIVU WANGU UCHIZI WAKE:01

Katika maisha yangu sikuwahi kuwaza kama kuna siku nitakuja nikose hata shilingi kibindoni,hata ile ya kunisaidia kupata chochote kitu cha kujitafuna katika midomo yangu na kuingia katika tumbo langu.

Maisha yangu ya ndoa kwangu yalikuwa ni magumu magumu sana,tangu nilipoolewa na mwanaume huyu hakuna kitu kimewahi kuwa sawa kabisa,ni mwanaume asiyejali kitu chochote kile,wanawake ndani kwangu wanapishana huku nikitambulishwa kuwa ni ndugu zake na mwisho unakuta wakiwa katika huba,hii ilinitesa sana na ndipo nilipokuwa nikiwaza kuondokana na hali hii,nitakwenda wapi?,Getrude mimi bado sikuwa nafahamu kabisa,nilikuwa katika dimbwi la mawazo sana.

Siku ile nikiwa nawaza nikiondoka nitakwenda wapi?,nitafanya nini?ndipo nilipomkumbuka rafiki yangu,kipenzi changu Lucy,huyu ni rafiki yangu wa muda mrefu sana,tumeishi miaka mingi sana kwa upendo tokea kipindi hiko tukiwa katika umri mdogo mpaka mimi ninaolewa ndiyo nilipotezana na marafiki zangu wengi akiwepo huyu Lucy.

Nilijua upendo wake kwangu,nilijua moyo wake wa upendo na namna tulivyowahi kuishi kwa upendo nyakati zile,hivyo nilipanga kumtafuta yeye mpaka nimpate kwani ndiye mtu wangu wa karibu tangu hapo na ndiye mtu ninaweza kuzungumza naye mambo ya ndani na akanilewa.

Nilimtafuta mtu ambaye nina namba yake,baada ya kupokea tu tulisalimiana na ndipo nikamwambia"samahani nina shida sana na Lucy una namba yake?"

Yule mtu aliniambia"acha mambo yako wewe unakosaje namba ya Lucy,unanitania ujue."

Nilijibaraguza tu na kisha nilisisitiza ya kuwa nilipoteza namba ile hivyo kama angekuwa nayo anipatie na ndipo yule niliyempigia aliniambia"subiri muda si mrefu nitakutumia."

Nami nikakubali.