webnovel

chapter 13

Nzagamba anarudi nyumbani na kuona kaniki zinazotengenezwa nguo za bibi harusi zikiwa zimeanikwa " haya kaingiwa na nini tena mama,na hizi nguo si nilimwambia azichome" anaongea kwa nguvu asira zikimjaa "mama,mama" anaita lakini kimya 'atakuwa kaenda wapi' anawaza.anaingia nyumbani kwake na kutoka,anaenda nyumba nyingine anayolala mama yake anaangalia bado hamuoni bibi sumbo.

Anazunguka nyuma ya nyuma anamuona bibi sumbo akiwa amekaa chini ya mti,anamfuata "unafanya nini mama,na kwa nini zile nguo hujazichoma" anauliza hata kabla hajafika " hiyo ndio salamu mwanangu" anamuuliza akimwangalia.

nzagamba anafika na kushangaa zaidi kumuona mama yake akiwa na kisonzo chenye shanga akitengeneza urembo anaotakiwa kuvaa mwali " mama unakichaa hivyo vyote vya nini?" anauliza hasira ikimpanda zaidi kwani hizo shanga alinunua mwenyewe kwa ajili ya mkewe mtarajiwa lindiwe na alitaka mama yake avitupe vyote baada ya uchumba wao kuvunjika " na mtengenezea mkamwana wangu bangili, si ni afadhali sikukusikiliza,kwa Mambo ya ghafla kama hivi tungefanyeje" anaongea bibi sumbo akiendelea kutunga shanga zake. pwaa! kisonzo kilichokuwa na shanga kimezagaa chini na kumwanga shanga zote " unafanya nini?" anauliza bibi sumbo akisimama alipokaa.

"kwa sababu hutaki kukata tamaa na kuamka kwenye ndoto zako nataka nikusaidie Leo" anaongea nzagamba akiondoka

"unataka kufanya nini" anauliza bibi sumbo akiinama na kuanza kuzoa shanga pale chini.

" naenda kuchoma na zile kaniki kama itakusaidia kuachana na mawazo yako".

" Nimepokea posa Leo" anaongea bibi sumbo na kumfanya nzagamba asimame na kugeuka kumwangalia mama yake " umesemaje?" anauliza akirudi alipo mama yake

" ndio,nimepokea posa Leo, najua hutaamini kwani hata Mimi sikuamini ila ni ukweli na kesho tunaenda kumuona msichana"

Nzagamba Anacheka kwa nguvu na kumfanya mama yake kutokuelewa maana ya kicheko hakikuwa Cha furaha " unazeeka vibaya sana mama yangu mpaka unashindwa kutofautisha ndoto na uhalisia"

" kwa hiyo unaniona Mimi nachanganyikiwa au"

" kama huchanganyikiwi basi Mimi ndio nachanganyikiwa"

" usijali kama unaona Mimi naota subiri kesho twende tukamuone Binti"

nzagamba anamwangalia mama yake usoni na kugundua kuwa atakuwa hataniii

" Nina uhakika huyo Binti atakuwa na matatizo au familia yake yote Ina matatizo wanaamua kututupia sisi zahama,ila msimamo wangu ni Mmoja tu sitaki kuoa hata kama Binti akikubali,kwa hiyo mama utaikataa hiyo posa kabla sijakuaibisha zaidi" Hali hii haiamini kabisa nzagamba kwani anajua wazi kabisa Amna msichana atakayekubali kuolewa na yeye na hata kama akikubali yeye hayuko radhi kumuoa Binti wa watu na kumfanya ateseke maisha yake yote bado Mbele atapata watoto nao pia wataingia kwenye mateso hakuwa radhi kuishi akiona hilo.

" Mimi ndio nimesema utaoa kama hutaki utanikuta nimejining'iniza juu ya mti huuu,na kuhusu Binti usiwe na wasiwasi kuwa atakuwa na matatizo kwani mtu aliyeleta posa namuamini sana" anasisitiza bibi sumbo akimpatia kijana wake vitisho ' nikimpata aliyechochea moto huu atanijua Mimi nani' anajiwazia nzagamba kwa hasira kwani yeye alishakubaliana na Hali halisi ya maisha yake na alikuwa na uhakika kuwa hata mama yake atakuja kukubaliana tu na hilo siku Moja lakini Kuna mtu amekuja na kutia chumvi kwenye kidonda.

