webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Realistis
Peringkat tidak cukup
245 Chs

MAFUTA NA MAJI

"Anawapenda wote wawili?" Akauliza kwa wasi wasi.

"Ha ha ha mama bwana, mimi sijui chochote, unaonaje umuulize mwanao akupe ukweli wote" Derrick akajaribu kukwepa maswali ya mama yake

"Derrick hebu acha kunilaghai ooohh" akamfinya tena kwenye mkono

"Aaaargh mama jamani" akalalama Derrick

"Kama hujui chochote kwa nini ulimleta Aretha na wakati unajua Joselyn atakuja na kaka yako?" Akamuuliza Derrick aliyekuwa akipuliza mkono ambao mama yake aliufinya...

"Nakusikiliza" mama yake akampa sura ya ukakamavu mwanae

"Okay.....okay mama. Mimi nilikuja na Aretha sababu ya kumtia wivu Joselyn. Sina ugomvi na huyo mwanamke bali mimi na yeye ni mafuta na maji" alipomaliza Derrick akanyamaza

"Ulijua kaka yako atakuwa njia panda wakiwa wote wawili hapa,kwa nini haukumjali ndugu yako zaidi ya mipango yako Derrick?"

Derrick akainama " mama nisamehe ila namna hiyo ndio mimi niliona namjali kaka. Nataka ajue kufuata moyo wake kwa mara ya kwanza kwenye maisha yake"

Mama yake akakaa kimya kwa sekunde chache kisha akamuuliza Derrick, "nilimuona Li akitabasamu ulipotaka Aretha aongozane na kaka yako, na yeye anahusika?"

"Mama jamani sijui kabisa kama Li anahusika. Mimi nilijaribu kuwapa nafasi wazungumze tu. Naomba niende Mrs Simunge nitachelewa darasani" akainuka na kutaka kuondoka lakini mama yake akamvuta akae.

"Sikia Derrick yule binti ni mstaarabu kabisa... na si vyema mkamfanyia michezo yenu ya ujana. Halafu kaka yako ni mtu mzima msijaribu kumfanyia mambo. Kama anamtaka mwacheni apambane mwenyewe." Akashusha pumzi kisha akaendelea

"Yule binti anakuchukulia kama rafiki... now heshima hiyo na si kumfanya kama mtoto mdogo unayeweza kumsukuma huku na kule. . Ni mkubwa yule usiutumie upole wake kumkandamiza....umenisikia Derrick Elvis?" Akamuuliza akimtazama usoni

"Ndio mama nimesikia. Nisamehe, nitamuomba na kaka msamaha... imetosha mama naomba niende" akaweka mikono pamoja na kuinamisha kichwa...

"Eeeshhhh..... haya nenda... usisahau jumamosi ni mgeni wangu. Asipokuja najua ni wewe"

"Hehehee umeshampenda mama" akasema Derrick na kukimbia baada ya kuona mama yake akimrushia mto uliokuwa kwenye kochi

"Aaaargh huyu kijana anakufanania Elvis"

******************

Masaa mawili ya kikao yaliyoyoma taratibu, katika ukumbi wa mikutano kila mkuu wa idara alikuwa makini kufuata maelekezo kutoka kwa Edrian Mkurugenzi Mkuu wa SGC pamoja na timu ya wataalamu wa mawasiliano wa kampuni. Linus

"Nafikiri maelekezo haya yatatusaidia utendaji wetu uwe mwepesi kwa sasa. Na kwa wale mlioko site tafadhali fanyeni scanning ya taratibu za oparesheni zote. Wanasheria watamalizia na vinavyopungua. Allan na mimi tutakuwa huko asubuhi kesho. Sina la ziada, nadhani maswali yote yamejibiwa. Niwatakie mapumziko mema, tuonane kesho."

Baada ya kusema hivi Edrian ainuka na kuelekea ofisini kwake. Akafungua jokofu na kutoa maji yake ya limao akanywa na kuelekea kukaa kwenye kochi huku akiangalia saa. Akaona itakuwa vyema akianza safari ya kuelekea kwa akina Aretha mapema asijekwamishwa na foleni.. akaweka vitu vyake na kuanza kutoka.

"Hey Loy fanya arrangement mapema za tiketi, Nitaenda G-Town na S-Town. Allan ataenda K- Town.. Nijulishe ukifanikisha"

Akatoa maagizo na kuingia ofisini kwa Allan

"Hey bro nina sehemu nawahi, nakuomba umalizie hapa. Tuonane kesho... tutakuwa na ukaguzi wetu. Loy anashughulikia tiketi."

"Sawa Bro, jioni njema"

Akatoka Ed akichukua lifti mpaka chini kwenye maegesho binafsi. Akaingia kwenye gari na kuanza safari ya kuelekea Moon street. Alipoingia tu barabarani aliona gari ya rangi ya kijivu ikiwa imeegeshwa pembeni ya barabara. Akavuta kumbukumbu ya jana usiku akahisi inafanana na ile iliyompita kwa kasi na kusababisha ajali ndogo. Akatamani kurudi lakini muda ulikuwa haumtoshi na yeye hakutaka mama yake Aretha amsubirie sana.

Akapiga simu yake.....

"Captain, kama una mtu karibu aangalie njia ya kuingia Lavender, kuna gari naitilia shaka... inafanana na ile ya jana usiku."

Alipokata simu akaanza kuwaza ni kwa namna gani atajaribu kumshawishi mama wa Aretha kuwa yeye ni mtu mwema kwa binti yake.