Chuo mimi nimemaliza moja ya chuo kikubwa hapa Dsm, baada ya kumaliza chuo sikutaka kurudi home kabisa maana niliwaza hata nikienda home kule nitafanya nini? Nikakae na mama tu? Niwe nakula na kulala? nikakukumbuka ule msemo unaosema mtoto kwa mama hakui bali analemaa akili.
Niliamua kwenda kwa Uncle wangu kukaa huku nikiendelea kutafuta kazi hapa mjini, alikua anaishi Mikocheni. Kipindi cha weekend nilikua natoka chuo nakwenda Mikocheni nashinda kule kwa Uncle then jumatatu narudi chuo, pale palikua kama home tu.
Nikaanza kusambaza CV kwenye mataasisi, makampuni, NGO's kwenye mabank na sehem nyingi tu hapa Dsm lakini patupu sikufanikiwa kupata sehemu hata ya kujitolea.
Kuna siku nilikuwa nimekaa na Uncle tunaongea akaniuliza umemaliza chuo sasa una mpango gani?. Nikamwambia abc zote kwamba nimepeleka maombi yangu sehemu mbalimbali nasubiri majibu kama nitafanikiwa ama laah. Akanambia kuanzia jumatatu tutaanza kwenda wote kazini, lakini utaweza mikiki ya Kariakoo?, nikamwambia ni bora nishinde huko kuliko kubaki hapa home, I hate that.
Kweli jumatatu ikafika tukaenda huko kwa Wachina, ile siku sikutaka kuuliza ni kazi gani lakini nilikua najua Uncle anafanya kazi kiwanda cha mabag. Tulivyofika pale kiwandani Uncle akanitambulisha kwa Mchina.
UNCLE: "Hey Mr ping this is my Uncle, My sister's son. Call him INSIDER."
MCHINA: "Ooh you look alike I thought is your son, akacheka. huyu mchina alikua hajui kiswahili hata ngeli alikua anaibia kwa mbali. Mchina akanambia hey "Rafiki" karibu."
MIMI: "Thank you."
Uncle akaniita niingie store akanambia kazi yangu itakua ni kusupply mabag kule Kariakoo, kwenye hii kampuni yeye alikua ni Sales and Operation manager na kampuni ilikua inatengeneza journey bags na backpack bags na pilot bags.
Canter ilikua imefika pale tayari kwa upakizi, so tukaanza kupakia mabag mle kwa gari na kuyapanga kuyapeleka Kariakoo kwa wateja. "Ipo hivi pale kiwandani sio kwamba ndo wanaanza kutengeneza hapana wanafanya assembling tu, material zote zinatoka China, pale ni kuassemble na kuyapeleka sokoni".
Ile siku nilipiga sana kazi nakumbuka tulipiga trip 2 ila kila tripu ilikua na bag 200, sio poa kupakua bag pale Kariakoo ni mtihani yaani foleni za watu zilikua zinakera sana. Uncle akawa ananilipa cash kwa siku 10,000/=, wakati naanza alikua ananinulia chakula ila baadae akaanza kunikataa so nikawa najilipia, kuhusu kwenda kazini tulikuwa tunaondoka wote kwa gari asubuhi.
Nikaimasta kazi kwa muda mfupi sana ikafika stage akawa ananiacha niende peke yangu na dereva mitaa ya Kariakoo na wateja nikawa nimewajua tayari haikuwa ngumu kwangu. Uncle akanambia upo vizuri ikafika stage hata madeni nikawa nakwenda kukusanya then napeleka bank, yaani unakuta nimekusanya madeni mpaka 80million, hiki ndo kipindi nilikua nashika pesa nyingi sana.
Nilikua nimejenga urafiki na baadhi ya wafanyakazi wa pale kiwandani, siku katika kupiga story jamaa akanambia naona sikuhizi umepanda cheo unapeleka mabag mwenyewe Kariakoo. Nikamwambia nimemasta kimtindo akanambia safi inabidi mzee wako majukumu yapungue maana umri unakwenda huko Kariakoo atuachie vijana. Jamaa akaniuliza posho si unapewa ukienda kupeleka mzigo?? nikamwambia sio haba kuliko kukaa bure, akauliza kwani unalipwa kiasi gani? nikamjibu 10,000. Jamaa akasema Uncle wako anakupiga atlist angekupa hata 50,000/= nikamwuuliza kwanini?, jamaa akanambia posho ya kwenda kupeleka mabag kwa siku ni 100,000/=
Jamaa akasema mzee wako anakuonea sio haki ile kazi ni risk, "hii kazi kama jamaa anavyosema kweli ni risk sababu unaweza kuibiwa kweupe, Kariakoo si mnaijua? "Kuna siku tulikua tunapakua mabag nilikua na moja ya wafanyakzi wa pale sasa jamaa alichanganya mafile akampa bag muhuni mwingine. Ilibidi akatwe kwenye mshahara, ni hivi tukikaribia Kariakoo tunawapanga wateja mapema. Kama mnavyojua maduka ya kariakoo yako barabarani plus yale mafoleni ni kichefuchef so huwa tunapakua mabag mlemle kwenye foleni. Mhusika anakuja na vijana wake wabebaji, inatakiwa uwakariri vzr maana ukizingua tu unaweza mpa mzigo mtu mwingine."
