webnovel

CHOZI LA UNYONGE

Auteur: john_oduor
Urbain
Actuel · 41.3K Affichage
  • 12 Shc
    Contenu
  • audimat
  • NO.200+
    SOUTIEN
Synopsis

Chapter 1SURA YA KWANZA

Mle garini akili haikuwa imetulia, fikra zake ziolikuwa mbali sana na pale barabarani. Bw. Nadama alikuwa akikumbuka majanga mengi ambayo alikuwa amepitia kwa miaka mitano aliyokuwa mshirika wa lile kanisa.

"Lakini bwana wee! Naogopa maneno ya watu," alikumbuka alivyomwambia rafikiye siku moja.

"You cannot prevent a bird feeder from flying in the sky but you can stop it from nesting on your head," alikumbuka alivyojibiwa katikati ya kicheko.

Kicheko kile kilifanya akajiona mdogo zaidi ya mwenzake, alimwangalia tena kwa macho ya uoga. Walikuwa wanatoka matembezini mwendo wa saa mbili za usiku.

"Watasema mchana na usiku watalala, watakayokusimanga hayatajiandika usoni mwako," Bw. Vura aliendelea kumshawishi, "angalia nilivyoendelea kwa huu muda ambao nimekuwa katika kanisa hilo la mwanga.

Alikumbuka jinsi siku hiyo kutoka asubuhi walipoondoka nyumbani kwake, mazingumzo ya mwenzake yalikuwa juu ya mada hiyo moja mpaka wakati wa jioni walipokuwa wakirejea kutoka ziara zao.

"Lakini naogopa kumuasi Mungu!."

"Basi utaendelea kuishi katika umaskini wako."

"Hiyo ni kasumba."

"Si hivyo unavyofikiri, ulitima utakuandama siku zote. Utakuwa unalala na kuamkia umaskini kama mjalaana."

Baada ya maneno yale kila mmoja wao alikaa kimya, Bw. Nadama alikuwa anafikiri jinsi sahibu yake aliamua kumuasi Maulana kwa sababu ya kujipa mali kwa njia mbi. Walipofika nyumbani kwa rafikiye, walikaribishwa kwa manukato na harufu nzuri za vyakula ambavyo vilikuwa vikiandaliwa, alichukua kibaiskeli chake aina ya Hero kilichokuwa kimefungwa vibuyu vya kutembeza maziwa akaondoka.

Moyoni alijua rafikiye hakuwa amefanya uamuzi wa hekima alipoamua kufuata njia mbadala na ile ya uokovu.

"I better die poor than sin against God," alijiambia akipiga darubini dakika chache ambazo zilikuwa zimepita akakumbuka lile gari la kifahari ambalo alikuwa ametembelea.

Alipofika kwake alimpata mkewe Bi. Tabasuri akiwa ameketi nje na wana wao. Watoto wake was walipomuona walimkimbilia na kumlaki kwa furaha, mkubwa kwa jina la Labibu akachukua baiskeli. Walikaa wakipiga gumzo ya kifamilia kisha baada yake kula, watoto waliondoka.

Walipobaki na mkewe ndipo alipomsimulia yale ambayo yalikuwa yametokea.

"Heri wachawi tisini na tisa kuliko mnafiki mmoja," mkewe alimuonya, "huyo ni mnafiki, si rafiki. Mtu anayekujali hawezi kukupa ushauri wa kishenzi namna hiyo, ishindwe..."

Alijaribu kujiondolea zile fikra kwa kutikisa kichwa bila mafanikio, machozi yakamtoka bila kutarajia. Alijiona mpumbavu kwa sababu ya uamuzi ambao alikuwa amechukua

*****

"Stoop!!! Don't kill him," Labibu alitoa ukemi uliowafikia wazazi wake upande mwingine wa nyumba.

Bi. Tabasuri alijizoazoa kutoka kitandani baada ya kusikia sauti ya mwanawe. Alipofika katika chumba chake, aliwasha taa akamuona mwanambee wake amekaa katikati ya kitanda chake huku amevuta blanketi kwa nguvu. Alikuwa ameroa kwa jasho.

"Are you alright?!' mamake alimuuliza akiketi kando yake.

Labibu hata hakuweza kuitikia kwa kinywa, akaitikia kwa kutikisa kichwa, alikuwa anahisi uoga kama mtu ambaye alikuwa ameona kitu cha kuogofya.

"Nini tena usiku huu mwanangu?."

"I ...'ve had sa...me dr...e..a...m,"alimjibu mamake akitetemeka, "tu...li...kuwa msituni na mdogo wangu Guta tukitunda matunda walipotokea."

Mamake alimeikiliza kwa makini zaidi, ndoto iyo hiyo ya kutisha ilikuwa ikijirudia katika familia yake.

