webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Realistic
Not enough ratings
245 Chs

MTU PEKEE KATIKA MOYO

Akasogeza meza ndogo karibu na Ed kisha akamimina maziwa kwenye glasi na kumkaribisha.

"Asante mama" akajibu Ed akisubiri kwa shauku nini kitamtoka mama huyu ambaye alielekea kukaa kwenye kochi la mmoja lililotazamana na alilokaa Ed.

Akamsubiri mpaka alipokunywa funda moja akaendelea na mazungumzo.

"Hapa ndio nyumbani kwa Aretha mwanangu, nashukuru kwa kumrudisha salama jana na pole kwa misukosuko ya barabarani."

"Asante mama, nashukuru pia kupafahamu hapa" Ed akajibu akijaribu kuwa sawa mbele ya huyu mama.

"Ni vizuri kukufahamu pia, nimemfahamu mdogo wako Derrick.. na hapa ni nyumbani kwake kabisa" mama akaendelea na kumzungumzia Derrick asijue alikuwa akibomoa hisia za Ed ambaye sasa alikunywa maziwa kwa haraka hadi yakabaki kidogo sana kwenye glasi. Aaaaah mama anataka kumaanisha kuwa anamkubali Derrick sana.. aarggghhh Ed alihisi ndani moto unamtafuna

"Ni mchangamfu sana, nilifurahi kuona Aretha kapata rafiki kwa kweli. Binti yangu ana aibu na muda mwingi hapendi kuwa kwenye mikusanyiko ya watu wengi" aliendelea mama huyu

"Aaaah. .. Sawa mama, atakuwa salama tu kwa Derrick" Ed akayasema maneno haya akiwa amebana meno asije mama akashtuka kwa mabadiliko ya sauti yake..

"Mwanangu nikuongeze maziwa?" akauliza mama

"Hapana, yananitosha kabisa." Ed akajibu, akatamani kuangalia simu yake walakini haikuwezekana maana aliisahau kwenye gari baada ya kupatwa na mshangao wa mama huyu kumkaribisha ndani.

"Sawaaa..mmm.najua unatamani kujua kwa nini nimekukaribisha ndani na sio kukupa koti lako tu mwanangu" mama akaamua kunyoosha maelezo kama ambavyo Ed alikuwa akiomba

"Ndio mama"Ed akajibu na macho yake yakatulia akitazama moja kati ya picha zilizowekwa kwenye ubao uliokuwa upande alioutazama wa ukuta...

"Mwanangu, wewe ni mtu pekee ambaye naweza kusema umeingia katika moyo wa Aretha. Siwezi kukwambia nimejuaje... lakini mimi ni mama yake. Namjua binti yangu"

Edrian akatamani ajipige kofi pwaaa ili kujiamsha kwenye maneno haya anayosikia kutoka kwa mama huyu... what! Aretha ananiwazia mimi....inawezekanaje hii?.... moyo wa Ed ulioparaganyika mwanzoni ukatulia tuli. Ni kama bahari iliyochafuka halafu ghafla kukawa shwari.

"Aamhh. .. eeh" hakuweza kuunda maneno yoyote kumjibu mama huyu aliyekuwa akimtazama Ed

"Usijali mwanangu najua na wewe unashangaa kama mimi ninavyoshangaa...nitakwambia kwa nini siku moja huko mbeleni kama utakuwa umeshawishika naye" mama akaendelea

Ed akatamani amwambie ameshawishika naye tangu alipomuona..

"Sasa mwanangu najua ulimwengu wako sio wake, lakini kabla hujaja niliongea na Derrick.. kanihakikishia wewe ni mtu mwema." Mama akameza mate kisha akaendelea

"Sikwambii umtumie binti yangu na wala sijakupa ruhusa ya kumfanya mpenzi wako..." Ed akashtuka lakini akajitahidi kuficha mshtuko wake kwa tabasamu

"Nataka umsaidie aweze kuenda sawa na ulimwengu wenu. Aweze kuwa binti mwenye uwepo wa kukabiliana na chochote katika kutimiza ndoto zake.. Anachora picha nzuri lakini anaogopa watu kumlaghai. Mfanye awe jasiri kama wewe" mama alimsihi Ed kwa msisitizo

"Oooh sawa mama. Nitajitahidi kufanya hivyo" Akajibu na kumrudishia mama tabasamu lake la kujiamini.

What! Wait yaani mama yake Aretha anampa ruhusa Ed kuwa karibu na binti yake... mzazi gani aweza kufanya hivyo.. Ed hakujua ashukuru au afanye nini..

"Kitu kimoja nakuomba" mama akaendelea na kumfanya Ed ainue macho yake kumsikiliza

"Mlinde na fujo zinazokuzunguka, pia kuna mambo yaache yajirekebishe yenyewe usijaribu kuyaharakisha kwake. Nakuamini kwa maisha ya binti yangu"

"Oooh my God.. mbona kama mambo yanakuwa rahisi kwangu" akajisemea moyoni Ed.

Akakohoa kidogo na kuamua kumuuliza mama huyu..

"Mama...samahani kwa hili naloenda kuuliza lakini natamani kujua kwa nini unaniamini hivi?" Ed hakutaka kuchukua vitu tu kwa wepesi. Aliamini kuna zaidi mama huyu anajua kuhusu Aretha na yeye..

Mama akatabasamu na kuendelea.."najua kama umeweza kuja kwangu, ukanywa maziwa yangu bila kuwa na shaka na mimi, basi nami nakupa imani hiyo hiyo"

Loooh mwanamke wa tofauti..Edrian akamwangalia kisha akatabasamu na kuinua kichwa..