"Nina uhakika huyo Binti atakuwa hajui Hali yangu mama, Nina wasiwasi kwamba anaweza akajua kesho akavunja uchumba. mtu atakayeteseka na kuanza kuuguza kidonda ni wewe mama ,kwa hiyo tafadhali mama usijipe matumaini" nzagamba anaamua kumpoza mama yake kumpunguzia maumivu atakayoyapata baada ya Mambo kuharibika.

" usijali kuhusu hilo Binti anajua Kila kitu kuhusu wewe na kakuchagua mwenyewe Cha pili Mzee Shana hawezi kuleta posa ambayo itavunjika kwani ataaibika unamjua huwa hapendi kudhalilika kabisa"

" Mzee Shana ndio kaleta posa!" anauliza nzagamba kwa mshangao kwani Mzee Shana anabinti Mmoja tu nae kachumbiwa au uchumba wa sinde umevunjika ndio kaamua kumuozesha kwake anawaza nzagamba akisahau kabisa habari ya tulya kwani aliisikia mara Moja tu na hakutaka kuifatilia.

" ndio maana nimekwambia unaoa mwanangu kwa uhakika mwaka huu mizimu imetusikia" anaongea bibi sumbo akinyanyua mikono juu kuonyesha ishara ya kushukuru akiwa na tabasamu usoni .

" kwani uchumba wa sinde umevunjika?" anauliza nzagamba akiwa kwenye Hali ya kutokuelewa.

"sio sinde,ni mpwa wake Mzee Shana, kasema katokea katika himaya ya wafugaji huko,ni mtoto wa mdogo wake Mzee Shana nani vile jina lake yule mtoto" bibi sumbo anaanza kufikiria jina la mama yake tulya " zunde,zunde ndio jina lake namjua vizuri yule mtoto alikuwa mzuri kweli kweli kama na Binti yake Yuko kama mama yake utakuwa umepata mke mrembo kweli,Tulya hata jina lake ni zuri pia"

Nzagamba anakumbuka kitu baada ya kusikia jina la tulya,siku ya sherehe ya matambiko aliwasikia vijana wengi wakimzungumzia na kilinge kusema ni binamu yake asiyetaka kuolewa.

" Yule Binti kichaa!" anaongea nzagamba kwa sauti kubwa iliyojaa mshtuko.

"kichaa?kwani unamjua?" bibi sumbo anamuuliza baada ya kuona mshtuko wa kijana wake .

" hapana sio hivo"

" eleza vizuri,hapana unamjua au chizi" bibi sumbo anaanza kupandisha Mori akijua Mzee Shana anataka kumwozesha chizi kijana wake,hata kama ana matatizo bado kama mama anataka kilicho Bora kwa mwanae.

"hapa sio chizi na hapana simjui,ila nilisikia vijana wakimzungumzia siku ya tambiko" anaeleza

" basi atakuwa ni mzuri kama vijana wote wamechanganyikiwa juu yake ukajiandae kwa ajili ya kesho"

nzagamba anaitikia kwa kichwa akiondoka,kichwani akiwaza nini kitakuwa kinaendelea mschana ambaye alikuwa hataki kuolewa Leo ghafla tu anataka kuolewa tena na yeye kati ya vijana wote hapa Kijijini na kwa maelezo ya kilinge hakuwa radhi kuolewa Leo wala kesho imekuwaje Sasa lazima Kuna kitu.

Anaamua jioni kwenda kwenye kikao Cha vijana wanapoongea Mambo mbalimbali lazima atajua kinachoendelea.

Tulya amelala siku nzima usingizi usije mbavu zimeanza kuuma kwa kugeuka kwenye kitanda kilichotandikwa ngozi,Giza linazidi chumbani na kuona miale ya mbalamwezi ikipenya na kuingia chumbani kwake,sauti za fisi wakipiga makelele kujidhihirisha uwepo wao Kuja Kijijini kula mifupa zikisikika kwa ukaribu kabisa zinamjulisha kuwa siku imeenda.

