webnovel

SURA YA KWANZA

BI. Zena alisimama karibu na dirisha kubwa la vioo akimpungia bintiye mkono kumuaga. Bintiye naye kwa upande mwingine alimpungia kwa furaha akiwa tayari kuondoka.

Baada ya dakika kama mbili hivi, gari lilitoka langoni, Bi. Zena akaachia machozi yamtoke.

Alikuwa amefurahia kwa mwanawe kupata barua ya kujiunga na chuo kikuu, lakini kwa upande mwingine mwito katika chuo kulikuwa kumemwachia donda ndugu moyoni kwa sababu alizojua mwenyewe.

"Mola amulinde na kumwepusha na majanga yote Hellena," alimtolea dua mwanawe akiondoka dirishani.

Aliingia katika chumba chake cha kulala kisha naye baada ya dakika kama kumi hivi akatoka akiwa amevalia nadhifu tayari kuelekea afisini alikofanya kazi.

Baada ya kumwagiza kijakazi aliyekuwa akifagia nje ya kasri lake, naye aliondoka kuelekea kazini kwa gari lake aina ya Land Runner.

"Nimepata barua ya kujiunga na chuo kikuu cha Zogo," alikumbuka alivyomwarifu babake kwa furaha siku aliyopata barua ya chuo, "asante baba, asante mama, asanteni nyote kwa yale mliyonifanyia kuhakikisha kwamba nifuzu maishani."

"Asante nawe mwanangu, tena wewe ndiye binti wangu wa pekee, ningefanya kila lililo la kheri kufanisi maishs yako mwanangu," babake naye alimwambia kwa furaha akimwangalia mamake.

"Ndiyo mwanangu, tunakutakia kheri njema uendako, wewe ndiye nguo ya kutusitiri uzeeni, tena wewe ndiye fimbo yetu ya uzeeni," mamake naye alimwambia kwa furaha kumpa tumaini.

Usiku uo huo mama wa mtu alimchinja jogoo wake aliyekuwa amemfuga kama kitoweo siku ya krismasi, walikula kwa furaha wakizungumza jinsi maisha ya familia yao yatakavyobadilika siku ambayo binti atakuwa kati ya mahafali.

" Siku hiyo, nitamwendea mtumishi wa Mungu, Bw. Roho Chafu aniazime koti lake, kuje kiangazi au masika, lazima nitahudhuria sherehe ya kivuko cha binti yangu, " babake alimwambia kumpa imani akiguguna mfupa wa mguu wa kuku.

"Siku ya krismasi mtasherehekea kwa nini ikiwa m'memchinja," Zena aliwauliza wazee wake kiwatania.

"Ah! Mwanangu," mamake alimaka kwa swali lake, "kuitwa kwako katika chuo kikuu kwetu ni sherehe kubwa hata zaidi ya krismasi."

"Ah mama! Kujiunga kwangu kuipiku siku ya kuzaliwa kwa bwana wetu mwokozi wa ulimwengu Yesu Kristo."

"Ndiyo mwanangu, kwa sababu kwangu mimi siku hiyo huwa haiwi siki ya kuzaliwa kwa mkombozi Yesu, bali kuidhinishwa kwa ibilisi fulani. Siki ya kusherehekea uovu ulimwenguni. Maovu mengi hutokea siku iyo hiyo unayotaja, watu wakashiriki ngono kiholela, mihadarati ya kila aina kitumika, kupotoshwa kwa watu wengi kwa sababu ya maingiliano ya karibu kati ya watu, watu kutoeleana ahadi za uongo kwa sababu ya kukopa senti za kutumia kwa siku moja na mengine mengi."

Walipiga gumzo ya familia kwa masaa mengi mpaka usiku wa manane alipoondoka na kuwaacha wazee wake wakiendelea, mwenyewe wakati huo akiwa na umri wa miaka kumi na minane. Chumbani mwake, usingizi ulimpiga chenga akasalia kugaagaa kitandani akifikiri jinsi maisha yatakavyobadilika pindi tu atakapojiunga na chuo kikuu.

"Aila yangu nzima itanitakia fanaka chuoni kwa sababu mimi ndiye mtu wa kwanza kujiunga na chuo katika ukoo wetu," alijisemea akitandaza tabasamu hafifu usoni, " 'well done my niece' my uncle will congratulate me, he values my mum so much and I hope he will be willing to lend a hand in paying for my fees and indeed he will because we are a family and we have to share our joy together."