webnovel

Ndo adhabu yako

"Nakutaka sasa hivi Ecca!" Akasema Alex akionekana kutokuwa na utani hata kidogo.Ecca akasimama kwa hofu baada ya kauli ya Alex.

"Hapana tafadhal"

Ecca akageuka akitaka kuondoka lakini Alex akamuwahi na kumtupa kwenye kochi!

"Hii ni dhambi jamani." Ecca akalalamika akilia kwa uoga na kutotaka.

"Mashetani ni viumbe wenye dhambi Ecca."

Alex akajibu akimsogelea Ecca ambaye hakua na ujanja wowote.Taratibu akamvua viatu Ecca na kuvitupa mbali!

"Usifikirie itakuaje Ecca....fikiria nini kitakupata kama utakuwa sio bikra."

Maneno ya Alex yakazidi kuuvunja moyo wa Ecca.Hakutaka kufanya hivyo bila ruhusa yake kabisa.

"Niache!!!!!" Akafoka Ecca na kumpiga Alex kwa glasi usoni.Akataka kurudia tena lakini Alex akamuwahi na kumnyang'anya ile glasi kisha akaitupa mbali.Taratibu akaifuta damu iliyokuwa inamtoka kwenye paji la uso na kuitazama.Ecca akabaki kutetemeka tu akijuta alichofanya.Ajabu,Alex alilamba damu yake.

"Tamu sana Ecca.Unataka nionje na ya kwako?" Akauliza Alex kikatili.

"Hapana,Sama...ha...ni."

"Unataka kwenda wapi?Nenda."

Alex akamuachia Ecca.Ecca akainuka na kutoka mbio.

"Naenda mbali sana na hapa."Akajisemea Ecca.Mbio zikawa ndefu lakini,ajabu akajikuta amerudi pale pale.Alex akacheka na kumsogelea Ecca kisha akambinya mkono.

"Mungu wangu." Ecca akapiga kelele kwa maumivu makali.Alex bado akaendelea kumbinya tu.

"Alex!!!!" Akapiga kelele Ecca.

"Hapo sawa.Lia kwa ajili yangu na sio yeyote."

Akasema Alex na kumfanya Ecca amshangae.Huyu ni mraibu wa kutesa.Alex akamuachia Ecca.Ecca akajitazama na kukiona kishimo kidogo,kucha ya Alex ilipenya.

"Hiyo ni adhabu yako."

Akasema Alex na kuondoka.