webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Real
Sin suficientes valoraciones
245 Chs

FIKIRI VYEMA

"Hello mama" Edrian aliita mara tu simu ya mama yake ilipopokelewa.

"Mwanangu uko barabarani eeeh?" Mama akamuuliza mara aliposikia mtikisiko wa sauti yake

"Ndio mama, narudi nyumbani." Edrian akamjibu na kutaka kuendelea lakini kabla hajafanya hivyo, mama yake akamwambia

Siku ukioa utawahi nyumbani maana nani anataka mume ambaye ni mlevi wa kazi"

"Hahahhaha mama umeanza kunisema. Jana nilipokuja na Retha ulinisifia kuwa napenda kazi yangu!!!....au tuseme... Akajitetea Edrian

"Aissshhhh...usije ukamtesa mke utakayemuoa buree" mama akamkatisha

"Tena hilo ndio haswaa limenifanya nipige simu muda huu" Edrian akamwambia mama yake

"Mmmmhhh kuna nini tena mwanangu" akauliza mama kwa wasi wasi

"Mama" akamuita wakati huo alisimama mbele ya geti la nyumba yake akisubiri mlinzi afungue geti. Mama yake alinyamaza kimya akimsikiliza.

"Tulipokuja juzi nilikwambia kuwa nitakuwa na Retha kwa jasho au kwa damu" akampungia mkono mlinzi na akaingiza gari ndani

"Ndio mwanangu, kuna mabadiliko?" Akauliza mama ambaye sauti yake ilibeba umakini wote

"Hapana mama, hakuna kilichobadilika isipokuwa kuna hatua ya haraka nianze nayo.." akashusha pumzi na kuendelea

"Jumamosi naomba ukaonane na wazazi wa Retha, hasa mama yake."

"Eeeehmm" mama akashtuka kisha akauliza

"Kumuona kama kumposa binti yao au?"

"Kama inawezekana kumposa siku hiyo basi ufanye hivyo mama" Edrian akajibu na kuegemea sehemu ya kuweka kichwa kwenye kiti ndani ya gari yake. Akaamua asishuke mpaka amalize maongezi

"Mwanangu aa. .hii ni aaahh oooh Mungu wangu.." mama sasa alitoka kwenye mshangao na kigugumizi cha ghafla kikampata

"Mama unalia au?" Edrian akauliza mara aliposikia sauti ya mama yake ikimezwa na hisia za machozi

"Aah..mwanangu n..n..nimeshangaa lakini nina furaha na wasi wasi kwa wakati mmoja" Mama akajikaza na kumjibu kijana wake

"Wasi wasi?" Edrian akashtuka

"Mwanangu mna muda mfupi sana na huyu binti, una hakika hatua hiyo sio ya haraka sana?" Mama akauliza pasipo kumficha wasi wasi wake Ed

"Mmkhhgh...Mama nataka kumuoa Aretha. Nina hakika kupita hata hisia zangu.. nakuomba jumamosi uonane na mama yake" Edrian akamwambia mama yake kwa uthabiti, mama akashusha pumzi na kumuuliza tena

"Kuna kitu maalum tutakizungumza napaswa kufahamu?"

Edrian akatabasamu "Nina safari wiki ijayo, nitakuwa nje ya nchi kwa wiki mbili"

"Mmmmhhh" mama akaendelea kumsikiliza

"Nataka nisafiri na Retha" Edrian akamwambia

Mama akanyamaza kwa sekunde, "mama" sauti ya Ed ilimfanya aendelee

"Mwanangu, nimeelewa, sasa nitaongea na mjomba wako na shangazi wanishauri na kama itafaa tutaenda wote"

"Asante mama. Nakuhakikishia mama nafanya hivi walau kumpa nafasi Retha apate ahueni kwani kuna mambo mazito yametokea ambayo hata mimi yameniathiri."

"Kuna nini kimetokea tena.?" Mama akauliza kwa mshtuko

"Hahaa mama usiwe na wasi nitakwambia ila kwa sasa naomba nikapumzike nina kazi asubuhi mapema kesho" akamwambia mama yake huku moyoni akishukuru kuwa aliomba kwa Inspekta Sunday tukio lile lote lisizungumziwe kwenye vyombo vya habari mpaka uchunguzi utakapokamilika

"Edrian" mama akamuita

"Naam mama" akaitikia

"Usifanye kitu chochote cha kuharakisha, fikiri vyema mwanangu"

Edrian akatabasamu "sawa mama. Asante"

Maongezi yalipomalizika Edrian akashusha pumzi na kisha akafungua mlango na kutoka.

Mara alipoingia ndani, akakutana na ndugu zake wote wakiwa sebuleni wakiangalia runinga. Derrick aliketi karibu na Li huku Coletha akiketi karibu na kochi lililotazamana na mlango wa kuingia jikoni

"Kaka, karibu" Coletha akamwambia Ed mara tu alipomuona akiingia huku hatua zake zikiishia kwenye ngazi ya kwanza kuelekea chumbani kwake

Walioomaliza kusalimiana, "Naomba tuonane mara moja huko juu" Edrian akamwambia Li na Derrick kisha akapiga hatua kuelekea juu

"Na mimi nataka nijue kaka Li" Coletha akalalamika

"Hahaha haya yanaitwa mambo ya kiume pacha" Derrick akamwambia huku aliinuka

"Kaka Li nije" Coletha akamsihi

"Ukija si unamjua kaka yako, pamoja na kuwa anakupenda atakutoa nje. Baki hapo hapo nitakumegea"

"Eeeh basi sawa kaka yangu nitakusubiri"