webnovel

Sehemu ya 10:kaka na dada

Emma akaandaliwa tayari kwa kuwa mke wa Amarilla.Ndoa haikupaswa kuchelewa hasa pale ambapo Amarilla mwenyew hakuwa na pingamizi lolote lile.Annia akachanganyikiwa asijue cha kufanya.

"Asante sana Zebrana..umenipa fursa nzuri sana kwa kweli.Ukiamka hapa tayari mimi nitakuwa mke halali wa Amarilla."Emma Akasema akiwa kando ya kitanda cha kamba alicholazwa Zebrana.Taratibu akatoka lakini ghafla akajikuta akishikwa mkono wake.Alipogeuka akagundua ni Zebrana.

Haraka akamsogelea na kukaa kando yake.

"Uko sawa wewe?"Emma akauliza akimpapasa kwenye paji la alionekana kumjali zaidi Zebrana.

"Hapa wapi tena jamani."Akajiuliza Zebrana akipepesa macho yake.

"Tuko kwenye ufalme wa Hadas,na mimi naolewa na kijana mzuri Amarilla.Tumepata bahati kubwa sana."Akasema Emma lakini Zebrana mawazo yake yote yakawa kwa mdogo wake Asteria.

"Nitarejea baada ya ndoa.Sawa eeeh?"Akaaga na kutoka haraka eneo. Asteria akabaki na maswali mengi kichwani.Sio rahisi kwa firauni kuamua Amarilla aowe mtu bila sababu za msingi.

Akakaa kwa muda mrefu sana hadi akachoka.Akaamua tu atoke angalau akachungualie tukio zima la ndoa.

"Mh kumependeza ..lakini mbona watu wamejazana sehemu moja?"Akajiuliza lakini ghafla,akapitishwa Emma akiwa anavuja damu nyingi sana maeneo ya mdomoni.Hakuelewa ni nini kimemkuta.

"Emma!!"Akaamua kuwafuata watu waliombeba Emma nyuma ajue hasa kilichomsibu.

Emma akalazwa kwenye kitanda akiwa anatetemeka kama vile kamwagiwa maji ya baridi katika msimu wa baridi kali.Alitamani kuuliza maswali mengi lakini angeweza je wakati yeye ni bubu?

Akashuhudia Emma akikata roho taratibu lakini kabla hajafa.. akaunyoosha kidole mahali alipo Annia na Amarilla.zebrana akawatazama asielewe alikuwa akimaanisha nini.Pale pale Emma akafariki.

Zebrana akajikuta akipagawa vibaya mno.

"Kafa... sasa twende ukaniowe mm."

Annia akasema na kuagiza Zebrana akamatwe.

"Muuweni alafu mukamtupe mbali."Annia akasema na kutoka haraka.Zebrana akachomwa upanga wa kifuani na kutupwa mtoni aliwe na samaki.

Wao wakafunga ndoa na Annia akapewa taji lake la umalkia.Alijawa na furaha sana.Akiketi chumbani kumsubiri Amarilla wafurahie lakini haikuwa hivyo.

"Ulitaka taji na umelipata sasa tufurahie nini.Mimi na wewe tutaishi kama kaka na dada."Amarilla Akasema na kumfanya Annia acheke kwa dharau.

"Eti kaka...! Wewe ni mume wangu.Huo ndio ukweli."

"Kwa hiyo?"

"Tutafurahia usiku huu mimi na wewe."

Annia akataka kumgusa Amarilla lakini akasukumwa mbali kisha Amarilla akatoka.