Bri akampa ishara atulie kwanza, "Sweetheart nikurudishe chumbani mara moja upumzike tushughulikie hili" akamwambia mkewe ambaye alikuwa na uso wa mashaka baada ya kuona Ed akiwa amebadilika ghafla...
"Okay,.....na Ed jitahidi kuwa na utulivu ili uamue vizuri!" Akainuka akisaidiwa na mumewe wakaelekea chumbani wakimuacha Ed ambaye alikuwa akiangalia baadhi ya namna ambazo zilipita hata kuifanya simu yake kuwa 'busy'. Akajaribu kupiga namba kwenye simu yake ikaita sana hakupokea aliyepigiwa
"Aaarrrgh, Aretha amenizimia simu" Ed aliwaza baada ya kumpigia Aretha ambaye hakupokea na alipojaribu kupiga tena simu ikawa imezima. Bri alirejea kutoka chumbani, akamshuhudia alivyokuwa akiiangalia simu yake, akamwangalia rafiki yake na kutabasamu "hatimaye Ed amempenda mwanamke"
Ed alisimama kwenye dirisha akiangalia nje, moyo wake ulikuwa katika maumivu akitafakari kwa namna gani Aretha atakuwa anamfikiria hadi kuamua kuzima simu. Akageuka na kuanza kuelekea mlangoni,
"Ed, unaelekea wapi sasa?" Brian akamuuliza
Akasimama na kushusha pumzi kwa nguvu kisha akamjibu "niliahidi kumrudisha nyumbani Aretha ngoja niende"
"Subiri bro, nitafuatana nawe___" lakini kabla ya Brian kumaliza Ed akamkatisha
"No, Bri, Rose anakuhitaji hapa,akijisikia vibaya nawe haupo itakuwaje!"
"Okay, sikia nachowaza, kwa nini usimwambie Derrick amfuate Aretha ili wewe upate namna ya kuongea na Lyn__"
"Sitaki kabisa kuongea nae, Aretha kazima kabisa simu, sijui kamwambia nini." Ed akazungumza kwa hasira
"Hey bro, calm down, kama hataki kuongea na wewe kwa sasa, mpe nafasi hiyo.
Natama____" simu ya Ed ikaita tena, mara hii alikuwa Derrick, ikaendelea kuita na wala Ed hakupokea kama ambavyo hakuweza kupokea simu ya Li. Ilipokata akampigia Coletha ili kujua kama Aretha bado alikuwapo nyumbani, simu ikapokelewa
"Hello Bro" Coletha alipokea
"Coletha, Aretha bado yuko hapo nyumbani" Ed
"Yupo huku bustanini, bro ni nini kinaendelea maana Lyn yuko hapa mambo anayomwambia mama yanachanganya"
Ed aliposikia hivyo uso wake ukazidi kuwa na mikunjo ya wazi
"Amemwambia nini?" Akauliza Ed
"Amemuonesha hizo habari za Insta, lakini kasema unamtambulisha hivi karibuni" Coletha akamjibu
"Mmmmmm" Ed akaguna na kumfanya Brian amuangalie akijua hali ya rafiki ni mbaya
"Amesema hayo mbele ya Aretha?" Akauliza Ed
"Ndio bro, halafu Aretha ni nani hasa maana unatuchanganya h____" Ed hakuweza kuvumilia akakata simu akafungua mlango na kutoka, lakini Bri akamuwahi.
"Ed nisikie, Aretha anahitaji muda atulie muongee ndio maana amezima simu. Nisikie mpigie Li au D aje akusaidie kumrudisha la sivyo atakataa kuondoka nawe."
"Hapana, she will understand" Ed akaongea wakati mkono wake ukiwa tayari kwenye mlango wa gari yake..
"Na vipi kuhusu Lyn, utamuacha hapo au utaondoka na wote?" Brian akamuuliza akiwa amemzuia kufungua mlango
"I don't care Brian, akibaki hapo au atembee kwa mguu ngoja niende"
"Ed, pale ni nyumbani kwa mama sio kwako, unataka Lyn apate huruma za mama zaidi" Brian sasa alipaza sauti akionesha kuchoka kumuelewesha Ed..
Ed akamwangalia rafiki yake, akatoa mkono kwenye mlango, akachukua simu yake na kumpigia Li ambaye alipokea mara ilipoita...
"Hello Bro"
"Uko wapi?" Ed akamuuliza mara alipopokea
"Niko na Allan Bronze house , umeangali___" kabla hajaendelea Ed akamkatisha...
"Chukua gari uende kwa mama, tukutane hapo, dakika 15" Kabla Li hajajibu chochote akakata simu.
"Nimefuata ushauri wako...naenda, nitakutafuta baadae. Asante bro" Ed akamshukuru Bri
"Yes, check me later, we need to talk" Bri akamgusa begani na kumuacha rafiki yake aondoke.
"This time, Edrian my friend is in love, Aretha nataka nikuone umewezaje kupasua mwamba hata utoe maji" Bri aliwaza huku alielekea ndani kwake.
Ed wakati akiendesha gari aliendelea kuongea na Captain ambaye alimweleza utafiti wake wa muda mfupi juu ya uwezekano wa mtu aliyepiga picha hizo kuwa na uhusiano na Joselyn. Akakumbuka kumpigia tena Coletha
"Coletha, nisaidie Aretha asiondoke. Nakuja usimwambie"
"Okay Bro, fanya upesi anamalizana na maua sasa hivi" Coletha akanong'ona