Shekhe akaletwa tayari kwa kumtibu osman.
"Huyu katupiwa jini hatari sana tena shoga.Itabidi atolewe nje ili tujue nani aliyemtumia."Shekhe akasema na kumfanya sultan Molvandra aite watumishi wote wa kasri.Jini akatolewa akiwa anapiga kelele za kuomba msamaha maana alikuwa akiteseka kwa kusomewa dua.
"Unaitwa nani?"Shekhe akauliza.
"Naitwa jini Jinaah."
"Unatokea wapi wewe na kwanini umtese Shahzad Osman?" Akauliza shekhe.
"Natokea Tanganyika na nimetumwa na mkuu wangu kumtesa huyu kijana."Akasema Jinaah na kumfanya sultan Molvandra ainuke.
"Nani huyo aliyekutuma.?Mtaje!!!"Sultan Molvandra akatoa amri.
"Yuko hapa hapa mkuu wangu mbona."Jini Jinaah akasema na kumfanya kila mtu ashikwe na shauku ya kumjua ni nani huyo.
"Muonyeshe."Shekhe akasema na kumfanya jini Jinaah anyooshe kidole chake.Kila mtu akashangaa baada ya kidole kuelekea alipo Asteria.!
"Huyu ndio mkuu wangu.Yeye ndiye aliyeniagiza kumtesa Shahzad Osman."Jini Jinaah akasema na kumfanya Asteria ashangae.
"Muongo wewe.Mimi sijamtuma jamani.Anadanganya." Asteria akajitetea lakini Arafa akamsogelea na kumpiga kofi zito.
"Tena usithubutu kabisa kuongea chochote kile.Baba huyu apate adhabu kali."
Arafa akasema akiwa amekasirika mno.
"we mtumwa umethubutu vipi kumroga kijana wangu?"Akafoka sultan Molvandra.
"Adhabu yako utapelekwa kwenye kasri la mtoni."Sultan Molvandra Akasema na kumfanya Asteria ashtuke.
"Sultan nisamehe tafadhali."Asteria akaomba msamaha.
"Nishakusamehe hapo."Sultan Molvandra Akasema na hapo Asteria akakamatwa na kufungwa kitambaa cheupe machoni.
Abrenda akamtazama dada yake na kupewa ishara ampeleke Asteria mahali husika.Akamchukua mpaka nje ambapo akamuingiza kwenye gari la farasi na kutoka naye haraka eneo lile.
"Namuhurumia sana huyu binti.Hakuna mtu aliyewahi kwenda kule na akatoka akiwa hai."Akasema mtumishi mmoja.
"Ujinga wake,nani alimwambia amroge Shahzad.Afe tu."Mwingine Akasema na wote wakaendelea na shughuli zao.
Msafara ukafika hadi kwenye mto mkubwa mno ambapo Abrenda akamteresha Asteria na kumfumbia macho.Hapo akauona mto mkubwa mno ambapo katika kati yake lilijengwa kasri kubwa vibaya mno la rangi nyeusi.
"Nataka unipeleke ng'ambo."Abrenda Akasema na hapo mvushaji akawavusha.
"Nataka umtese huyu Kisawa sawa hadi ajute kwanini alizaliwa.Umeelewa?"Akasema Abrenda akimueleze mbibi fulani mwenye umri wa miaka kama 76 hivi.
"Sawa sultana usiwaze ndio kazi yangu hii."Yule mbibi akasema.Abrenda akageuka na kuondoka zake.
"Nifuate wewe."Akatoa amri yule mbibi.