"Watu magwanda mekundu ka...ma damu wa...ka...tokea na ku...anza kutukimbiza," aliendelea kumsimulia mamake ndoto yake.

Kwa utaratibu babake alikuja na kusimama mlangoni akamwangalia mkewe, kisha akamgeukia mwanawe. Wote walikuwa wamevalia nyuso za hofu.

"Endelea," Bw. Nadama alimuamuru mwanawe.

"Wa...li...kuwa wamebeba mapanga, tulipokuwa tunakimbia, ulitokea lakini hata ulipotokea penyewe hatukuona, uli...ja...ri...bu kutuokoa lakini kwa bahati mbaya ulijikwa ukaanguka, kisha wale watu wakakufikia tayari ku...ku...angamiza. Ni...lipo...a...ngalia aliyeinua upanga, nilimuona Bw. Vura."

"Mimi...!" babake alimaka.

"Ndiyo."

"Ndipo nilipowaomba wasimuu..."

"Is it not same dream Guta had frequently before his death?!" Bi. Tabasuri alimkatiza mwanawe akimgeukia mumewe.

"Ndiyo, lakini mimi sina nguvu zozote kuikatiza," alimjibu mkewe akigeuka na kuanza kuondoka.

"Wachukulia vipi tukimyembelea Bw. Mhifadhi kesho na kumueleza haya!"

"Kesho nina shughuli muhimu za biash..."

"Shughuli muhimu za biashara," mkewe alimkatiza kwa kumrudishia maneno yake, "kwani hizo shughuli ni muhimu kuliko mwanao? Sio!."

"Si hivyo, vyote ni muhimu lakini ni heri nishughulikie haya Kwanza."

"Chaguo la kwanza ni biashara," mkewe alimwambia kwa uchungu, "he is obsessed with money that he even don't care about us."

Baada ya maneno yale chumba kilikuwa kimya, Labibu alikuwa amemkaribia kabisa mamake.

Pale mlangoni alipokuwa amesimama baada ya kusitisha muondoko wake alikuwa na mawazo chungu nzima, baada ya kuingizwa katika kanisa hilo na rafikiye Bw. Vura, hakuwa anataka kusikia neno lolote kutoka kwa makanisa mengine ndiposa alikuwa anasita kwa mwito wa mkewe kwenda kumuona mchungaji wake wa awali.

"Unaweza kumaliza ugeni wetu kwa mchungaji kisha ukaenda zako," mkewe alivunja kimya, "kwa sababu sitaraji kikao chenyewe kuzidi masaa mawili."

"Nishakusikia Bi. Mshauri, nitaenda ingawa shingo upande," Bw. Nadama alimjibu mkewe kisha akaondoka.

Bi. Tabasuri aliketi kando ya mwanawe akifikiri jinsi mumewe alikuwa amebadilika si kidogo. Aliona tofauti kubwa sana kati ya Nadama waliyefunga naye pingu za maisha na yule ambaye alikuwa akiishi naye kwa wakati huo.

Japo si kama Happ awali ambapo hata cha kutia kinywani walikuwa wakikosa, Nadama wa wakati huo hata alikuwa anapata pesa za kuistarehe familia yake, lakini mapenzi ya baba kwa wana yalikuwa yamepungua kwa asilimia kubwa.

Alikaa pale chumbani na mwanawe kwa dakika thelathini kisha akainuka na kumbusu pajini na kuanza kuondoka, kwa ghafla Labibu alimwangukia na kukamata guo lake.

"Usiniache mama!" Labibu alimlilia mamake, "naogopa."

"Unaogopa nini?!"

"Naogopa kuota tena, naogopa mama!."

"Ni sawa mwanagu," Bi. Tabasuri alimwambia, akarudi nakuketi kando yake.

"Do you think it will happen to him?!"

"Hapana mwanangu," mamake alimpa imani, "hiyo ni ndoto tu, isikutie hofu. Mungu tunayemtumikia atatulinda dhidi ya muovu shetani."

"Ni kweli Mungu hamuachi mja wake, ila siku hizi baba na ibada ni kama giza na mwanga. Kila siku ya Jumapili hutoa vijisababu ambavyo havina manufaa kukwepa kanisa."

*****

Bw. Vura aliegesha gari lake kando ya lango kisha akashuka na kuelekea katika ofisi ya meneja wake. Aliangalia na kuchunguza yale mazingira kwa upole.

"Angalau nami niwe na wafanyakazi namna hii," alijiambia baada ya kuona wafanyakazi walivyoinamia kazi zao, "si Kila wakati 'mi kuwa mtumwa."

Alipofikia mlango wa ofisi aliukomoa kwa nguvu na kujitoma ndani kwa fujo bila hata mkaribisho, Bw. Siga alimwangalia mkubwa wake kwa mshangao na mwenzake uso ukajaa wasiwasi.

