webnovel

2.Mitafaruku ya familia

kupendwa kwa Lecho na Wakalekye na baba yao zaidi ya wale wingine ,polepole kulianza kuchochea ugomvi baina ya wake wale wengine sita wote wakimwelekezea Veronica lawama za masaibu yao .labda ni wivu walimuonea kwa kutunukia mtoto mvulana huku wao wakijikopa mabanati tu ,jambo ambalo lilifanya Magwada kuanza kualika Veronica katika chumba cha malazi cha mfalme ilihali hao walifungiwa nje . Wazee wajamii walifurika kwa magwa karibu kila siku ili kuona iwapo kutakuwa na njia mwafaka za kusuluhisha matatizo yale kabla ya kutumbukia nyongo.walijitahidi kadri ya uwezo wao si kwa ushauri si kwa kushirikisha kila mmoja katika chakula cha mchana au ata chai ya asubuhi haya yote yalifanyika ile kuisimamisha himaya ya mfalme Magwada.

" Laiti ningalijua hawa wake wengi hivi singewaoa ,wananikosesha amani na utulivu katika machweo yangu mmmmh lazima suluhu ipo." alisikika Mfalme akisema siku moja jioni baada ya kughasiwa na kelele zilizotokana miongoni mwa bibi zake ,eti sababu mmoja kachapa mtoto wa yule mwingine.

Makenzi alipendekeza kwa mfalme siku moja kuwa ili kudumisha amani pale kiamboni ni lazima baadhi ya wanawake wangechujwa pale na kupelekwa mahali pengine ,swala la aridhi ya kuwajengea makao mapya halikuwa tatizo kwani mfalme alikuwa na aridhi kubwa aliyoridhishwa na babake .Wengi wa washauri wake waliunga mkono swala la kuamisha baadhi ya bibi na watoto wa Magwada ,na kujengewa mahali pengine ili amani iweze kudumishwa pale nyumbani.

Kwake Magwada alikuwa na wazo tofauti na mpango kabambe ,Yeye aliazimia kuwatwisha wake zake wote kazi ya muda mrefu na yenye uchovu, ili kuwafanya wanyamaze na inawasaidie kuregesha heshima yao.Ikawa kila siku Magwada anatigiza ganda la kibiriti kwa wake wengine kando na veronica aliye kuwa na mtoto mdongo.Mzee hakuchoka kutingiza kwani alifahamu fika methaali isemayo atafutaye hachoki ,akichoka keshapata, alitingiza viberiti na kwa hakika baada ya mwenzi mmoja boma lake lilijaa wanawake ambao walikuwa wakikibia hapa na pale wakitapisha kutokana na kazi aliyoifanya usiku wa majuma mawili yaliyokuwa yamepita.ugomvi pale nyumbani ulipungua hatua baada ya ile ingine, utulivu ,amani na furaha ikarejea pale kwa mzee Magwada,.

Alikenua na kupiga tabasamu moja kali lililohanikiza faraja ,Angeonekana akiwa mwenye furaha muda kwenda ule. mwingine,ishara ya kuwa kesha shida ushidi kati ya hali tatanishi iliyotishia kuipoka amani pale kiamboni mwake.Veronica na dume lake lililopew jina la Wakalekye kazi yao ilikuwa kula ,kwenda masalani na kulala.Veronika kesha kuwa malikia halisi kwani mfalme alikuwa anaamka na kubarizi katika joto lake karibu kila siku.Wale wengine sita walikuwa tayari washa pewa dozi lao nono na kutulia ,ugomvi na mucene ukawapungua.Palishuhudiwa urafiki wa kufa kuzikana katika ya wake wote saba ,ajabu iliyompata Magwada ,kwani hakutarajia hali hii ingewai rejea miongoni mwao, kwake ushirika wa bibi zake ulikuwa usha harabika la hasha si kuharibika ulikuwa usha tubukia usaa, kama ni kuharibika basi ulikuwa ushapita kiwango cha kurekebishwa, ulibakisha kufanyiwa matambiko ya maziko tu.