Jamaa baada ya kufunguka hayo pia akanambia mzee wako kila bag anapata commision kwa bag la set 3 analipwa 1,000 na set 2 analipwa 700 (Zile bag za safari, set 3 ndani zinakuwa mbili yaani ukifungua zipu za bag kubwa ndani kuna kuwa na bag 2. Na hizi set 2 ukifungua zip ndani kunakuwa na bag 1), nikawaza hata lunch najilipia, uncle anaplay fouls sio haki.
Nikakumbuka matukio mengi tu mfano sometimes nikipeleka mzigo before sijaondoka atanambia ukifika Kariakoo piga simu kwamba TRA wamekukamata risiti sio sahihi, then utasema wanataka million 2, so mchina alikua anatuma hela. Nilikua nafanya hayo yote afu atanipa 50,000 tu au asinipe kabisa, nikikusanya madeni kama na million 30 atanambia ingiza kwa account ya kampuni maybe million 27 then million 3 nampelekea, zile ndo zilikua commission zake. Uncle wangu alikua anapiga sana hela shida alikua na madem wengi sana.
Kufupisha hii story, Mchina akaanza kunikubali sababu nilikua nampa ushauri baadhi ya mambo, akawa close sana mimi. Hiki kitendo Uncle hakupenda aliona kama nataka kumpokonya ugali wake, nikaona anaanza kunikataa mara anipe kazi ya kwenda kuangalia madogo shuleni, sababu zikawa nyingi mara biashara imekua ngumu sijui mambo yakikaa sawa ataniita. Kama msomi nikajua hapa sina changu, maana jamaa kule kazini alikua ananipa mkanda mzima kinachoendelea. Ukweli hii kazi ilikua inanisaidia sikosi hata pesa za vocha na matumizi yangu binafsi.
Nikaanza kukaa home na Aunt yangu, yeye alikua ni mama wa home tu. Hakuna kitu kigumu kama kuishi na ndugu inahitaji moyo na uvumilivu sana. Aunt yangu ni mvivu sana hata kwenye masuala ya mausafi hayuko active, nafikir ni moja ya sababu Uncle akawa na michepuko mingi. Ubaya sasa Uncle alikua anamsikiliza sana Aunt kwa lolote alilokua anasema yaani ni shida. Sasa hapa home tulikua tunabaki mimi na Aunt, madogo 2 wako boarding mmoja wa kike ndo alikua mdogo ansoma anatoka asbh anarudi jioni.
Nikaanza kuwa house boy wa mle ndani naamka Asubuhi sa12 nimpikie mtoto chai, baada ya hapo nitafanya usafi na kuosha vyombo, mchana nitapika chakula, jioni ninakazi ya kupikia mbwa chakula na kumwagilia miti na maua. Hizo kazi zote nilikua nafanya mwenyewe kila siku na nilikua nafanya kwa moyo wote.
Unaweza kushangaa mwanaume nawezaje kufanya hizo kazi lakini nilifunzwa nikiwa mdogo na mama yangu mzazi pamoja na dada yangu. Ikafika stage akaanza kunipa kufua nguo za Uncle na mdogo wangu ambaye ni mtoto wa mwisho (ambaye huwa naamka asubuhi kumpikia chai), nikaona haya mazoea yamezidi sasa.
Kuna siku nilikua natoka pale home Asubuhi kwenda mjini kwaajili ya interview na kusaka fursa, wahenga wanasema fursa haikufuati nyumbani unatakiwa ukaitafute. Sasa nikiondoka pale asubuhi mara nyingi anakua amelala na uncle wangu huwa anatoka sa11 au 12. Sometimes kuepusha makazi kama hayo nilikua nakwenda mjini au kwa washikaji kupoteza muda tu.
Aunt wangu akawa anampa taarifa Uncle kwamba huwa naondoka bila kuaga afu narudi usiku. Kuna siku Uncle alinikaripia sana nikamwambia Uncle navyotoka huwa anakua kalala kumwamsha sio busara, napia nikitoka sio naenda kuzurura nakwenda kutafuta kazi. Uncle akasema kama umekua mkubwa humu ndani nenda kapange ili uwe huru. Kama mwanaume niakanza kufikiri namna ya kutoka pale ikiwezekana nikapange nianze maisha yangu ya kujitegemea.