"Ah! Bw. Vura, umenishtua," Bw. Siga alimaka akimkaribisha.

"Kwani hukuwa unanitarajia au lazima nikiwa kwa ziara ya kuchunga mali yangu lazima nikujuze mjo wangu?!"

"Si hivyo."

Yule mgeni wa bwana Siga alikuwa amekaa kimya akiwasikiliza wale wawili walivyokuwa wanazungumza. Bw. Vura alimwangalia mzee kwa jicho la dharau, alivyokuwa amevalia suruali iliyochanikachanika na koti lililokuwa na kiraka cha rangi ya zambarau karibu na mfuko wake ndiko kulikofanya mwenzake akamshusha hadhi na kumuona kama si chochote.

"And what is doing here?" Alimuuliza Bw. Siga akimwashiria yule mzee kwa kidole.

"Ni mmoja wa wanabiashara wenzetu," Bw. Siga alijibu baada ya sekunde kadha.

"Wanabiashara! Wanabiashara! Wanabiashara, siku moja utaingiza hapa wevi ukidai ni wanabiashara. Sasa kizee kama hiki tunafanya nacho biashara gani?!"

"Ah! Kijana," yule mzee alimaka baada ya kusikia matamshi ya mwenzao, "huna heshima hata kwa watu wa umri sawa na babako!."

"Hasira ni hasara bwanangu," Bw. Siga alimtuliza bosi wake alipoona anaanza kupumua kwa nguvu.

"Tell him am who," Bw. Vura alimuamuru meneja wake.

Bw. Siga alifanya alivyoagizwa akamjuza mteja wao kuhusu yule ambaye alikuwa amewasili, mzee alimwangalia Bw. Vura kwa muda kama ambaye hakuwa anaamini nafasi ya mnenewa katika kampuni hiyo.

"Nisamehe Bw. Mdogo," yule mzee aliomba msamaha akimyoshea mkono, lakini Bw. Vura alisusia salamu.

"Mshajuana Sasa tunaweza tukaendelea na biashara zetu, tafadhali tupe muda tukamilishe tulichokuwa tunafanya," Bw. Siga alimuomba akimuashiria atoke nje.

"Humu sitoki," alipinga akivuta kiti chake karibu na meza, "lazima nijue mnachotaka kufanya."

"Sawa basi, utakaa usikilize lakini usizungumze," Bw. Siga alimkubalia shingo upande. Aliyeambiwa alimwangalia kwa kijicho lakini hakuwa anaweza kumfanyia lolote kwa sababu zake mwenyewe.

"Tutakulipa Jumatatu baba," Bw. Siga alimuomba yule mzee, "tuvumilie kwa hizi siku ta..."

"Kulipa mzee kama huyu deni!!" Bw. Vura alimkatiza mwenzake, "huo ni ubadhirifu wa hali ya juu!."

"Mwanangu, dunia tambara bovu," yule mzee alimuonya.

Bw. Siga alikuwa amepandwa na mori, alitaka kumtoa nje kwa nguvu lakini akasusia baada ya kuona angepoteza kazi.

"Ni shilingi ngapi?"

"Laki tano."

"Ukitoa pesa hizo utakuwa unafilisi kampuni yangu?!"

"Lakini anahitaji kulipwa, ni haki yake," Bw.Siga alimtetea mteja wake.

"Haki! Haki! Haki, maneno yako siku zote ni yayo hayo," Bw. Vura alimfokea akigonga meza kwa nguvu nusra kuivunja, "hujui haki humu nchini mwetu Gunga ni ndoto, kama hakuna haki katika ofisi zetu za juu, huyu mzee ni nani nimtendee haki."

Kwa ghafla Bw. Siga alicheka kwa sauti kubwa ikiyosikika mpaka nje ya ofisi hiyo, wenzake wakaangaliana kisha wakamgeukia. Hasira ilikuwa imemzidia Bw. Vura, alimuona mwenzake kuwa mbadhirifu.

"Nini cha kuchekesha?!" Alimuuliza akionekana aliyeghadhabika.

"Unaongea kuhusu ukosefu wa haki, unataka haki ipatikane vipi ukiwa mwenyewe si mhaki!"

"Kwanza hayo mambo ya haki ns mhaki tuyaweke kando, alifanya nini kugharimu kiasi hicho cha pesa?!"

"Amekuwa mwanabiashara mwenzetu kwa miaka mitatu sasa. Tumekuwa tukipokea lori za mawe kutoka kwake tukiendeleza shughuli zetu za ujenzi. Ni kwa muda wa miaka mitatu amekuwa akizungushwa humu mpaka leo."

"Mawe tu! Kwani yana madini yapi kugharimu pesa hizo; dhahabu, almasi, fedha au shaba?!"

