Edrian aliketi na Aretha kwenye baraza la juu la jengo hili la Ashanti huku wakifurahia machweo ya jua yaliyoleta rangi ya dhahabu kwenye mazingira yaliyowazunguka. Kwa Aretha ilikuwa mandhari safi iliyompa mawazo mengi ya kuchora picha zake.
"Rian..naomba siku moja nikae hapa nipate kuchora mandhari hii" Aretha akiwa amesimama karibu na mtungi mkubwa wa maua alimuomba Ed
"Unaweza kuja wakati wote, nitakupatia kadi yako ya kuingilia" Ed akamjibu akiwa amekaa kwenye kiti chake
"Unamaanisha watu wengine hawaji huku?" Aretha akauliza
"Yes, ni kwa sababu za kiusalama. Huwezi jua mtu anaweza kupatumiaje mahali hapa. Ili kulinda matukio kama kujirusha chini, ni mimi pekee nina "access" na sehemu hii. Wanaokuja kufanya usafi huja huku nikiwapo."
"Ooh....ni vizuri, usalama ni wa msingi. Na mimi unaamini sitaweza kupatumia vibaya?" Aretha alizungusha macho akiwa ametabasamu
Ed akampa ishara asogee alipokuwa, Aretha akaenda, akanyoosha mkono kumwelekea. Aretha alipompatia mkono, Ed akamvuta na kumketisha miguuni pake, akamsogelea sikioni na kumwambia kwa sauti ya chini,
"Sababu hautakuwa peke yako 'princess', I will be watching you"
Aretha aliyekuwa ameweka mikono yake usoni alitabasamu huku akiinama mbele kwa kuwa sauti ya Ed ilikuwa ikipuliza kwenye ngozi ya sikio lake na kumtekenya.
Mikono ya Ed iliyopita tumboni kwa Aretha ilimpa nafasi ya kulaza kichwa chake mgongoni kwa Aretha.
"Retha" akamuita taratibu
"Mmm" akaitika
"Bado unataka kumtafuta baba?" Akauliza Ed kwa hisia za kujali
"Aahm" Aretha akashangaa
"Tunaweza kuendelea kumtafuta Retha usi__"
"Hapana Rian...usisumbuke" Aretha akamkatisha huku akijaribu kuinuka
"Usiinuke Retha, baki hapa, najisikia vizuri ukiwa mikononi mwangu"
"Eehmm" Aretha akashtuka na kurudi kuinama kisha akaendelea
"Kama yeye hanitafuti nadhani hanihitaji"
Kama msumari wa moto hisia za huzuni zikamchoma Ed akamuinua Aretha kisha naye akainuka. Akamgeuza wapate kutazamana usoni.
"Retha, usipate huzuni kwa ajili yake. Let's be happy. Hata kama siku akija ataona kiasi gani alipoteza mtu muhimu karibu yake" akamvuta na kumkumbatia
"I am here" Ed akasema alimbusu kwenye paji lake la uso. Aretha akatabasamu na kumshukuru Ed..
"Rian...thank you. Wakati wote maneno yako yanaishi ndani yangu."
Wakakumbatiana, Ed alitamani wakati huu usiishe. Kumweka Aretha kwenye mikono yake kwake ilikuwa ni shauku tangu siku ile alipomuona.
"Rian... ninamjua mama, atakuwa ameshakaa barazani ananisubiri nadhani tuanze kuondoka" Aretha akainua uso na kumwambia Ed ambaye alikuwa akichezea nywele zake kwa nyuma...
"Aaaaahhh..sawa Retha. I only want you here" akamwachia na kuondoa chupa zao za vinywaji na kuzitupa kwenye ndoo ya uchafu iliyokuwa pembeni. Wakati huo Aretha alisimama karibu na chuma kubwa lilioweka kuzuia mtu kukaribia mwisho wa ukuta wa jengo, akaangalia mwonekano wa A-Town. Akatabasamu kwa furaha...
"Retha umesahau" Ed akageuka na kuelekea alipokuwa amesimama
Aretha akageuka kwa mshangao akijiuliza amesahau nini, "mhhhh"
"Umesahau 'princess' uliniahidi nini?" Ed akasimama karibu nae akimuangalia machoni..
"Sikumbuki Rian.." Aretha akajitahidi kukumbuka
"Picha yangu uliniahidi"
"Ooooh Rian..nisamehe" Aretha akamsogelea Ed na kumshika mikono mara alipoambiwa alisahau picha..
Ed akatabasamu akimuangalia alivyokuwa ameshika mikono yake,
"Okay, utanieletea lini?"
Aretha akatulia na kuiachia mikono ya Ed akafikiri, "Jumanne?"
"Kwa nini isiwe kesho?" Akamuuliza akiinua nyusi zake juu akitabasamu
"Aahmm" Aretha nae akamwangalia usoni akang'ata mdomo wake wa chini akifikiria asijue macho ya Ed sasa yalimwangalia mdomoni na si machoni tena..
"Haa. .haya sawa nitakuletea kesho"
"Unatoka darasani saa ngapi?" Ed akamuuliza
"Saa saba mchana"
"Utaibeba picha hadi chuoni?" Akauliza Ed
"Yes.. kuna mahali nitaiweka kabla sijatoka darasani"
Ed ambaye macho yake bado yaliangalia midomo ya Aretha "nitakuja kukuchukua chuo ukanipatie picha yangu nyumbani"
"Aahmm" Aretha akashangaa, kabla hajatoa maelezo, midomo yake ikavamiwa na ile ya Ed na busu zito likawapoteza.