webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Realistis
Peringkat tidak cukup
245 Chs

ALISAHAU

"Ooooh Rian nisamehe sana, sikujua ingekuwa hivyo" maneno haya yaliambatana na kwikwi za kulia

Edrian akamkumbatia, ile mikono ya Aretha iligusa mgongo wake ambao ulikuwa hauna hata kipande cha nguo. Msisimko ulisafiri kwenye mwili wa Edrian hadi kwenye fahamu zake. Akamrudisha nyuma kidogo Aretha, mkono ukashika kidevu chake na kumuinua

"Retha, unaweza nipatia dakika chache nivae kisha tuongee?" Akamwambia huku kidole gumba chake kikifuta machozi usoni kwa Aretha ambaye alitikisa kichwa kukubali.

Edrian akampeleka mpaka kwenye kochi, akamketisha . Aretha akainama akiminya vidole vyake huku akiomba moyoni Ed asivalie pale

Edrian akaelekea ilipo kabati akatoa pajama zake za kulalia akazibeba kisha akaelekea bafuni huku akimuacha Aretha akishusha pumzi akishukuru.

Alipomaliza akatoka na kujiunga na Aretha kwenye kochi la watu wawili lililokuwepo mle ndani. Harufu nzuri ya manukato ikakijaza chumba kile. Hayakuwa manukato makali bali harufu nzuri yenye kustarehesha ilikuwa puani kwa Aretha.

"Harufu nzuri kweli" akawaza Aretha

Hata alipoketi, bado Aretha aliendelea kuinama huku akifinya vidole vyake..

"Retha, sogea kwangu" Akamuita huku tabasamu laini likionekana usoni kwake

Aretha akasogea, lakini Edrian akamuelekeza alale kwenye miguu yake. Aretha akataka kugoma lakini Ed akamtania "Kama hautaki kulala miguuni kwangu basi nikulaze kitandani" Aretha aliposikia hivyo akalala kwa haraka kwenye miguu yake huku akiangalia pembeni, lakini Ed akamgeuza apate kumtazama vyema kisha akamuuliza,

"Nambie kwa nini ulikuwa unalia?" Edrian akamuuliza huku akichezea nywele zake

"Eeeeh" Aretha akajikuta hajui ajibu nini

Edrian akamtania, "Ikiwa utakuwa hunijibu kila napokuuliza nitakubusu hapa" akaelekezea midomo yake kwenye ile ya Aretha na kumpa busu jepesi. Aretha akafumba macho!

Kabla ya kujibu, meseji ikaingia kwenye simu ya Ed, akachukua na kusoma kisha akaweka pembeni

"Wifi yako anasema chakula tayari, unaenda kula?" akamwambia huku tabasamu likimtoka upande mmoja

Aretha akashtuka kusikia 'wifi' akashangaa"Eeehmm" alipokuwa kwenye mshangao huo midomo ya Ed ikampiga busu huku ulimi ukifanya ziara yake na kumuacha Aretha na miguno ya raha

Akaachia alipoona Aretha akianza kusema taratibu, akamwangalia, naye Aretha akafumba macho! "Utaenda kula?" Akamuuliza

"Na wewe utakuja?" Akauliza Aretha

Edrian akainama akambusu tena mara hii hakuachia. Aretha sasa hakumuacha Ed amkimbie, mkono wake ukamshika shingoni

"Mmhh" Edrian akaachia mguno mara alipoona Aretha akimpokea pasipo kusita, sekunde za mahaba haya zikapita pasi na wao kujua hadi mlio wa simu ikiita ulipowashtua

"That's my sister" akasema Edrian baada ya kumuachia Aretha ambaye sasa alijaribu kujiweka vyema

"Unashuka chini kula au wakuletee huku?" Akauliza Ed huku tabasamu likiwa wazi usoni mwake

Aretha akiwa amefumba macho akajibu "Wewe utakula?"

"Utakapokula wewe na mimi hapo hapo!" Akajibu Ed

Aretha akafumbua macho na kumwangalia Ed ambaye aliinama kumtazama "basi amua wewe wapi tule"

Akachukua simu na kupiga, "baby sisy pole nilikuwa bafu, unaweza kutuletea tu chakula"

Aretha akamwangalia kwa kumshangaa, lakini Ed akajitetea "unataka nimwambie tulikuwa tunafanya nin__" kabla hajamaliza Aretha akamuwahi kwa kumuwekea mkono mdomoni lakini Ed akaubusu

Aretha kainuka haraka kama mtu aliyekumbuka kitu "Rian, huoni Coletha atashangaa kuwa tumekaa wote chumbani?"

Edrian akamwangalia huku akitabasamu "Kwa hiyo hautaki ajue kwamba sisi ni wapenda!!!"

"Aah.. hapana simaanishi hivyo ila_" Aretha akajaribu kujitetea lakini mlango ukagongwa na macho yao yakaelekea huko

Edrian akainuka kuelekea mlangoni wakati huo Aretha akakimbia upesi kuketi kwenye kochi

Mlango ulipofunguliwa, Edrian akarudi nyuma kumruhusu Coletha kuingia

"Nimeona kimya nikajua umeahirisha kula!" Coletha akamwambia Aretha huku akiweka chakula kwenye meza

"Hah...hapana ni..nilisahau" Aretha akajikaanga na kumfanya Ed amtanie

"Alisahau mara alipoingia, msamehe"

Coletha akamwangalia kaka yake kisha akacheka na kumgeukia Aretha ambaye alijikausha kama hakusikia!