Anaamka kwa kujikongoja na kushusha miguu yake chini ya kitanda nakuanza kutembea kuelekea njee akiwa peku miguuni kwani anajua mwili wake hauwezi hata kubeba viatu vyake vya ngozi, anapiga hatua chache na kupamia kitu kinaanguka kutokana na giza haoni hata anapoganyaga anapiga hatua nyingine na kukanyaga maji hapo anagundua kuwa kapamia kipeo Cha maji alicholeta sinde mchana bila kujali anaendelea kutembea na baada ya hatua chache kidole chake Cha mwisho kinapita karibu na nguzo inayoshikilia nyumba hiyo na kujiburuza anatoa ukelele wa maumivu akichuchumaa chini kushika kidole chake mara mlango unafunguliwa anaingia sinde akiwa na kandili anamuona tulya akiwa amechuchumaaa chini

" umeamka,nilijua bado umelala nikaona niletee kandili usikae gizani" anaongea akimfuata alipo.

" si ungeleta mapema kwani jua limezama saa hii unaona Sasa" anaongea tulya na kuanza kulia kwa nguvu akipata sababu ya kumtoa machozi.

" khee! unalia sababu nimechelewa kuleta kandili?" sinde anauliza kwa mshangao

" nimepamia nguzo na kidole changu kinaumaa" kilio Chake kinazidi kuongezeka.sinde anamwangalia na kutamani kucheka lakini anabana kicheko chake akijua tulya atalia zaidi,anaweka kandili kwenye kibao kilicho juu ukutani ambao ni maalumu kwa kuwekwa kandili Ili iangaze nyumba nzima na kumfuata alipo " lete nione" anainamana na kushika mguu wake mkono wake mwingine unashika kidole "hiki ndio kimeumia" anauliza.Tulya anaruka na kulia zaidi.

Sinde anashindwa kubana kicheko chake safariii na kucheka kwa nguvu huku akikaa chini " pole,nyamaza" anampa pole akiendelea kucheka.

"Unanipa pole huku unacheka ndio pole gani hiyo" anauliza huku akifuta machozi yake.wote wanakaa wakiegemea ukuta baada ya kimya kifupi tulya ananyamaza kulia na anaonekana Yuko vizuri kidogo.

" haya unajisikia vizuri Sasa" sinde anamuuliza akimwangalia usoni na tulya anaitikia kwa kichwa,sinde anaanza kucheka tena na kumfanya tulya kumpiga.

" acha,kinachokufurahisha nini?" anamuuliza nayeye akianza kucheka wote wanacheka na baada ya vicheko vyao kuisha kinapita kimya kirefu Kila Mmoja akiwa na yake kichwani.

" Umefikia muafaka gani?" sinde anavunja ukimya,tulya anavuta pumzi ndefu na kutikisa kichwa chake kikienda kushoto na kulia " utakataa tena?" sinde anamuuliza akitoa mgongo wake ukutani na kugeuka mzima mzima kumwangalia " sio hivo,kwa nilipofikia sina namna itanibidi tu kuolewa na huyo" anatulia kidogo kana kwamba alijui jina la mtu anayetaka kumuoa wakati alimtaja mwenyewe " nzagamba" anamalizia kutaja jina akifumba macho yake na kuegemeza kichwa chake ukutani kama mtu aliyepitia masaibu ya mwaka na hapo bado yalikuwa yakimjia asijue Cha kufanya.

Sinde anarudi na kukaa mkao wake uleule wa awali "hapo kweli safari hii mpango umekuwa matumizi hongera kwa harusi" sinde anaongea na kumfanya tulya ageuke na kumwangalia jicho la kummeza na yeye kucheka kidogo.

Ghafla sinde anaamka na kukaa vizuri " lakini mpango wako umefanikiwa " anaongea macho yakimjaa bashasha tulya nae anatoa kichwa chake ukutani na kumwangalia kwa mshangao " mpango gani?"

" mpango wako wa kutaka kuolewa na mume wako tu" anaongea lakini tulya bado anamwangalia kwa kutokumuelewa na sinde anaendelea " sikia,Amna mwanamke anayetaka kuolewa na nzagamba zaidi yako,kwa hiyo ukiolewa nae utakuwa ni wewe peke yako tu mpaka mwisho wa dahari" uso wa tulya unabadilika kutoka kwenye uso wa makunyanzi ya mawazo mpaka uso wa matumaini " kweli sikuwaza hivyo hata kidogo,nimefanikiwa" tulya anacheka kwa nguvu sinde nae huku wakikumbatiana " subiri" sinde anaongea na tulya anavunja kumbatio lao "nini umekuja na faida gani nyingine"

