webnovel

SURA YA KUMI NA MOJA

Pale kizimbani Bw. Siga alikuwa akimwangalia hakimu kwa macho ya uoga, hiyo ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kortini, alihofia hatma yake baada ya hukumu iwapo angekula kalenda au angeachiliwa kuwa huru.

Kando yake Bw. Vura alikuwa amesimama, hakuwa kama mwenzake. Alionekana mtulivu, alijua yeye ni ndege mwenye mbawa za nguvu na ingemuwia rahisi kujinasua kutoka kwa mtego uliomnasa.

Upande mwingine bikizee ambaye hawakuwa wanamfahamu alisimama kwa msaada wa mkongojo wake, mwelekezi wa mashtaka alisoma kesi mbele ya umati kisha akamgeukia yule ajuza.

"Bi. Chonde, una chochote cha kuelezea mahakama?," Mwelekezi wa mahakama alimuuliza yule bibi baada ya kumkaribia.

"Ndiyo mwanangu," Bi. Chonde alinena kwa sauti iliyojaa kutetemeka, "niwie radhi kwa kukuita mwanagu."

"Hakuna baya mama."

"Kwanza ningependa kujitambulisha, mimi ni bibiye marehemu Arina."

Bw. Vura na mwenzake waliangaliana kwa mshangao baada ya kusikia uhusiano kati ya yule bibi na mfanyakazi wao wa awali, Bw. Vura alimnong'onezea.mwenzake maskioni naye akaitikia kwa kichwa.

Kando yao mwanaume aliyevalia suti nyekundu alisimama, kwapani alikuwa amebeba mkoba mweusi. Alimsongea Bw. Vura kizimbani wakazungumza kisha akafungua mkoba wake na kuanza kupekuapekua makaratasi yaliyokuwa ndani.

"Kutokana na kifo cha mjukuu wangu Arina, sina mengi ya kueleza mahakama ila alikuwa amebadilika si kidogo," Bi. Chonde alielezea akitokwa na machozi.

"Usilie bibi," mwelekezi wa mahakama alimpoza, "lakini kabla ya kifo chake alikuwa amekwambia chochote kilichokuwa kinamkera?!"

"Hapana mwanangu, lakini majuma mawili kabla ya kifo chake, tabia ilibasilika kabisa. Alianza kukaa pekee yake akionekana mwenye mawazo na kila nilipoenda kwake aliniondokea. Nilijaribu kumuulizia kilichomtia mazonge lakini akakata kunambia."

Bi. Chonde aliinua uso wake na kuwaangalia mahasidi wake kwa hamaki, Bw. Siga aliangalia chini kuepuka mtazamo wa bikizee yule. Macho yake ni kama yalimhukumu kwa kitendo alichokuwa amefanya.

Bw. Vura alikuwa amemkazia macho ya kuogofya lakini Bi. Chonde alikuwa mjasiri kupita kiasi.

"Baada ya kifo cha Arina, ulipata habari yoyote iliyokuwa imesababisha kubadilika kwake kwa kipindi kile kifupi?," mwelekezi wa mahakama aliendelea kumhoji.

Bi. Chonde bila kujibu alifikia kibeti chake kikuukuu akachomoa kitabu fulani na kumkabidhi, naye aliyepewa bila kukifungua akampa jaji.

"Mjukuu wangu alikuwa ameniambia kwamba ningetaka kufahamu chochote kumhusu ningepata humu, nami baada ya kifo chake nikamuita mmoja kati ya rafiki zake akaja akanisomea, ndipo nilipojua chanzo cha kifo chake," Bi. Chonde alielezea mahakama akifuta machozi.

"Nikieleza mahakama kwamba Arina alikuwa anamtaka Bw. Vura kimapenzi itakuwa nasema umbea kweli...mara nyingi nilikuwa nishapata malamishi kutoka kwa mwajiri wake..."

"Huo ni uongo, mwanangu nilimlea akaleleka vema."

"Nikisema mjukuu wako akiwa upeoni pa macho yako alikuwa na tabia tofauti kabisa na kule kazini utapingana na hayo?!"

"Kweli dunia rangirangile; ukweli unaweza kubasilishwa ukawa uongo na uongo ukawa ukweli kujifaidi," Bi. Chonde alisikitika, "lakini kumbuka mabaya mawili hayaungani yakawa zuri moja."

