webnovel

sababu kuu

Alicia akaupokea mkono wa Mesel na kupanda juu ya farasi, haraka wakaondoka zao.

kwa upande wa Ecca sasa akawa anazidi kulia

"Bora tuwape eneo watu wenye pesa zao sio wewe!"

"Tafadhali nielewe.. nitalipa nikipata"

"Funga mdomo wako Ecca...""

mtoza ushuru akazidi kufoka

"Unajua kutumia vifaa vyenyewe,unajua?"

akafoka mtoza ushuru kwa hasira

"sasa tumia na ole wako ushindwe.."

akamtupia zeze Ecca na Ecca akaliokota na kuliweka vizuri.Mtoza ushuru akakaa chgni na kufumba macho.

"Nasikiliza Ecca,anza kuimba usinipotezee muda wangu bure"

akasisitiza mtoza ushuru .Ecca akavuta pumzi na kuanza kuimba.

Mwisho akamaliza na kuanza kulia kwa kwikwi

"wow!umebarikiwa sauti Ecc"

akasifia mtoza ushuru lakini ghafla wakaja walinzi wa Nora na kusimama nyuma

ya Ecca.

"ni nani aliyeimba huo wimbo .nani???."

wakauliza kwa ukali mno.

"huyo binti mbele yenu"

mtoza ushuru akajibu haraka haraka .wale walinzi wakamkamata Ecca na kutoka naye eneo lile haraka.Ecca akabaki anatetemeka tu hasa baada ya kuingizwa kwenye baa ndogo isiyo na watu.Mbele alikuwa amekaa Nora akipata kinywaji taratibu .Ecca akapigishwa magoti kinguvu nguvu

"kwanini umeimba huo wimbo?"

akauliza Nora,Ecca hakua na jibu la haraka la kumpa

" nijibuu!!!!!!" akafoka Nora na kumfanya Ecca apate ujasiri