webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · realistisch
Zu wenig Bewertungen
245 Chs

ASANTE ZANGU

"Hapana aa namaanisha ndio lakini umetokezea tofauti na matarajio yangu.. umemaliza kazi?"Aretha akamuuliza mara alipomkaribia

"Nimemaliza nikaona ni vyema tutazame machweo ya jua pamoja" Edrian akamjibu kisha akaweka ule mfuko mezani. Na kumfanya Aretha atazame ule mfuko

Edrian akainama na kumbusu kwenye paji la uso kabla hajasogea kwenye meza nyingine akaona picha ambayo Aretha alikuwa akiichora. Akasogea kuiangalia lakini Aretha akamuwahi na kumvuta nyuma

"Usiangalie haijakamilika Rian" Aretha ambaye pamoja na kumvuta Ed bado hakuweza kumzuia kuitazama ile picha..

"Sawa mpenzi siangalii, ila wewe sasa angalia kwenye huo mfuko mimi zawadi yangu nataka uione" akasogea kwenye meza yenye matunda akachukua tena tufaa la kijani akala

Aretha akamwangalia Edrian kwa uso wa mshangao, akafungua mfuko uliokuwa juu ya meza. Akatoa mkebe uliofungwa vyema kwa namna ya zawadi, akatoa karatasi ya juu na mara hiyo macho yake yakawaka kwa furaha

Edrian sasa alisimama akiwa amemtega mgongo Aretha huku akitafuna tufaa. Kichwani bado alikuwa na mashaka akitamani kumuuliza Aretha ni nani aliyekuwa akizungumza nae...

Akiwa kwenye mawazo yake alishtuliwa na mikono Aretha iliyomshika tumboni akimkumbatia kutokea nyuma.

"Oooh asante sana Rian, nashukuru mno mpenzi" yalikuwa maneno yaliyomtoka Aretha huku machozi ya furaha yakilowanisha shati ya Ed.

Edrian aliposikia hivyo akatabasamu kwa furaha, Aretha alimkumbatia kwa ghafla kwa furaha nyingi kiasi cha kufanya tufaa lililokuwa mkononi kwake kuanguka.

"Rian ulijuaje nahitaji hiyo 'set', ooooh Mungu wangu asante sana"

"Retha basi yatosha nitashindwa kupumua" Rian akamtania

"Oh samahani" Aretha akarudi nyuma na kumpa nafasi Edrian kumgeukia

"Umefurahi lakini furaha yako imeangusha tufaa langu" Edrian akajifanya kuwa amekasirika

"Aaaaa jamani, samahani sana Ri_" lakini kabla hajamaliza Edrian akamsogelea sana Aretha na kumfanya ashindwe kumalizia alichotaka kusema

"Unakumbuka bado nakudai samahani nyingine eeh?"

"Mmmmh" Aretha akaguna huku akijaribu kuinua macho yake kuyakabili yake ya Ed lakini asiweze akaangalia pembeni

"Umeifurahia zawadi?" Akauliza

"Ulijuaje nahitaji brashi mpya, yaani kila kitu kimo ndani. Oooh asante sana Rian" Aretha akashukuru. Moyo wake ulijaa furaha kwa zawadi ile kutoka kwa Ed ambayo ni mkebe wenye vifaa vya uchoraji ikiwemo brashi ngumu na laini.

"Retha, asante zangu si unazifahamu?" Akamuuliza huku akiwa amemshika kidevu akimwangalia usoni

Aretha akajaribu kurudisha macho asimtazame usoni lakini hakuweza akaamua kufumba macho. Naye Ed akabaki akimtazama machoni

"She is adorable" akawaza

Aretha akaamua kufumbua macho baada ya kuona Edrian hafanyi chochote,

"Good! Naomba asante yangu sasa" Edrian akamwambia kisha akafumba macho mpaka aliposikia midomo ya Aretha ikimbusu taratibu kwenye ile yake. Akamuwahi na kupitisha mkono wake mmoja kiunoni mwingine ukatulia shingoni. Akalibana lile busu alilopata kwa midomo yake na kumfanya Aretha akubaliane na kile alichotaka kwa kumruhusu apitishe ulimi wake kwenye midomo yake. Wakazama katika busu hilo kwa sekunde kadhaa kabla ya kumuachia Aretha ambaye alionekana kuhitaji hewa.

"Hii ndio asante kutoka kwa mpenzi wangu." Edrian akamwambia kisha akamshika kiuno na kumuongoza hadi kwenye kiti. Alipomkalisha akachukua chupa ya maji na kumpa Aretha ambaye hakumwangalia usoni lakini akitabasamu

Baada ya kunywa maji, Edrian akaketi kiti cha pembeni na wakati huo mandhari ilikuwa katika mchanganyiko wa rangi ya dhahabu na wekundu wa miale ya moto.

Kimya kikapita kati yao kabla ya Aretha kuzungumza

"Rian" akaita.

"Mmmh" akaitika Ed huku akiinyoosha miguu yake na kuegama kwenye kiti

"Nina ombi" Aretha akamwambia, kisha akaendelea kwa kutambua kuwa Ed alikuwa akimsikiliza

"Kuna fursa imetokea nataka kuitumia vyema"

"Aahm fursa hiyo itaingilia safari yetu?" Edrian akauliza

"Haaaa hapana..sina uhakika kama itaingilia"

"Ninachokuomba princess usiruhusu chochote kiingilie hii safari." Kulikuwa na msisitizo mkubwa kwenye sauti ya Edrian kiasi cha kumfanya Aretha kusita kuendelea