Meneja wake alishindwa namna ya kumueleza akubaliane naye kwa kile alichotaka kufanya. Alijua kwa sababu ya tamaa, mwenzake aliona ugumu moyoni kutoa kiasi hicho cha pesa.

Yule mzee pale alipokuwa ameketi aliyapima maongezi ya wawili hao kwa mizini.

"Lakini mwanangu kuna ubaya gani nikilipwa!" Yule mzee alimuuliza kwa upole, "kuna wenzako ambao wanahitaji pesa hizo. Mawe yenyewe yamekuwa adimu lakini huwa nafanya chochote kuhakikisha m'meyapata, sa' sioni ubaya wowote nikifidiwa."

"Umeamua kunimwagia shida zako za nyumbani."

"Si hivyo, lakini pesa hizo zina matumizi yake, hata wenzangu tulosherikiana nao washaanza kuniona mjanja sifa ambayo similiki hata nukta moja."

"Kwa nini tusimpe anachodai," Bw. Siga alimtetea yule mzee baada ya kusikia malalamishi yake.

"Ni sawa mzee, kujia pesa zako baada ya wiki tatu," Bw. Vura alimwambia, "lakini lazima utatuachia kiinua mgongo."

"Sawa mkubwa," mzee aliitikia kwa sauti ya chini akiinuka tayari kuondoka.

Bw. Siga alimwangalia alivyokuwa anaondoka akatambua kwamba hakuwa na furaha, aliondoka lakini alikuwa akinung'unika. Alipofika mlangoni alimwangalia akatikisa kichwa kisha akaondoka, moyoni aliona mwajiri wake hakuwa amefanya vema.

Pale alipokuwa ameketi, Bw. Vura aliinuka akaenda karibu na dirisha kuchungulia nje, akamuona yule mzee akitoka nje ya lango kisha akarudi alipokuwa ameketi.

"Kwa nini tusiyapuuze malipo hayo, hicho ni kiasi kikubwa sana cha fedha."

"Lakini biashara huwa haifanywi hivyo."

"Hayakuonekanii kwamba tutakuwa na nakisi kubwa sana katika akaunti yetu iwapo tutatoa pesa hizo!."

"Lakini hiyo si haki, amekuwa mwaminifu kwa kututumikia. Ni heri nasi tuwe waaminifu wakati wa ma..."

"Mara haki...uaminifu," Bw. Vura alifoka, "utafuata nitakayokuambia au..."

"Ndiyo, nitafuata lakini mengine unayokusudia kufanya si halali."

"Wewe nisikilize, utakachofanya ni kuficha stakabadhi zote zinazoonyesha kumekuwa na biashara kati yetu na kizee kile."

"Atatupeleka kortini."

"Atakuwa amejichimbia kaburi mwenyewe."

"Kisha tukishafanya hivyo?!"

"Kortini tutapeleka laki mbili kunyosha mkondo, ni heri kuliko kuharibu pesa hizo."

"Unafahamu kwamba maingiliano kati yetu na wateja yanaweza kukuza au kuporomosha hii kampuni. Watu wakishasikia ambayo yametokea hawatatuamini tena na wala hawatataka kufanya biashara nasi."

"Hilo lisikutie shaka, simba asiye na meno hata ukimpa mnofu hautamfaidi chochote."

"Bwana wee!!! Usiseme hivyo, midomo ya watu hutoa sumu na dawa mtawalia, maneno ya watu yanaweza kukukuza au kukuporomosha."

"Nishashiba na semi zako, we fanya nilivyokuagiza kisha yote ya baadae niachie. Sijapata kuona mwanaume muoga kama wewe, ni heri ungezaliwa mwanamke."

Bw. Siga hakuweza kujibizana naye tena, mwenzake kwa hamaki akasukuma kiti mpaka mlangoni.

"I think is clear," Bw. Vura alitoa kauli yake ya mwisho kisha akaondoka.

Mle ofisini alibaki akiwazia maongezi ambayo yalikuwa yametokea kati yake na bosi.

"Mwenye nguvu mpishe," alijiambia kwa sauti ya chini akichukua kalamu na kuanza kujaza fomu fulani ambazo zilikuwa zimezagaa pale mezani, "heri niitwe muoga lakini niwe namtendea haki mwanadamu mwenzangu."

Baada ya kazi yake pale ofisini, alitoka akaenda kuangalia watendakazi walivyokuwa wanaendelea na kazi zao. Kila alipopita aliwapata kimya, walikuwa wakizungumza na vifaa vyao vya kazi.

Vous aimerez aussi

audimat

  • Tarif global
  • Qualité de l’écriture
  • Mise à jour de la stabilité
  • Développement de l’histoire
  • Conception des personnages
  • Contexte mondial
Critiques
Pleurage! Vous seriez le premier commentateur si vous laissez vos commentaires dès maintenant !

SOUTIEN