" vipi kuhusu nyama,unavyopenda nyama hivyo utaweza kuishi maisha yako kwa kula panzi na ndege" sinde anaongea na kumvunja tena moyo tulya " kwani kulikuwa na ulazima wowote wa kunikumbusha uhalisi wa maisha yangu,kuniacha tu nilale na furaha nilioipata kidogo ukaona vigumu" anaongea na kumpiga sinde kidogo begani na kurudia mkao wake wa awali wa kuegemea ukuta " samahani,limekuja tu" anaomba samahani sinde naye akiegemea ukuta " unaomba samahani ya nini,nivizuri tu umenikumbusha Ili nianze kuzoea"

" subiri nikuletee chakula utakuwa na njaa mchana hujala" anaongea sinde akisimama

"kwani nyie mmekula"

"mda mrefu,kama ulivyosema jua halijazama Sasa hivi" anaongea huku akiondoka.Baada ya sinde kuondoka tulya anafumba macho yake na kuegemeza kichwa ukutani akikigongesha ukutani akiwa anatafakari mstakabali wa maisha yake kuanzia kesho na namna atakavyo pambana nayo 'ni bora ya nzagamba kuliko manumbu,Kila mtu anamzungumzia vizuri hata kama sijawahi kuonana naye najua hata nipiga kama manumbu' anawaza na kufikia tamati ya maamuzi yake ya kuolewa na nzagamba.

Nzagamba anafika Mahali wanapojikusanya vijana wote waliooa na wasiooa na kujadili Mambo mbalimbali huku wakinywa.moto mkubwa ukiwaka mbali kidogo na walipokaa kwa makundi makundi.

"nzagamba!" anaongea kijana Mmoja aliyemuona na wengine wote kugeuka na kuangalia alipo wasiamini kama amekuja.rafiki yake mkita anaamka na kumfuata na kukutana njiani " siamini kama umekuja,karibu siku nyingi kweli hujaja kwenye mikutano kama hii" anaongea mkita akimkumbatia "acha Mambo ya kitoto bwana" anaongea akimsukuma mkita asimkumbatie.

Wote wanasogea na kutengeneza nafasi Ili nzagamba nae apate nafasi ya kukaa katika mduara wao, anakaa karibu na mkita aliyekuwa amemganda kama ruba.Mmoja anachukua kibuyu Cha pombe na kumimina kwenye kipeo na kumpatia " karibu" nzagamba anapokea kipeo " asante" anawaanagali vijana wote waliokuwa wakimwangalia kana kwamba ni mgeni na kutabasamu kidogo.

Ni kweli hajaonekana siku nyingi kwani vijana waliokuwepo hapa wengi walikuwa ni wadogo wengine hawajui hata majina na wao wakimshangaa nzagamba maarufu wanaemsikia tu au kumuona kwa mbali, wengine wakitoka vikundi vingine Kuja pale alipokaa kwa ajili ya kumuona au wengine kuhakikisha kama kweli ni yeye amekuja. ndani ya dakika Moja kundi lao likawa kubwa kuliko kawaida kwa vijana waliomzunguka.

Licha ya nzagamba kutokuwa na bahati bado vijana wengi walikuwa wanampenda na kumchukulia kama shujaa wa kuigwa kutokana na ufundi wake wa matumizi ya silaha.nzagamba anapeleka kipeo mdomoni kama ilivyokawaida Yao anatakiwa anywe pombe yote kwenye kipeo pasipokupumzika kama adhabu ya kuchelewa,na yeye alikuwa na kosa lingine la kutokufika kwa mda mrefu. Anakunywa mpaka anamaliza na wote wanampigia makofi na kushangilia "aongeze tena" wanapiga makelele na miruzi kwa pamoja "ongezeni tu,nyie vijana wa Leo mtakuwa hamjui ni namna gani nzagamba anakunywa hata mlete vibuyu vyote hapa halewi" anajigamba mkita akimshabikia rafiki yake "atuonyeshe" vijana wanapiga makelele tena " mpeni" mkita anasema na kipeo kingine Cha pombe kinaletwa na nzagamba anakipokea akicheka anapeleka mdomoni na kuanza kunywa na vijana wakishangilia kumhamasisha kunywa,lakini kabla hajamaliza kipeo kinapigwa na pombe yote inammwagikia usoni mpaka kwenye nywele kifuani na nyingine kupita puani na kumfanya ashindwe kupumua vizuri.