webnovel

Ajali ndogo

"Nimeitikia wito wako baba."

Akasema Alexander baada ya kupata wito wa King Blooden.

"Sawa,nimekuita hapa nataka utume barua ya wito katika kila ufalme."

"Hata maadui zetu au?" Akauliza Alexander.

"Bila shaka.Kwani unadhani watatufanya nini sisi?" Akauliza king Blooden kimtego.

"Hakuna na hawatokuwa na cha kutufanya. sisi ndio vinara wa wote.Unajua hilo baba." Akajibu Alex kwa ujasiri.

"Nimeelewa"

"Barua za nini lakini?"

"Kesho kutwa kutakuwa na sherehe kubwa mno na ningependa wote wawepo?"

"Sherehe za kuhusu nini baba."

"Tutagawa tuzo kwa nchi yenye mashujaa wengi zaidi alafu pia huu ni msimu wa mauzo ya mafuta na silaha za milipo.Umesahau?"

"Ooh.Ni meelewa sasa.Hapo hakuna yeyote atakayeweza kupinga."

"Naelewa."

"Lakini..."

"Lakini nini Alexander?"

"Kwanini hiyo kazi usimpe mwandishi?"Akauliza Alexander kwa jeuri.

~"Nora" Ecca akaita akisimama kwa mshtuko .

"Ecca..uko sawa?Na mbona unalia sasa.Nini atizo diva wangu?:'"

Akauliza Nora akimsogelea Ecca.

"Tafadhali usinisogelee Nora "

Ecca akafoka na kumfanya Nora ashangae.

"Kwanini?Mbona umenibadilikia ghafla?"

"Tafadhali ondoka.Sitaki kukuona hapa."

"Kwanini?"

"Utanisababishia matatizo mimi.Ondoka tafadhali"

"Ecca tafadhali nisikilize..." Akaomba Nora akimshika mkono Ecca.

"Utaniambia kwanini ulikuwa walia'?" Akauliza Nora kwa upole.

"Kichwa chauma tu wala hakuna tatizo."

Akajibu Ecca akifuta machozi.

"Huo mkono wako umekutana na ajali gani labda?"Akauliza Nora na kumfanya Ecca autazame.

"Hebu nione Ecca"

"Hapana!!!!!!!!" Ecca akauficha mkono wake haraka.

"Nani kakufanyia hivi sasa?"

"Ajali ndogo tu."

"Ajali!Sijui hata kwanini nauliza.Huyu ni kaka,si ndiyo?"

"Aaah...." Ecca akajikuta akipata kigugumizi.Nora akamsogeza Ecca kando