webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Realistic
Not enough ratings
245 Chs

HII INATOSHA

"Rian una uhakika tutapata mahali pa kuketi naona hadi nje pamejaa!" Aretha akamuuliza Ed walipofika Lunch Hour Restaurant. Mgahawa ambao ulipika chakula kizuri na bei yake ilikuwa rafiki kwa kila mtu.

"Usijali Retha bado kuna nafasi kwa ajili yetu" akachukua simu yake na kupiga ikaita kisha ikapokelewa.

"Rommy niko hapa nje" Ed akaongea akisubiri making ya upande wa pili.

"Sawa, nakusubiri" Ed akajibu na kukata simu!

"Retha dakika kumi tutaingia"

"Sawa"

"Kuna kitu nataka kukwambia princess" Ed akamwambia Aretha..

"Aahm" Aretha akamjibu huku akiondoa macho yake kwenye simu na kumuangalia Ed tayari kumsikiliza.

"Joselyn alikuja ofisini kwangu leo" baada ya kusema maneno haya Ed akamuangalia Aretha usoni kusoma hisia zake kabla ya kuendelea. Aliona utulivu katika hisia za Aretha kitu kilichomfanya aendelee,

"Alikuja na bahasha yenye picha ambazo zinatuonesha tuko pamoja." Ed akaendelea kumuangalia usoni lakini Aretha alimpa ishara kwa kutikisa kichwa kuwa aendelee.

"Kuna picha ambazo zinatuonesha aaahm..tukiwa pamoja aaa kitandani..ambazo anakusudia kukuletea uzione ili uniache" Ed alimeza mate baada ya kuona Aretha amebadilika kidogo usoni "Damn you Lyn" akamlaani mawazoni mwake Joselyn, akajikaza na kuendelea

"Lakini Retha, sikukwambia ilitokeaje nikawa na ukaribu ule wa hadi kitandani na Lyn, nakuomba unipe nafasi nikuelezee" Akamwangalia Aretha ampe ruhusa ya kuendelea..

"Rian" Aretha akamuita kwa sauti ya upole huku macho yake yakiangalia vidole vyake.

"Eehm" Ed aliitika na wakati huo mapigo ya moyo ghafla yakaongezeka akihofia nini Aretha angesema. Ghafla Retha akamwambia "nikumbatie"

"Eeeeehm" kwa mshangao kama hakusikia vyema akamwangalia Aretha ambaye alisubiri Ed afanye alichomuomba huku akitabasamu

Akaachia mikono yake na kumkumbatia Aretha huku majibu tofauti yakipishana kichwani kwake kujibu swali la, "nini maana ya hili kumbatio"

Au Aretha ndio ananiacha?

Au ameumia kwa hilo?

Aretha akajitoa mikononi mwa Ed akamwangalia huku tabasamu lake likiendelea kumchanganya zaidi, akasogeza mkono wake wa kushoto akauweka kifuani kwa Ed ambaye aliweka juu wa kwake akiushika wa Aretha

"Najua mambo mengi yataibuka hasa kuhusu wewe na yule dada Rian. .a aahm ninachagua kukuamini pasipo kusikiliza kilichotokea. Wala usisumbuke kunielezea, Rian..am over 20 hata kama sina experience na uhusiano naweza elewa. Umemuacha si kwa sababu yangu bali una sababu zako. Ni kawaida kwa yeye kunifuatilia mimi ili kunichanganya. I love you hii inatosha hata akituma picha sitaziangalia. Amani iwe ndani yako"

Ed ambaye aliugandamiza mkono wa Aretha kifuani alitamani kumnyanyua alipoketi ambebe... akauchukua mkono na kumbusu sana, "Thank you Retha"

Simu yake ikaita, "Eeh tayari Rommy" akaitika. "Okay tunakuja kupitia huko nyuma" akakata simu, akamgeukia Aretha na kumwambia nafasi ilikuwa wazi tayari waende. Kabla ya kushuka akamshika Aretha kwa ghafla mabegani, "please a simple kiss Retha" akambusu kwa taratibu mdomoni kisha akamwambia "twende princess" akainama na kufungua mlango wa upande wa Aretha kwa ndani.

Wakaelekea mlango wa nyuma ambao uliwaepushia macho ya watu wengi waliokuwa wakipata chakula.

Ed akaushika mkono wa Aretha mpaka walipokutana na Rommy ambaye aliwapeleka kupitia jikoni hadi walipotokea kwenye ukumbi mdogo wa VIP ambao sasa ulikuwa na watu wachache. Baadhi yao walionesha kumfahamu Ed

"Mr Simunge" mhudumu akainama kwa heshima kisha akawaelekeza kwenye meza ambayo ilijitenga kidogo na nyingine.

Walipoketi, akachukua oda zao na akaondoka huku akiahidi kurejea na juisi.

*******************

"Loy eeeh?" Renatha akamwangalia Loy ambaye alikuwa kwenye mgahawa uliokuwa kwenye jengo hili la Ashanti.

Karibu asilimia kubwa ya wafanyakazi waliofanya kazi kwenye jengo hili walikuja kula kwenye mgahawa huu. Mchana huu Loy aliketi kwenye meza peke yake akipata chakula cha mchana. Aliwahi kwa kuwa Ed bosi wake aliondoka mapema. Akaamua kuja kula mapema kabla ya kukabiliana na baadhi ya ratiba za Ed ambazo Allan alikabidhiwa kuzikabili.

"Yes, Loyce" akamjibu Renatha ambaye aliketi bila wasi.