webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · realistisch
Zu wenig Bewertungen
245 Chs

UKURASA

Alfajiri, katika uwanja wa ndege wa A-Town, Edrian na Aretha walikuwa katika sehemu ya uhamiaji wakikamilisha taratibu zote. Baada ya hapo waliekea sehemu ya mizigo kisha wakachukua mabegi yao na kuelekea kwenye mlango wa kutokea.

Mara mlango ulipofunguka, Edrian ambaye alisukuma torori lililobeba mabegi ya safari, alikuwa wa kwanza kumuona Li ambaye alipiga hatua kuwasogelea huku nyuma akifuatiwa na Frans.

Wakasalimiana huku Aretha na Frans wakikumbatiana kwa furaha, wakaelekea kwenye gari

****************

Mlio wa simu ulimshtua Edrian ambaye alikuwa usingizini ikiwa ni mida ya mchana, akageuka kuchukua simu iliyokuwa juu ya meza ndogo pembeni ya kitanda. Alipotazama nani aliyepiga akapokea haraka

"Captain kuna nini!" Akauliza huku akijigeuza na kulalia mgongo

"Fungua ukurasa wa NaT na GGnet kuna taarifa zimesambazwa"

"Sawa, fuatilia chanzo chake halafu subiri nitakwambia cha kufanya" Ed akamjibu na kukata simu mara moja. Akaingia kwenye mitandao ya kijamii akitafuta GGnet na mara akaona picha kadhaa akiwa na Aretha kwenye maeneo tofauti huko Australia. Akainuka na kuketi akiegemea ubao wa kitanda.

Akaangalia zile picha lakini uso wake ukaweka tabasamu la mbali kisha akasoma kilichoandikwa lakini kabla ya kuendelea simu ikapigwa, akaipokea mara moja

"Retha"

"Rian, samahani kukutoa usingizini" sauti ya Aretha ilikuwa na wasi wasi

"Hujaniamsha, niko macho nahisi kwa sababu hiyo hiyo iliyokufanya unipigie" Ed akamjibu

"Umeona na wewe!"

"Nimeona Retha, naomba usifadhaishwe, na usimjibu yeyote atakaye kupigia. Pumzika na ukiweza zima simu. Nitakutafuta baadae. Nakupenda Retha"

"Sawa. Rian" Aretha akamuita

"Ehmm"

"Tafadhali usiache kunipigia, baada ya masaa matatu nitawasha simu." Alimaliza Aretha

"Sawa" Edrian akakata simu na kuendelea kusoma kilichoandikwa.

Ilikuwa ni taarifa yenye aya moja tu, lakini kulikuwa na picha mbili zikimuonesha akiwa na Aretha na picha nyingine moja alikuwa na Joselyn ambaye alimpakata mikononi mara alipoanguka wakati wakitoka kwenye mgahawa wa the Lounge! Lakini picha moja iliyomshtua zaidi, walichukua picha ya tukio la Rising Star Show, ambapo Ed alikutana na Aretha kwa mara ya kwanza. Ed alimshika mkono Aretha huku macho ya Aretha yakimtazama kwa aibu..

'Wamewezaje kuipata hii picha' Ed akawaza

Juu ya zile picha maneno yafuatayo yaliandikwa;

'Kuna wakati ni vigumu kuficha upele, usipokuwasha ukiwa peke yake utakuwasha kwenye kadamnasi. Kwa haya 'Senior Bachelor' ndiye au tusubiri kujikuna"

'Mhhhh' Edrian akaguna, "mabingwa wa maneno acha niwape la kusema"

Akazima simu yake akarudi kulala.

*************

Masaa matatu yakapita na Ed alikuwa bado amelal, Aretha ambaye alipojaribu kumtafuta haikuwa rahisi kwake kuamini kuwa hakuna kinachoendelea. Akapiga namba ya Coletha

"Oooh wifi yangu nafurahi kukusikia tena" Coletha akapokea kwa furaha baada ya kuona aliyepiga ni Aretha

"Asante Coletha, nisamehe tu ila ninajaribu kumpata Ed kwenye simu lakini namba yake haipatikana"

"Hahaha atakuwa bado amelala. Unataka nimwamshe?"

"Aaaahm nitakuwa mkatili au unaonaje?" Aretha akamuuliza Coletha japo alifahamu alitaka kumwamsha

"Hahaha ngoja nimwamshe usijali, moyo wako utatulia" Coletha akamjibu huku akicheka

Akamgongea kaka yake mlango. Akagonga mfululizo hadi Ed alipoamka

"Kuna nini Coletha unajua huwa si___" kabla hajamaliza Coletha akamkabidhi simu huku akitabasamu

Baada ya Ed kusikia sauti ya Aretha, akamwambia anawasha simu muda mfupi atampigia

Akamrudishia Coletha simu na kumshukuru. Mara alipowasha simu yake kabla ya kuongea na Aretha, simu ikaingia kutoka kwa Allan

"Hello Allan"

"Hello Bro, pole kwa uchovu" sauti ya Allan ilikuwa na wasi wasi

"Asante, Vipi kuna shida Allan?" akamuuliza

"Ndio kaka, tuko na Alphonce, ila tunahitaji msaada wa Captain. Mfumo wa mawasiliano umezima ghafla kutoka G-Town. Hatujui nini kinaendelea ila tuna mzigo unatakiwa kutoka huko"

"Mhhhhh" Ed akaguna kisha akaendelea, "kama mfumo umezima ghafla Captain atakuwa na taarifa na naamini yuko njiani kuja hapo. Nakuja"

"Sawa kaka"

Edrian akashuka na kuelekea bafuni..