webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Realistic
Not enough ratings
245 Chs

SIKUOGOPI

Ilikuwa saa kumi alfajiri walipowasili katika uwanja wa kimataifa wa Kingsford Smith. Aretha alikuwa na uchovu mwingi lakini mara tu gari waliyoipanda iliposimama kwenye hoteli ambayo iliandaliwa kwa ajili yao.

Aretha akageuka na kumtazama Ed kwa mshangao wenye kuchanganyika na furaha, kisha akarudisha macho yake kutazama uzuri wa hoteli ile. Ed akashuka mara tu mlango wa gari uliponguliwa na mhudumu. Gari waliyoitumia ilikuwa na nembo ya hoteli hii.

Mara aliposhuka, tayari kulikuwa na wahudumu wawili wakike na wakiume, wakamkaribisha kwa pamoja. Aretha akafuata mara Ed alipotoka. Yule mhudumu wa kiume akaelekea nyuma akisukuma kitoroli, ambapo dereva alifungua kwenye sehemu ya mizigo na kumruhusu kuchukua mizigo. Yule mhudumu wa kike akamuomba Edrian wafuatane naye.

Wakaelekea kwenye lifti iliyowapeleka mpaka ghorofa ya kwanza ambapo Aretha akamshika Ed mkono kumuonesha hawezi kuvumilia kwa hiyo furaha aliyokuwa nayo.

"Retha subiri kidogo nikusuprise tunakoelekea" Ed akazungumza kwa kujiamini kisha akamshika begani mara waliposimama mbele ya meza ya mhudumu mwingine

Wakathibitisha uwepo wao pale na kisha wakakachukuliwa mpaka chumba chao kilichoandaliwa. Ed aligundua ukimya wa Aretha mara alipoona mlango wa chumba kilichochukuliwa ni mmoja, akatabasamu na kuinama usawa wa sikio lake akamwambia

"Tutalala wote princess sitaki uwe peke yako"

Aretha akamwangalia kwa mshangao lakini hakuwa na wasi wasi usoni, nae akamrudishia tabasamu japokuwa moyoni mapigo yake ya moyo yaliongezeka...

Mhudumu akaweka kadi na mlango ukafunguka kisha akaitoa na kumkabidhi Ed,

"Enjoy your stay Mr&Mrs Simunge" akainama na kuondoka baada ya Ed kumshukuru pia huku Aretha akijaribu kubana kicheko aliposikia maneno ya mhudumu yule.

Ed akamfinya kidogo begani Aretha, ambaye sasa alicheka kwa sauti huku akishtuka kuwa walisimama kwenye korido ambalo lilijaa ukimya, Ed akasukuma mlango na kumpa nafasi Aretha kuona chumba watakachoishi kwa hizo wiki mbili

Aretha akaingia ndani na akaelekea moja kwa moja kwenye sofa nzuri zilizoweka mkono wa kushoto karibu na meza ndogo ya chakula. Akatupa mkoba na yeye mwenyewe kujitupia kwenye sofa lile..

"Waaaaoh kochi laini hili" akasema Aretha huku akiendelea kushangaa mandhari nzuri ya chumba hiki. Rangi ya chumba ilikuwa ni nyeupe lakini karibia vitu vingi vilivyokuwamo vilikuwa rangi ya dhahabu. Makochi, mapazia na kabati ndogo iliyokaa karibu na dirisha vinakshiwa kwa rangi nzuri ya dhahabu. Kulikuwa na milango mitatu ambayo miwili ilikaribia kabati la kioo lililohifadhi vitabu vya historia.

Alipotazama pembeni mizigo

Aretha akamtazama Edrian ambaye alisimama karibu na mlango mmoja wapo akifurahia shauku yake..

"Miss Thomas, tafadhali karibu chumbani kwetu" Edrian akamshtua Aretha ambaye sasa aliangaza macho yake kwenye michoro ya picha zilizobandikwa ukutani.

"Aaaah" akageuka na kumtazama Ed ambaye alifungua mlango taratibu na mwonekano wa chumba ukawa wazi machoni kwa Aretha mdomo wake ulibaki na alama ya "O"

"Presidential suite"

Kitanda kikubwa kilionekana, nakshi yake ilikuwa kama mojawapo wa vitanda vinavyooneshwa kwenye filamu za kufikirika za "Disney". Meza ndogo ilikaa pembeni ya kitanda huku pazia zilifanana na zile zinazoonekana kwenye nyumba ya mwanamfalme.

Kulikuwa na mlango mwingine mkono wa kushoto na pembeni yake kulikuwa na kiti na meza kubwa ya kioo.

Aretha akaingia na kuketi kwenye kitanda huku akibonyeza godoro lile

"Kaoge upumzike kwa masaa machache yaliyobaki nitakuwa na ratiba baada ya masaa manne" Edrian akamwambia huku akisogea palipo na mlango ule akafungua,

"Bafuni hapa, mlango hapo kushoto ni kabati la nguo, unaweza muita mhudumu au ukapanga mwenyewe. Nitakuwa kwenye mlango unaofuata ikiwa utanihitaji" akaachia tabasamu mara alipomaliza kumwambia Aretha

"Aaahmm...ni ofisi au?" Akauliza kwa mshangao

"Hahaha Retha, mlango wa pili ni chumba na ofisi hapo hapo. Uliogopa eeh!" Edrian akamchokoza

Aretha akatikisa kichwa kukataa, "Hapana Rian.. sikuogopi hata kidogo." Akamjibu huku akikunja mikono yake kwenye shuka

"Are you sure?" Akamuuliza