Nikapata wazo tangu nimalize chuo sijawai kwenda home mkoa kusalimia acha niende home nikasalimie wazazi wanipe na baraka. Kuna siku Aunt alinitia hasira sana, ilikua usiku inakwenda saa 2 nikatoka kwenda dukani kununua vocha niliacha simu chumbani. Kumbe wakati nimetoka Uncle alirudi akaniulizia hakunikuta ikabidi apige simu ikawa haipokelewi. Wakati nimerudi nikaona gari ipo uwanjani nikajua mzee karudi naingia ndani namkuta seblen kavimba hatari. Nikamsalimia Uncle shikamoo pole na kazi hakujibu, akaniuliza ulikuwa wapi usiku huu? Maana simu hupokei, kabla sijajibu Aunt akaropoka "huyu alikua kwa kidem chake kule bondeni taarifa zake zote ninazo kazi umalaya tu".
Nikaona hizi dharau sasa nakua kama mtoto nikamwambia Aunt mimi tayari ni mtu mzima hupaswi kunipangia mambo ya kufanya, mimi kama kijana pia nahitaji kuwa na mpenzi na haki yangu naomba uwe na mipaka, nikaenda zangu chumbani. Aunt akasema kama umekua mkubwa si uende ukapange ili uwe huru??, nikajua hapa nishachokwa sipaswi kuendelea kung'ang'ania, akufukuzaye hakwambii toka.
Huyu mwanamke ambaye Aunt alikua anasema kidem changu ndo mama junior wangu mpaka sasa. Ni mke wangu japo sijafunga ndoa ila taratibu zote nimekamilisha kama kulipa mahari, bado ndoa ya kanisani tu. Niseme tumetoka mbali sana from Nothing to something, ni mwanamke anayenipenda sana na kunijari anasifa zote za kuitwa mke. Namshukuru Mungu kwa kuniletea huyu mwanamke kwenye maisha ni moja ya mtu ambaye ameplay part kubwa kwenye mafanikio niliyonayo. Tumebarikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume ana miaka 2 sasa tumwite Junior.
Nilikua kwenye dimbwi kubwa la mawazo sana. Wakati niko room nikawaza jumamosi acha niondoke niende home mkoa kusalimia na pia niongee na wazazi juu ya mustakabali wa future yangu. Kesho yake nikamwaga mama Junior alishtuka sana mbona ghafla? something wrong? nikamwambia NO! nataka nikawasalimie wazazi lakini nitarudi ASAP.
Mama Junior akaomba tusex maana ilikua ni miez 5 toka tuanze mahusiano hatujawai kukutana. Na ile jioni nikaona acha niwaage na hawa akina Uncle wanaweza kufikiri vibaya, nikategea Uncle amekaa seblen nikamsalimia, then nikamwambia Uncle Jumamosi mimi nitakwenda home kusalimia then nitarudi. Uncle akashtuka mbona haraka hivyo kulikoni? nikamwambia ni muda sijakwenda huko ni vizuri kwenda kuwajulia hali wazazi. Uncle akanambia bhasi kesho uende hata Kariakoo ununue vitenge vya mama, nikamwambia kesho ambayo ni "ijumaa" nitakwenda chuo kufuatilia cheti changu hivyo sitoweza kwenda Kariakoo. "Kumbe nilikua na timetable na mama Junior", uncle akatoa hela akanipa kuhesabu ilikua 100,000 cash.
Jumamosi kweli nikaondoka kwenda home jioni nikiwa na bashasha nikafika mkoa nikashangaa jinsi mji ulivyojengeka maana ni miaka 3 ilipita bila kukanyaga. Nikachukua bajaji mpaka home kushuka mama akaja akanikumbatia….
MAMA: "waaoohh mwanangu nilikumisi sana jamani, naona umepungua sana shida nini?"
MIMI: "Mama maisha haya na stress za ajira nitanenepaje?"
MAMA: "umerudi sasa ule kwa bidii, maziwa, mayai yapo yakutosha akatabasamu, twende ndani. "Maana wakati tunaongea haya tulikua nje getini".
Kiukweli nilivyofika home nilifarijika sana moyo wangu ulijawa na furaha sana. Bhasi ile jioni tukala dinna as family, wakati tunakula mama akaongea huyu mdogo wako anasoma science lakini hesabu hawezi zero kabisa, itabidi uangalie namna ya kumsaidia. Nikamwambia mama haina shida kesho nitakaa naye chini tuongee vizuri. Baada ya dinna nikakaa na wazee tukaongea sana kuhusu maisha, wakanitia moyo sana, tukafanya maombi tukaenda kulala.
Kipindi naandika ule uzi "Sitaomba kazi acha niwe jeuri tu" nilikua nimeridhika na maisha tayar sina stress niko home. Ilikua ni kucheza PlayStations na masela wa huku home full raha niko home kwa mama stress za maisha natolea wapi!?. Naamka asubuhi chai ya maziwa, mayai 2 ya kuchemsha ya chienyeji, mkate umejaa blue band. Kama unawazazi jitahidi uwapende wazazi wako wakiwa hai, wazazi wanatuombea sana kwakweli na hakuna anayependa kuona mtoto akiteseka.
Itoshe kusema baada ya kurudi home milango ikafunguka sikukaa muda nikapata kazi.