Hakimu alifunguafungua rijala aliyokabodhiwa na mwelekezi wa mahakama kwa haraka kisha akaiweka kando. Alimwangalia Bi. Chonde kwa dharau kisha akageuka na kumtazama wakili aliyemtetea Bw. Vura na mwenzake.

"Ewe hakimu mtukufu, ningependa utoe hukumu yako kulingana na yote ambayo umesikia," wakili alitoa ombi lake mbele ya mahakama.

Pembeni alipokuwa amesimama, Bi. Linda machozi yalimtiririka akafuta kwa kofi lake. Kulingana na mtazamo wake, alijua hukumu ilikuwa ishatolewa hata kabla kesi kusikilizwa.

"Kwa sababu ya kumharibia jina Bw. Vura na kampani lake kwa madai ya uongo," hukumu ilitolewa, "Bi. Chonde ametozwa faini ya milioni tano au shamba lake lililoko Kinondoni."

"But sir...," Bw. Siga alimaka.

"Sheria ishachukua mkondo wake."

Bi. Linda alitoka polepole alipokuwa amesimama hadi mezani pa makarani wa korti, akatoa bastola yake, pingu na kitambulisho cha kazi akaviweka mezani. Watu wote walimwangalia kwa mshangao, lakini aliyestajabia zaidi ni hakimu.

"Inspector! What are you doing?!" hakimu alimuuliza kwa hasira.

"Nimewacha kazi," Bi. Linda alimjibu kwa ukakamavu, "siwezi kuwa naleta wenye hatia mahakamani kuondolewa na kutwishwa wanaodai haki."

"Nani alisema hayo, jaji anakuamuru uchukue vifaa vyako vya kazi mara moja."

"Kwa mara ya kwanza nitakaidi amri ya korti," Bi. Linda alimjibu hakimu kisha akaanza kuondoka.

"Guards! Arrest her!" Hakimu aliamuru askari wa korti, "she has disobeyed court order."

"Yarabi! Mtoto wa watu amefanya nini!" Bi. Chonde alitoa ukwenzi alipokuwa amesimama.

Askari mara moja walimtia mwenzao pingo kisha wakamsukuma korokoroni, kati ya wale walinzi wanne mmoja alionekana kuudhika baada ya amri kutolewa juu ya Bi. Linda.

"Heri tuachane naye," aliwaambia wenzake baada ya kumfikisha korokoroni, "hana ubaya wowote."

"Si' tunafuata amri," wenzake walimjibu kwa pamoja.

Hakimu alivunja kikao kisha akaondoka akionekana msononefu, mbele ya korti Bw. Vura alienda na kumsalimu wakili wake.

"Asante ndugu," Bw. Vura alitoa shukrani kisha kila mmoja wao akaondoka.

Bw. Siga aliwaangalia akatikisa kichwa, Bi. Chonde nyuma yao machozi yalimtoka kama matone ya mvua, uchungu ulikuwa umemzidia moyoni baada ya kufungwa kwa Linda.

***

Mlango ulifunguka kwa ghafla kisha Bi. Alizeti akajitoma ndani kwa fujo, Bw. Nadama alimwangalia mkewe kisha kwa pamoja wakamgeukia binti yao. Bi. Alizeti alisimama pembeni mwa chumba hicho machozi yakimtoka kwa uchungu.

"Tueleze nini kimetokea," Bw. Nadama alimwambia.

"Mwezi sasa unatimia kutoka tulipoonana naye," Bi. Alizeti aliwaambia akifuta machozi, "sijamuona tena kutoka kioja hicho kilipotokea kanisani."

"What!" Bi. Tabasuri alimaka, "and you mean you have not reported to any authority!"

"Niliripoti polisi lakini sijapata chochote kutoka kwao, baada ya tukio hilo kutokea nilipuzilia mbali kwa wiki tatu lakini baada ya kuona kwamba anakawia sana ndipo nilipoamua kuchukua hatua nyingine."

"Wewe hamjali mumeo," Bi. Tabasuri alimkashifu, "majuma matatu bila shughuli yoyote!"

