webnovel

Sehemu ya 9: Shetani au binadamu?

Asteria akamfuata yule mbibi nyuma ambapo akampeleka kwenye chumba maalum kwa kuosha vyombo.Vyombo vilikuwa ni vingi mno.Ni vile vyote ambavyo vilikuwa vikitumika katika kasri kuu.

"Fanya haraka uoshe hivyo vyombo.Nikirudi hapa nikute vimeisha."Akasema yule mbibi na kutoka.Asteria akaanza kuosha vyombo lakini ghafla,akajikata.

"Aah;!!!!"Akaugulia maumivu lakini hakuna namna.Akaendelea kuosha vyombo.

"We mwehu huoni kama unachafua vyombo na madamu yako."Akasema yule mbibi kwa hasira.

"Njoo nikupe dawa ya kukata hiyo damu."Akasema yule mbibi.Asteria akamsogelea na kumpa mkono ampake dawa hiyo.

Yule mbibi akamtazama Asteria kwa muda mfupi kabla hajatoa kisu na kumchana kwa nguvu.Jeraha likawa kubwa lenye kuvuja damu.

"Tulia mjinga wewe."Akafoka na kutoa kimkoba kidogo chenye unga unga kisha akamminia.

"Aaaaaaaah!"Asteria akapiga kelele akigala gala chini kwa maumivu makali sana.Ule unga kazi yake ilikuwa ni kuchimba chimba kile kidonda.

"Amka na ukafue nguo huko."Akasema yule mbibi na kumvuta Asteria kwenda naye mtoni.

"Aya ufue."Akasema.Asteria alipogusa tu maji yalikuwa yakimuwasha mno.Akatoa mikono yake haraka.

Kwenye kasri kuu, Sultan Molvandra akaletewa umbea na Zuleykha kuwa Asteria anafanya mpango wa kutorokea ngome jirani habari ambayo sio ya kweli.Bila shaka kuna mtu amemtuma.Sultan akachukia kugundua hilo.Akatuma wanajeshi Magiri wakamuuwe Asteria bila huruma.

"Hapana, lazima niende nikamsaidie Asteria."Hadija akajisemea na kutoka haraka eneo lile.

"Nenda mkafe wote huko huko."Zuleykha akajisemea na kutoka haraka eneo lile apeleke umbea mwingine.

Asteria akiwa anafua ghafra akaguswa bega na kugundua ni mmama mmoja mstaarabu kweli kweli.

"Hujambo mwanangu?"Akamuuliza.

"Sijambo mama."Akajibu akitabasamu.Yule mmama akakaa kando ya Asteria ili wapige stori angalau.

"Unaonekana mrembo... inaonekana Watu wanakutumia sana."Akasema yule mama mtu mzima.

"Hapana bwana...mimi sijawahi hata kuwa na mwanaume kwenye maisha yangu."Akasema Asteria akiendelea kuosha vyombo.

"Kwa hiyo wewe ni bikira?"Akauliza yule mmama.Asteria akakubali kwa kichwa tu.

"Aah.... Asteria nikikutazama naona kabisa unapaswa kuwa malkia."Akasema na kumfanya Asteria acheke.

"Aah mimi wala sina hiyo ndoto.Nitakuwa malkia wa nani mimi."

"Arash...utakuwa malkia wa Arash."

"Eti Arash...wala sitegemei."

"Niamini mimi Asteria..unasifa kubwa mno ya kuwa sultana."Akasema lakini ghafla,wakaibuka watu kutoka majini.Kabla hawajagundua chochote...yule mmama akakatwa upanga wa tumbo.

"Asteria kimbia...wewe unapaswa kuwa sultana wa hili taifa..."Akasema yule mmama na kufariki papo hapo.

"Aah!"Asteria akakimbilia ndani na kufunga mlango ajiokoe.Hawa ni wanajeshi wa kifalme.

Mlango nao ukavunjwa na watu kuingia ndani.