webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · realistisch
Zu wenig Bewertungen
245 Chs

ANATAMANI KUNIONA

"Unampigia Aretha eh?" Akauliza Linus

Coletha akatikisa kichwa kumkubalia na wakati huo simu yake ikapokelewa,

"Hellow Aretha"

Upande wa pili Aretha akaitika, "safi Coletha unaendeleaje?"

"Niko poa, uko sehemu gani hapo chuoni?" Swali ambalo lilionekana kumshtua Aretha

"Eeehm!"

"Uko wapi maana ndio tunaingia hapa getini?"

Aretha akampa maelekezo mahali alipokuwa akimsubiri huku akishangaa kama Coletha ndie aliyetumwa kumchukua au ni bahati tu kuwa yuko pale chuoni. Akiwa ameketi katika moja ya vibwete vilivyokuwa karibu na jengo la Utawala, alikuwa na uwezo wa kuona magari yaliyoingia. Kwa mbali aliiona SUV nyeusi ambayo aliitambua vyema si tu kwa muonekano bali hadi namba ya gari.

Akashusha pumzi na kuinuka moyo wake ukiwa na shauku ya kumuona Coletha aliamini itakuwa ndiye alikuwa akiendesha. Akapita hatua kuelekea kwenye gari alipokaribia kushika kitasa cha mlango Coletha akafungua taratibu,

"Arethaaaa" Coletha akashuka na kumkumbatia akizidi kumchanganya Aretha ambaye aliangalia upande wa dereva lakini macho yake yakakutana na kioo cheusi ambacho kilifanya iwe ngumu kwake kuona mpaka aliposikia sauti

"Coletha hebu mwachie mwenzio apumue eeeh" Linus akamshtua mdogo wake.

Achana na kaka Li, njoo tukae zetu huku uniambie mambo yakoje upande wako. Coletha akamshika mkono na kwa pamoja wakapanda kwenye gari.

"Habari ya mchana Aretha" Li akamsalimia huku akiwasha gari

"Salama kaka, pole kukusumbua kunifuata" Aretha akajibu huku akiketi vyema.

"Ondoa shaka Aretha, tuko pamoja" Li akamtoa wasiwasi Aretha

"Hiyo njano imekupendeza sana" Coletha akamwambia Aretha ambaye alivalia blauzi ya kitambaa chepesi cha njano na suruali nyeusi huku chini akivaa raba zake nyeupe.

"Asante Coletha" akapokea pongezi zile huku akiinama kwa aibu kukwepa kuonana na Li ambaye alikuwa amemezwa macho yake barabarani ambapo waliingia baada ya kutoka chuoni.

Njiani Coletha ndie aliyetawala mazungumzo ndani aliuliza maswali mbalimbali kwa Aretha huku mara kadhaa Linus akimkatisha ili kumpa nafasi mwenzie apumue.

"Bro ulikosea sana maana huyu mdogo wetu ni shida duuuh" aliwaza Linus

Safari yao ikaishia kwenye jengo la Ashante, Edrian alikuwa tayari akiwasubiri kwa shauku kubwa ya kumuona Aretha. Alipoona simu ya Li, mara moja akaipokea huku akiinuka tayari kuondoka ofisini kwake.

"Nakuja" akamjibu. Akaelekea ofisini kwa Allan lakini Loy akamjulisha kuwa yuko kwenye kikao kifupi na mhasibu.

"Natoka Loy, naomba uzingatie tulivyoongea. Naweza nirudi au la" akaaga Edrian na kutoka ofisini huku akisimama baada ya kuona ujumbe ulioingia kwenye simu.

"Rian unakuja?"

Ujumbe ulitumwa na Aretha ukaweka tabasamu usoni kwa Ed akabonyeza kitufe cha kufungua lifti, mlango ukafunguka akapiga hatua kuingia

"Mr Simunge tafadhali nisubiri" Renatha aliyepiga hatua kwa haraka akasogea na kutaka kuingia kwenye lifti.

"Renatha tafadhali tumia lifti wanayotumia wengine." Ed katika sura iliyobadilika ghafla akamjibu na kubonyeza kitufe cha lifti kumshusha chini

"Lakini nili_" Renatha akajaribu kumwambia Ed lakini jicho aliloliona kwake lilimfanya anyamaze na apige hatua kurudi nyuma

"Allan yuko ofisini atakusaidia." Mara alipomaliza mlango ukajifunga na lift ikamshusha huku akijibu ujumbe aliotumiwa.

"Nakuja princess" akajibu kisha akatabasamu na kushusha pumzi

"Retha anatamani kuniona aah" akawaza taratibu

Akafika na kushuka kwenye lifti akapiga hatua taratibu kuelekea alipoona gari yake imesimama. Eneo hili la maegesho rasmi lilikuwa na magari machache lakini ya kifahari.

Kule ndani ya gari Linus alimuona kaka yake akija, akashuka kwa kujua kuwa Edrian ataingia sehemu ya dereva.

"Hey Li vipi mbona umeshuka? Akamuuliza kwa mshangao

"Ni nafasi yako Bro au?" Li akajibu

"It's been a while, you will drive us bro" Edrian akamwambia huku akielekea upande wa abiria

Kule ndani Aretha aliibia kumwangalia Ed akija, mapigo yake ya moyo yalidunda haraka huku tumboni joto na baridi kwa wakati mmoja vilipita.

"Unampenda Big brother Aretha eeh" Coletha alimnong'oneza alipogundua macho ya Aretha yalipoangalia

"Aaaahm" Aretha akashtuka