webnovel

Sura ya 2:Pete

Urithi wa taji

Sehemu ya pili 2

"Annia mpendwa....najua utapitia mambo mengi sana baada ya kifo changu lakini usisahau mila zetu."

"Nazijua baba tena vizuri."

akajibu Annia bila kuelewa vizuri.Firauni akatabasamu na kumtazama Annia kwa huruma kidogo

"Unajua mkubwa ndio huwa anarithi eh?"

akauliza Firauni swali lililomshtua mno Annia.

"Baba..."akaita kwa mshtuko.Senet sasa akamtazama Annia.

"Wewe ndio mrithi wa taji langu."

"Baba mara zote mtoto wa kiume ndio hurithi taji so wa kike."

"Naelewa ila ili kaka yako awe mtawala lazima akuowe."

Annia hakusema neno zaidi ya kutazama pembeni tu.

"umeona sasa?nadhani utaamini kuwa hapa kwetu wanawake ni vyombo vya starehe tu.huo uzuri wako wote sasa mali yang"

akasema Senet na kumfanya Annia atabasamu kwa mbali.

"Usisahau kuwa mimi ni mkubwa wako hivyo fikiria nikikataa itakuaje?"

Akajibu Annid na kumfanya Senet acheke.Sio ajabu kwa kaka na dada kuowana ndani ya misri enzi hizo.Annia akamgeukia baba yake na kumpa taarifa nyingine.

"Baba...pete imeibiwa"

"Pete!Pete gani hiyo labda?"

akauliza akiwa na mashaka kidogo

"Pete ya ukoo...tena ni ya Amrilla."

"Nini!!!!!!!"hapo firauni akashtuka sana

Amrilla ni binamu yao kina Annia.Yeye anaishi mwenyewe maeneo ya msitu milimani.Hapendi kukaa na ndugu zake na pia ni hatari mno kukaa karibu na watu wa kawaida.Hakuna aliyewahi kuiona sura yake hata kidogo maana huvaa mask muda wote na ni vigumu mtu kumtembelea.kiumri alikua sawa na Senet.Ubaya ni kwamba ile pete Annia ndio alimuibiwa Amarilla ingawa kiutani ..je akijua itakuaje?na pete imepoteaje?

Dada!"

Asteria akafika nyumbani na kumuita dada yake ambaye ni Dragona.Ni mrembo balaa

lakini tatizo yeye ni bubu,hawezi kuongea akasikika.

"Dada umasikini kwaheri..nimeokota hii pete."

akamuonyesha Dragona ile pete.Dragona akashtuka mno baada ya kuiona ile pete.Haraka akamnyang'anya kuhakikisha kama ameona sahihi ama la....

facebook..author bahati