"Maybe he's de...," Labibu alikatizwa kwa mngurumo wa radi uliosikika kutoka nje.

Mvua iliyofuata mngurumo huo ilinyesha kama ambayo ilikuwa na kisasi juu ya insi wote katika jumba hilo, iliandamana na upepo mkali uliotishia kung'oa paa la nyumba hiyo. Kila wao alibaki kimya.

Japo Bw. Nadama alikuwa mtu asiyemjali Bw. Mhifadhi kwa sababu zake mwenyewe, hisia za huruma zilimjia akaanza kumsikitikia Bi. Alizeti. Alimwangalia mkewe kisha akamgeukia bintiye, mgeni wao akatoka polepole alipokuwa mpaka kochini.

Alijionea wivu kwa kuwa mchoyo wa penzi la kweli kwa mumewe wa miaka ishirini na mitano.

"Tutaandamana sote baada ya mvua kupungua, ila usiwe na shaka, atarudi," Bi. Tabasuri alimliwaza.

Mvua ilinyesha kwa masaa mawili, nje kukajaa vijito vidogovidogo vilivyoteremka kutoka kila upande. Mwendo wa saa mbili za usiku walitoka wote wakajitoma garini tayari kwa safari ya kumrudisha mgeni wao kwake.

Safari ilianza, Labibu alimtazama mamake kama aliyekuwa na jambo la kumwambia.

"Lakini hata siku hiyo mwenyewe ulikuwa mchoyo kwa mumeo kiasi cha kumuasi na umati," Bi. Tabasuri alivunja kimya mle garini kwa kumkosoa mwenzake.

"Hayo usemayo ni kweli, la..."

"Kosi si kosa, ila kurudia kosa ndiyo kosa," Bw. Nadama aliingilia kati.

"Si makosa yote hujirudia maishani."

Bi. Tabasuri alianza kukumbuka matukio ya siku hiyo kama mbayo yalikuwa yametokea muda mfupi tu uliopita.

Siku hiyo ya Jumapili ilikuwa kama siku nyingine za kawaida kabla Bw. Mhifadhi hajakuzia uozo ulioenea katika jamii kwa mahubiri yake.

"Kila mtu angekuwa anampenda mwenzake anavyojipenda, dunia ingekuwa pema kuliko peponi," alikumbuka jinsi sentensi moja ilibadili manthari kwa nusu dakika pale kanisani.

"Aisee! Nyamaza kama huna la maana kuhubiri," ghulamu mmoja aliinuka bila heshima kwa mhubiri wake na kutamka yale.

"Kama nyi ndiyo viongozi wetu wa kesho, jamii nzima inaenea uozo," Bw. Mhifadhi alimjibu yule mvulana baada ya kutambua kuwa ni mwenyekiti wa kundi la vijana pale kanisani.

"Kama unataka kuandika biblia nyingine nenda 'kajiunge na wayahudi uyahudini," ghulamu mmoja aliinuka na kumtupia yale maneno, hadhira nzima ikaangua kicheko.

Licha ya matusi aliyomiminiwa aliendelea. Mingurumo ya chini kwa chini ilianza kusikika. Kisha mumewe akainuka na kutoka nje akionekana aliyeudhika. Mwenyewe akiwa amefungua kinywa kwa mshangao, msichana alikuwa nyuma yake naye aliinuka akatoka. Kitambo kidogo vijana watano hivi waliinuka, kisha umati mzima ukainuka na kutoka nje.

Yeye na bintiye walisalia pekee yao wamemtazama mhubiri wao madhebahuni. Kilichomshitua zaidi ni kuwa hata Bi. Alizeti aliungana na waasi kumuacha mumewe.

"Uwe na usiku mwema," maneno yale yalikatiza fikra zake, alipoangalia mbele yao na kuona nyumba ya Bi. Alizeti alishusha pumzi, safirini salama.

"Tukipata habari yoyote tutakupa taarifa, usikate tamaa," mwenzake alimpa imani.

Bi. Alizeti aliitikia kwa kichwa kisha akaanza kuondoka kuelekea nyumbani kwake. Manyunyu yalikuwa bado yanadondoka, walimwangalia hadi alipoingia ndani ya nyumba kisha nao wakaanza safari kurudi nyumbani kwao.