webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Politique et sciences sociales
Pas assez d’évaluations
245 Chs

YEYE NA CHARLZ

"Mbona uko hapa?" Ed akamuuliza huku akiangaza huku na kule kuona kama atamuona Aretha. Lakini bado alishangaa kuona huyu dada akimuita kama alimfahamu. Aligundua sauti ya yule dada ndio ile ile aliyoisikia kwenye simu yake jana usiku.

"Wewe ni nani hasa?"akauliza tena Ed

Kabla ya yule dada kutoa jibu, simu ya Ed ikaita, akapokea mara moja alipoona ni Derrick aliyempigia

"Bro niko hapa chuoni, kuna jambo kuhusu_" lakini kabla ya Derrick kumaliza Ed akamkatisha

"Derrick nakutumia ramani ya mahali nilipo njoo" akakata simu na akafanya kama alivyomwambia

"Ed naomb_" akaongea taratibu yule dada lakini Ed akamkatisha

"Wewe ni nani na kwa nini uko hapa? Na je Aretha yuko wapi?" Akamuuliza na kuanza tena kuipiga simu ya Aretha ambayo mlio wake ulisikika mle ndani

Yule dada akainua uso na kumuangalia Ed kwa huruma kuonesha alihitaji msaada wake kumfungua. Lakini Ed alianza kupiga hatua kufuata mlio wa simu..! Nyumba hii ilionesha ilikaliwa na watu japokuwa vitu vingi havikuwa na mpangilio kabisa. Nyuma sauti ya yule dada ikasikika na kumfanya Ed kusimama

"Nitakuonesha Aretha alipo lakini rudi kwanza nikwambie kuhusu yeye na Charlz."

Edrian akarudi nyuma na kusimama mlangoni akamuangalia yule dada huku akili yake ikijiuliza nini kinaendelea mahali hapa

"Unataka kumuona Aretha lakini yeye ndie alinifunga hapa na_" Ed aliposikia hivyo akageuka na kutembea akifuata korido

"Ed huyo Aretha na Charlz ni wapenzi wanakudanganya wewe!" Yule dada akaendelea kupayuka maneno kwa sauti lakini Ed hakusimama bali akaendelea hata alipofika kwenye sebule ndogo ambayo ilikuwa na kochi kubwa moja, TV kubwa ukutani meza ndogo na jokofu dogo. Mezani kulikuwa na vipande vya sigara vingi. Ed alipoangalia akaiona simu ya Aretha ikiwa kwenye kochi pamoja na begi lake. Lakini pia kulikuwa na simu nyingine pembeni ya begi la Aretha.

Akasogea ilipo simu ya Aretha akaishika na kuangalia akaona simu zake, lakini kilichomshangaza ni kuona muda aliomtafuta uko sawa na ule ambao namba ya Charlz ilionesha kumpigia na bado ikaonekana walizungumza.

Alipoinua kichwa chake akaona korido nyingine karibu na jokofu akaanza kupiga hatua lakini kabla ya kufika akasikia geti likisukumwa na hatua za watu zikisogea. Akajibanza kwenye ukuta huku akisikiliza sauti,

"Njooni mnisaidie, Aretha anataka kuniua" yule dada aliposikia sauti za wale watu waliposukuma geti akaanza kuita msaada.

Ed aliposikiliza kwa makini akagundua ni Derrick japo hakujua ni nani ameongozana nae,

"Brother" Derrick akaita huku akipiga hatua kuja kwenye sebule

"D acha kuita hivyo kwa sauti" sauti ya kike ilimzuia D

Edrian aliposikia hivyo akasogea na akamuona mdogo wake

"Bro nini kinaendelea hapa na ni nani huyo mwanamke?" Akauliza Derrick huku nyuma yake akifuatiwa na rafiki yake wa kike ambaye Ed alipomuona akamkumbuka

"Sijui lolote, vitu cha Aretha viko hapa na kuna simu nyingine hapo na_"

"Hii simu ni ya Charlz" Derrick akaishika na kumfuata kaka yake ambaye aligeuka kuukabili mlango mliokuwa mbele yake

"Bro tuite polisi au?" Derrick akamuuliza

"Nope, kwa mazingira haya ni aidha tuhusike au Retha na Charlz wahusike, sijui kwa nini vitu vyake viko hapa."

Akamjibu huku akipiga hatua za taratibu na kushika kitasa..

Big brother au tupige chuoni? Angie aliyekuwa nyuma ya Derrick akauliza kwa sauti ya chini

"Watu wengi wakijua tunakuwa hatujasaidia chochote" Ed akamjibu

Akakijaribu kitasa kikafunguka, akausukuma mlango taratibu na kupiga hatua kuingia

Kile alichokiona mbele ya macho yake kilimfanya asiendelee mbele, huku mkono mmoja ukiwa umeshika kitasa

Derrick aliyekuwa nyuma yake akashtuka kwa nini kaka yake aliganda pale aliposimama

"Brother kun_" kabla ya Derrick kumaliza Edrian akageuka na kwa haraka akamsukuma nyuma

"Subirini hapo" Ed akamwambia Derrick kisha akaingia ndani na kufunga mlango kwa haraka akiwaacha Derrick na Angle katika mshangao

Yule dada aliyefungwa kule stoo akaendelea kumuita Ed kwa sauti ya juu.

Derrick alipoona imekuwa kelele akaelekea kule stoo huku Angie akimfuata kwa nyuma maswali yakiwa wazi ndani yao kuhusu Ed kuwarudisha