Veronica aliendelea kutanuka kiafya,si sura si umbo si urembo uliomfanya muchuchu wake kumdondokea kila jioni kama fisi aliye ona mbuzi kwenye kamba baada ya njaa ya siku ayami.Na urembo huu wote hakuna kile kingemzuiya Magwada kukosa hanjamu za mapenzi kwa kike huyu ,kwani alikuwa kabarikiwa kama mtoto wa kimarangoli kutoka kule kakamenga nchini kenya.Miguu ilikuwa imewanda vizuri ya kumvutia mwanaume yeyote yule ambaye kila alfajiri upiga saluti bila kuamrishwa.

Baathi ya walinzi wa pale nyumbani walianza kudondokwa na mate wakikitanzama chakula cha bosi wao,,wengine hata wangesikika wakisema , " ningalikuwa na uwezo ningalipiga penalti moja la kiisure....",tatizo tu ni kupatikana ,kazi na maisha yangu yangu yote yatakuwa kwisha na ata kuzikwa katika kaburi la sahau.

Magwada alizidi kumpenda Veronica tangia kuchomoza kwa jua hadi kuzama kwa kalenda ,penzi hili likichochewa na bidii yake katika kuchapa kazi, urembo na umbo lake lililokamilika,angalikuwa na mashombo basi angesema ndio wakati hasaa ukoko unaalika maua ,bali kwa utulivu na uelewa wake ,aliidhamini ndoa yake na wanyumba wenzake, mumewe akafurahishwa na tendo hili.

Emilly mke wa mwisho wa mfalime magwada ndiye aliye jifungua wa kwanza ,katika ya hao wengine tano ,kwa bahati za jalali Emilly alijikopa mtoto wa kiume akapewa jina Wakarema.Kutokana na zile hati hati za kujifungua ulie uchovu na maumivu ya uzazi,Emilly alikawia kujifungua kwa muda ufaao na hivyo kuihadhiri afya ya Wakarema ,Bali mkunga aliye kipokea kitoto hicho hakuwa na wakika kama mtoto yu salama.

Kwa sababu hii Mfalme akaamrisha Emilly aangaliwe kwa karibu na mkewe Veronica ,tokea pale Emilly akawa anapokea huduma za kimalikia ,si kusaidiwa kwa kufuliwa nguo,kupikiwa ,kulala vyakula vinono hadi kuwa mhisani wa mumewe kila usiku.Wale wake wengine tano walizidi kupambana na hali zao ,kusukumana na matumbo yalionenepa Kwa kustahimili kilicho ndani yao.

Emilly aliye ona Veronica kama hasidi mkuu na aliyefaa kuzongomezwa ahera,sasa hivi ndio alikuwa amabaki ukuni muhimu wah kuhifadhia moto wakati wa mvua za masika, wakawa marafiki wa chanda na pete ,kila mahali waaandamana ,Mbona hayo mabandiliko yote katika mahusiano ya hao wawili, idhibati tosha kuwa kweli kiatu cha baniani mbaya dawa . .Hatimaye Magwada alipata ulitulivu wa moyo kutoka na amani iliyokuwa ikishuhudiwa katika ka kiambo chake.

Namna magwada alikuwa ametimiza majikumu yake ya unyumba kwa mfululizo,basi vivyo hivyo safari za wake zake zilianza kukamilika mmoja baada ya mwingine wakitengana kwa majima mawili tu iwapo mmoja angechelewa zaidi.wengine wakijifungua vivilana na wengine vijalunga visichana.Vijakazi wa pale kiamboni walikuwa na majukumu mapya kila baada ya juma,si kuviosha vitandiko vya vito hivi ,si kufua mashuka,ya kwashikia watoto. na hata mashuka yaliyo kuwa na shahawa za mfalme wao akijamiana na wake wale wengine hasa veronica.Wengine wakilalamikia maumivu ya uzazi veronica alikuwa akifurahia kumkamua mme wao ,vilivyo .

Magwada alikamuliwa vilivyo ama kwa kweli angelikuwa tui la maziwa basi Veronica angelimaliza na kuwaachia wenzake masanzo