webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Realistic
Not enough ratings
245 Chs

LOVE ME BACK

Edrian alishusha pumzi na kuinuka kitandani..akatoka chumbani kwa mwendo wa pole pole huku akiwaza kwa nini Lyn yuko pale alfajiri ile. Alipotoka kwenye mlango mkubwa uliompeleka nje akaangaza kumtafuta mlinzi, akamuona akitokea upande wa nyuma akielekea alipokuwa amesimama.

"Kaka kuna usalama? Nimesikia mlango unafunguliwa ndio nikaja" mlinzi akamueleza

"Hamna tatizo kuna mgeni wangu hapo nje nisaidie kumfungulia geti" Huku akipiga miayo akamwambia mlinzi

Mlinzi akaweka silaha yake vyema na kuelekea getini akageuka kumuuliza Ed

"Ana gari nifungue kubwa..?"

Ed akatikisa kichwa kumkatalia, mlinzi akaelekea kwenye geti dogo na kufungua.

Lyn aliposikia geti likifunguliwa akashuka kwenye gari iliyomleta ambayo ilikuwa ya kukodi.. akaelekea ndani huku akimshukuru mlinzi ambaye alionekana wazi kushangaa ujio ule wa mapema..

"Oooh Ed nisamehe kukuvamia ila nitaenda wapi" Lyn akaelekea aliposimama Ed huku mikono yake ikiwa imeachiliwa kumkumbatia..na alipomkaribia akamkumbatia Edrian ambaye alibaki amesimama asielewe mwanamke huyu kapatwa na nini.

Aliposhtuka akagundua mlinzi alibaki amesimama akishangaa, akamshika mabega Lyn na kumuelekeza waingie ndani.

"Oooh sorry babe nilisahau" Lyn akaomba msamaha baada ya kugundua sababu ya Ed kumuelekeza ndani..

Ed akatangulia ndani huku Lyn akimfuata kwa nyuma. Alipofika sebuleni akapata wasi wasi ikiwa atakaa na Lyn pale basi huenda ndugu zake wakapata mshtuko. Akapanda ngazi kuelekea juu huku akikata kona kuelekea ofisi yake na sio chumbani.

Lyn akatamani amuulize Ed kwa nini wanaenda ofisi yake ya nyumbani badala ya chumbani, lakini akaazimu kunyamaza.

Alipofungua mlango wa ofisi, Ed akaelekea ilipo meza yake akaegama na kumwangalia Lyn ambaye alipofunga mlango akaelekea aliposimama. Kabla Lyn hajaongea chochote Ed akamuwahi

"Lyn hebu kaa chini tuongee"

Lyn akarudi nyuma na kukaa kwenye sofa akamwangalia Ed kisha akaweka uso wake wa kudeka..

"Ed najua nimekuja bila taarifa, lakini sikujua wapi niende baba amenifukuza"

"Nini" Ed akauliza kwa mshangao.. inawezekanaje hiyo, Martinez Kussah kwa binti yake huyu..Hapana, Ed akaamini kuna kitu nyuma ya hiki anachofanya Lyn..

"Babe jana ulinikatia simu, nikajua umenikasirikia sababu ya baba. Nilipoenda kumwambia aache anayoyafanya kwako ndio akanikasirikia" Macho ya Lyn yakaonesha kujaa machozi na ndani ya sekunde yakaanza kutiririka huku akivuta makamasi mepesi yaliyoashiria kulia kwake...

Edrian hakujua nini afanye, moyoni hakuwa na shaka kuwa Lyn anaigiza haya yote. Haikuingia akilini kwa Ed kuwa Martinez anaweza kumfukuza binti yake kwa kumhoji tu...

Edrian akabaki amesimama pale pale akimuangalia Lyn.

"Babe... mimi sihusiki na chochote na nilimwambia baba sababu hunipendi siku hizi unadhani nahusika. Kwa nini lakini" Lyn akaanza kulia tena sana na kwikwi zikaanza...

Ed akachoka akaamua kumsogelea na kuchuchumaa karibu na magoti ya Lyn, "Lyn naomba uache kulia tuongee vizuri maana sijaelewa hata kidogo kwa nini umeondoka alfajiri"

Lyn akainua sura na akamwangalia kwa macho yaliyojaa machozi na ghafla akamkumbatia Edrian ambaye alishtuka na kujikuta anakosa uwiano sawa na kuangukia kwa nyuma.

Lyn akatumia muda huo mchache kwa kuwa alikuwa juu ya Ed akamkumbatia Edrian na kuendelea kulia huku nywele zake zikiwa zimezagaa kwenye kifua cha Ed.

"Babe nisamehe mimi, sijui chochote, please love me back...I miss you" aliongea kwa sauti laini iliyojaa kudeka na kwikwi za kulia

Kabla Edrian hajapata namna ya kuinuka kwa kuogopa kumuumiza Lyn iwapo angetumia nguvu... mkono wa Lyn ukaanza kumpapasa kifuani..Akashtuka!

Akamshika mabega na kumsukuma taratibu aweze kurudi nyuma..Lyn akainuka na kumwangalia

"Lyn hebu kaa uniambie kwa nini uko hapa" sauti ya Ed sasa ilijaa mitetemo ya hasira...

Lyn akainuka na akaketi kwenye kochi huku akiweka nywele zake vizuri. Ed nae akainuka na kuelekea kwenye meza aliyoegama mwanzo. Uso wake ulionesha wazi hasira kwa mikunjo kuonekana kwenye paji la uso wake...mikono yake iliyoegama kwenye meza ilionekana kabisa imekunjwa kwa mfano wa mtu anaye jaribu kudhibiti ghadhabu..