webnovel

HE LOVES ME

Edrian aliendesha gari pasipo kusema neno lolote mpaka alipofika nje ya geti la nyumbani kwao Lyn. Kabla ya Lyn kushuka Ed akamwambia

"Nimekupa onyo la mwisho, sitarudia tena ila mtamuona Edrian msiyemjua wewe na baba yako."

Kabla Lyn hajajibu neno lolote Ed akamuashiria ashuke..

"Sawa Ed, nakupenda hata sasa" Lyn akasema huku akishuka.

Ed hakusubiri Lyn afunguliwe geti akaondoa gari na kuelekea kwa Captain. Njiani akampigia Brian,

"Nimefanya kama ulivyosema niambie hatua ya pili, nataka kumuona Aretha Bri, kesho tunatakiwa kuonana."

"Ed, relax. Muamini Aretha kuwa atakupa nafasi muongee.. Mpigie kesho asubuhi. Lakini pia namjua Li atajua namna ya kumuweka sawa... Nenda kwanza ushughulikie ya msingi"

"Okay...Asante Bro!

Akaelekea kwa Captain, Ed alihisi uchovu wa mwili wake wote kwa shughuli za kutwa nzima na bado mambo aliyofanya Lyn yalimzidisha hasira.

**********************

Li alipoondoa gari nje ya geti alimwangalia Aretha mara kadhaa na kugundua binti huyu mawazo yake yalikuwa mbali na sio katika majumba anayoyatazama. Akaamua kuvunja ukimya uliokuwepo kati yao kama ukuta

"Unaweza kujuaje mtu anakupenda Aretha? " Li akaanzia hapo

Aretha akageuza macho na kumuangilia Li kwa mshangao "Aha"

"Nimewaza tu, kujua mtu anakupenda inaweza kuwa rahisi na ngumu kwa wakati mmoja eeh" Li akaendelea

"Mhhh. ...hata mimi sijui" Aretha akajibu

"Fikiria, kama hujui mtu anakupenda, unaweza kuwa unawaza mengine na kufikiri vingine tofauti na yeye" Li akaendelea taratibu

"Na jambo lolote akilifanya unaweza kulihukumu vibaya au vizuri kwa sababu hujui tu"

Aretha ambaye sasa alimsikiliza Li, aliwaza anaelekea wapi na hayo maongezi. Alipoangalia nje akamgeukia tena Li..

"Aaa.. Mbona hatujaingia Avenue kituoni, hapo ndio gari zinaoatikana kwa urahisi!" Aretha akauliza huku macho yake yakimwangalia Li na kurudi barabarani..

"Nitakupeleka hadi nyumbani Aretha, Edrian kaniagiza nifanye hivyo nami nitatimiza maagizo yake" Li akajibu

Aretha akashtuka na akaweka mikono yake kifuani "mmmhhh"

"Aretha" Li akamuita

"Hmmmmm" akageuka kwa aibu zaidi kumuangalia Li

"Unaweza ukachagua kumuamini bro au usimuamini, kwa sababu utakuwa sahihi katika yote" Li akanyamaza kuyapa nafasi maneno haya yamuingie Aretha ambaye alikuwa akitazama vidole vyake.

"Aaahm" alishangaa Aretha, Li akaendelea

"Utakuwa sahihi kwa sababu Aretha humfahamu Ed. Na kama mtu humfahamu ni rahisi kumfikiria vyovyote vile. Kila anachofanya kwako kinaweza kikabeba tafsiri yoyote utakayo" Li akameza mate taratibu na kuendelea

"Mimi nayemfahamu Ed, ninayejua maisha yake ni rahisi kumuamini anaponiambia kitu"

Aretha akafumba macho na kumuuliza Li, "aah unasema haya kwangu kwa nini?"

Li alifurahia swali hilo na kwa ufupi akamjibu "Sababu Edrian Elvis Simunge anakupenda"

"Aaaah" Aretha akashtuka zaidi na hakuweza kumwangalia Li usoni wakati huo..

"Aliponiagiza nikulete nyumbani, hukuniambia nikwambie haya, ila sitaki kumuona akiendelea kuwa "desperate for love" Aretha" akaendelea

"Hujui kwa muda gani tulitamani kumuona anaishi maisha ya kumpenda mwanamke kama ambavyo anafanya sasa tangu akuone"

Aretha aliyekuwa kimya akageuka na kumwangalia kwa haraka Li usoni kisha akamuuliza "lakini anaye__" kabla ya kumaliza Li akamkatisha

"Unadhani mpaka nasema hivyo sijui Aretha kuwa kuna mtu? Kilicho muhimu ni kwamba hajawahi kuwa 'desperate' kwenye hilo penzi kama alivyo kwako. Anakupenda"

"Eeeeh" Aretha akashangaa

"Huo ndio ukweli. Ukiamua kumsikiliza, ukamuamini na kumpa nafasi utakuwa umefanya vyema!" Li alipomaliza kuongea walikuwa wanakaribia Moon street.

Moyo wa Aretha ukapata fukuto ambalo lilikuwa ni matokeo ya kusikia Ed anampenda, akainama huku akichezea vidole vyake..

"He loves me mmm"

Akawaza moyoni mwake, akajisikia vibaya kwa kumdhania Ed kuwa alimdanganya kuhusu kuwepo kwa Joselyn..

"Hakujua kama Joselyn angekuja leo, mengine ambayo una mashaka nayo mpe nafasi atayaelezea mwenyewe, Aretha"

Aretha akashtuka baada ya Li kumpa majibu ya kitu ambacho alikiwaza muda huo huo.. "haaa alijuaje ninachowaza"

Gari ikasimama kwao.

次の章へ