webnovel

CHALLENGE

Mara alipoingia ofisini kwake, Renatha akavuta karatasi kwa hasira akaikunja kwa nguvu zake zote hadi ikawa kimpira kidogo. Akairusha kwa nguvu hadi kwenye mlango, akaendelea kufanya hivyo hadi sauti ya mlango ukigongwa ilipomshtua,

"Aaaaaaarghh, nani tena?" Akainuka na kuelekea mlangoni akainama kuokota zile karatasi, lakini kabla ya kumaliza mlango ukafunguliwa

"Who gave you__" kabla ya kumaliza maneno yale macho yake yakakutana na yake ya Allan ambaye alikuwa katika mshangao wa kile alichokiona

"Aaah samahani Allan" akaachia tabasamu ambalo bila shaka lilishindikana kutoka sababu lilichanganyika na hasira, akainama kuendelea kuokota karatasi zilizobaki

Allan hakuongea chochote bali nae akainama kuokota kitendo ambacho kilimshtua Renatha

"Tafadhali acha tu nitamalizia zimebaki chache"

Allan hakumsikiliza akaendelea kuokota wakati Renatha akiwa amesimama akishangaa kwa nini hamsikilizi.

"Nafikiri ofisi sasa imekaa vizuri. Tunaweza kuongea?" Allan akamuuliza huku akimpita na kuketi kwenye kiti kilichokuwa mbele ya meza ya Renatha.

Renatha akashusha pumzi na kuelekea kilipo kiti chake kuketi. Akamwangalia Allan ambaye uso wake ulijaa tabasamu, akaamua kuanza kujisalimisha kwanza yeye kwa kile alichokifanya

"Mr Nubri na_"

"Niite Allan" akamkatisha

"Oh sawa, Mr Allan_"

"Just Allan" akamkatisha Renatha tena

Renatha akashusha pumzi, "Allan, samahani kwa sura uliyoikuta huku ndani. Nilikuwa najaribu shabaha yangu" akamdanganya Allan

"Hahaha unapenda mpira wa kikapu Renee?" Allan akauliza kwa shauku

Renatha akashtuka swali ambalo hakutegemea kuulizwa, akamwangalia Allan machoni kuona alimaanisha alichomuuliza.

"Ndio napenda Allan." Akamjibu alipojiridhisha na unyofu wa moyo wa Allan

"Ulishawahi kucheza?" Akauliza Allan na msisimko ule ule

Renatha akatulia na kuegama kwenye kiti, "More like Candace Parker"

Allan akashtuka, "Unamjua Candace Parker, oooooh my God.. Naomba tucheze siku moja"

"Aaaaah" ikawa zamu ya Renatha kushangaa

"Okay, tutacheza nusu saa tu, atakayeshinda ana haki ya kusema chochote anachotaka kutoka kwa aliyeshindwa." Allan akamwambia kwa msisimko mkubwa

Renatha akatabasamu kwa furaha, "Sawa. I challenge you to it. Niambie lini"

"Kesho jioni baada ya kazi, nitabeba vifaa vyangu na mpira. Nitachagua mahali tutakapocheza." Allan akainuka na kunyoosha mkono kumwelekea Renatha "Deal?" Akauliza baada ya mkono wake kupokelewa.

Renatha akaachia tabasamu, "Deal". Wakaachana, Allan akatoka ofisini kwa Beno akiwa na furaha asijue kwa Renatha ilikuwa ni fursa adimu kwake kufikia lengo lake.

"You are lovely Allan. Looking forward to our challenge"

Akakunja karatasi na akalirusha kwenye tundu la ndoo ya takataka, "holaa"

************

Aretha alitumia muda mwingi akiwa amelala chumbani kwake kama daktari alivyoshauri.

Muda wa mchana aliamka na kuelekea maliwatoni, aliporudi chumbani kwake baada ya kuoga, akakutana na meseji tatu kutoka kwa Beruya ambazo zilimfanya aketi taratibu kwenye kitanda chake na macho yakaanza kulowana machozi.. lakini kabla hajaendelea kulia mlango ukafunguliwa, mama akaingia na sinia la chakula,

"Inua uso Retha kwa nini unajificha" mama akamuuliza baada ya kuona, hakuinua kichwa kumwangalia

Aretha akainua kichwa na macho yake yaliyo lowana machozi yakaonekana. Mama akavuta hatua na kukaa pembeni ya binti yake.

"Retha" akaita taratibu

"Abeeee" akaitika katika kwikwi za kulia

"Naomba unisikilize" mama akamwambia

"Kila binadamu anabeba nguvu na udhaifu kwa wakati mmoja. Kuna ambao wamekubali kuwa wenye nguvu tu ambao madhaifu yao wamekataa kuyaona. Wanafanikiwa lakini kuna watu wanaumizwa na nguvu zao" akameza mate kisha akaendelea

"Na kuna watu wamekubali kuwa wadhaifu, hawa nao wanaishi katika simanzi, kwa sababu wenye nguvu wanawaumiza. Na wao wamekubali kuumizwa. Lakini kuna watu wamechagua kukusanya nguvu zao na madhaifu yao. Hawa wanalia kisha wanainuka na kukung'uta mavumbi wanasonga mbele" mama akamaliza na kumwangalia Aretha

"Wewe ni nani mwanangu?" Akamuuliza huku kiganja cha mkono wake kikigusa shavu la Aretha kwa kumjali

ตอนถัดไป