webnovel

kuolewa na wewe

Ecca akaelezea kila kitu mpaka Nora akaamua kumsaidia.Mwisho akamuacha na mlinzï mmoja wa kumuhifadhi.

Alicia na Mesel tayari walianza kuwinda huku wakitabasamu .Alicia akajikuta akipata furaha ambayo hakuwah kuipata.

"Asante Mesel ."

"Kwaninh Alicia?"

"Umenifanya nisahau maumivu yote kwa wakati huu."

"Usijali Alicia,naona kuna walinzi "

"Wapi?"

"Pale"

akaonyesha Mesel na kumfanya Alicia ageuke kumtazama.Alikuwa ni Nora akiwa anatazama maeneo ya Godis huku akitabasamu.Alicia akajikuta akitetemeka kwa hasira na michozi kuanza kutoka.

"Mbona unalia mpendwa" akauliza Mesel kwa kutoelewa

"Muuwe yule mtu Mesel."

akasema Alicia kwa hasira.

"Siwezi kumuuwa mtu bila sababu ya msingi ."

"Muuwe !hutaki lete hapa!"

Alicia akakamata upinde na mshale na kumlenga Nora maeneo ya kifuani.

"Siamini kua unataka kuuwa .Najua huwezi ."

akasema Mesel

"Yeye ni sababu kuu kuwa kwanini nimekubali kuolewa na wewe."

akasema Alicia kwa hasira