webnovel

Sehemu ya 3: mwanamke mjinga kweli kweli

Hatimaye ni asubuhi tulivu.falme ilipambwa kwaajili ya kuwàpokea vijana wa Sultan.Watu wengi walijaa kwenye ukumbi wa shughuli.

"Aah jamani huku kuzuri."Asteria akasifia baada ya kuwasili akiwa na Abrenda.

"Kaa kwa kutulia sawa wewe?"Abrenda Akasema na kumfanya Asteria akae kimya.

Punde tu msafara ukawasili eneo la tukio.Watu wote walikuwa makini kutazama wanaoshuka.Buti likatangulizwa na hapo akashuka mwanaume mmoja mwenye mvuto wa kipekee.Kwa kumkadilia tu ana umri wa miaka 25.Bado kijana sana.Oh bila shaka huyu ni Arash.Arash akazungusha macho yake, yakagongana na ya Asteria.Akapotezea na kusogea mbele.

"Kaka jamani nilikukumbuka sana."Akasema Abrenda akimkimbilia na hatimaye wakakombatiana kwa furaha kubwa.

"Asteria...."Ghafla Asteria akaitwa.Alipogeuka akashtuka kuona ni Fahyma eti.Inamaana na yeye kaja huku ama.Ndiyo,si kashamuona lakini.Ikambidi amsogelee na kumtazama kwa hasira.

"Eeh jicho gani tena hilo jamani."

Fahyma Akauliza na kumfanya Asteria amtazame kwa muda mrefu.

"Nataka kurudi nyumbani kwetu."Ndiyo kauli pekee aliyoitoa Asteria.fahyma akacheka kwa dharau.

"Mbona njia ya kurudi nyumbani ipo mbele yako."

"Iko wapi?"

"Ile pale."Fahyma akaunyoosha mkono wake mahali alipo Arash ambaye alikuwa akimsogelea baba yake taratibu.

"Una maana gani hasa?"Asteria akauliza.

"Umeiyona ile kofia aliyovaa yule mwanaume,.kamvue kisha uikanyage kwa miguu yako alafu sema nataka kurudi nyumbani.Sawa?"Fahyma akasema.Asteria bila kuchelewa akamsogelea Arash na kumvua kofia kisha akaanza kuikanyaga kanyaga.

"Nataka kurudi nyumbani kwetu!"Asteria akafoka.Watu wote walibaki kumshangaa yeye.Kathubutuje kumvua kofia ya utawala Shahzad mwenye nguvu na roho ngumu kama Arash?

"Umeisha Asteria"Fahyma akajisemea na kutazama tu.

Arash akakunja ngumi kwa hasira na kumsukuma Asteria chini!

"Walinziiiii"Akaita na kumsogeza mlinzi mmoja mwenye mjeledi.Akamsogelea Asteria na kuanza kumpiga.Asteria akabaki tu kulia kwa maumivu makali.Alipigwa viboko vingi sana hadi aliporegea.

"Kaka inatosha!"Abrenda akamvuta Arash maana aliona atauwa bure.

"Arafaaa"Akamuita dada yake mkubwa.

"Ndiyo kaka."Arafa akasogea asikilize maagizo ya kaka yake.

"Lete nembo ya utumwa hapa"Arash Akaagiza na hapo kikaletwa chuma cha moto chenye namba(14). Arash akichukua na kumgeuza Asteria kisha,akashindilia kile chuma bila huruma.

Asteria akalia na kulia lakini wapi.Arsh alipochomoa akakuta tayari alama imekaa.

"Mpelekeni ndani."Arafa Akaagiza.Yeye ndio kiongozi wa kuwadhibiti watumwa wote ndani ya ufalme.Aateria akaburuzwa kwenda ndani.

"Nilikuonya lakini."Akasema Abrenda akiwa na huzuni kubwa.

Asteria akapelekwa kutibiwa kabla hajaanza kazi rasmi ya kutumikia kasri kama mnenguaji maana ndio kazi ya namba yake.

"Saiv kuwa makini,watakuuwa kabisa.Tii maagizo yao"Akasema mwanamke ambaye alikuwa akimsindikiza kwa daktari.