PAH PAH PAH
Ni sauti ya nyundo ya mbao iliyomshtua mfungwa namba 2203 kutoka katika kumbukumbu yake ya siku ya tukio.
"Kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha , kama ni kweli mtuhumiwa alihusika na kifo cha waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, hivyo basi kwa mamlaka niliyonayo ninahairisha kesi hii mpaka tarehe 2 mwezi wa 12 mwaka 2090. Mtuhumiwa ataendelea kuwa lumande mpaka ushahidi utakapo jitosheleza kutoka upande wa wakili wa serikali." Aliongea mzee Yule hakimu wa kesi namba 2003 aliyokabidhiwa yeye kama hakimu na jaji mkuu.
Mfungwa namba 2203 hakuweza kufatilia kilichoendelea kwenye kesi yake, mawazo yake yalikuwa mbali hivyo kufwata kile kilichoamliwa na hakimu. Lakini alifahamu yote yameweza fanikiwa kutokana na mwanamke mmja ambaye yeye ndiye alikuwa akimfahamu na ndiye aliyeweza kuamua ni nini kifanyike na hakimu wa kesi hiyo.
Walinzi waliobeba silaha walimkokota mpaka nje ambapo kulikuwa na gari la kubeba wafungwa. Bila kupoteza muda walielekea katika gereza lililopo mkoani mbeya. Gereza hilo lilitumika kushikilia wafungwa mbali mbali waliotenda makosa mbali mbali ya mauaji , ufisadi, uhaini pamoja na ubakaji.
Viongozi mbali mbali waliopita kutoka serikali zilizopita waliotumia madaraka yao vibaya waliweza shikiliwa katika gereza hilo ambalo linasemekana kuwa na ulinzi mkubwa kuliko gereza lolote nchinin Tanzania. Hivyo kupelekea kupelekwa kwa mfungwa namba 2203 katika gereza hilo pia.
"Nitaweza timiza mpango wetu kweli nikiwa muke ndani? Aliwaza mfungwa namba 2203 huku akitazama nje kupitia madirisha madogo ya gari hilo la wafungwa.
"Nitawamaliza taratibu bila kwa msaada wa wafungwa wengine".
"Nahitaji marafiki kwa sasa? Aliwaza mfungwa namba 2203 huku akijiweka sawa pingu alizokuwa amefungwa mkononi mwake.
Sauti ya helikopta ilisikika na kundi la watu waliovalia mavazi meusi walijitayalisha kwa ajiri ya kurukia juu ya gari lile la wafungwa.
Kishindo cha kitu kizito kutua juu ya gari hilo kilisikika na baada ya dakika moja bomba dogo lilitoboa paa la gari hilo na moshi ulioambatana na chemikali ya usingizi iliingia kwa kasi katika gari hilo.
Dereva na maaskari hao zaidi ya kumi walizimia baada ya moshi huo kuingia katika mfumo wao wa upumuaji, byuma ya gari hilo waliingia watu wawili waliokuwa wamevalia vifaa vya kuzuia moshi huo na moja kwa moja kumchukua mfungwa namba 2203 amabaye wakati huo aliweza kuona kwa mbali akitolewa ndani ya gari hilo na kufungwa kamba iliyokuwa imeunganishwa na helikopta kiunoni mwake. Tukio lilitumia dakika tano tu na mfungwa namba 2203 alitoweka katika eneo lile pamoja na kikundi cha watu wasiojulikana amabao waliimaliza timu nzima ya ulinzi iliyowekwa kwa ajili ya mfungwa 2203.
Helikopta ilienda kwa kasi katika mlima mmoja uliopo jijini mbeya na kutokomea nyuma ya mlima huo. Nyuma ya mlima huo kulikuwa na jingo lililojengwa chini ya ardhi. Sehemu ya chini ya ardhi ilifunguka na helikopta hiyo kuingia chini ya ardhi hiyo ambamo kulikuwa na sehemu kubwa uenye uwazi wa kuweza kuishi watu zadi ya elfu moja.
Mfungwa namba 2203 alianza kupata fahamu na kuona sehemu aliyopo. Kulikuwa na taa kali zilizoweza kuumiza macho yake pale alipofumbua mboni za jicho lake.
"mbebe haraka mpeleke chumba cha mahojiano". Aliongea mmja wa wale watu waliovalia nguo nyeusi.
"sawa mkuu". Walijibu vijana wawili kwa pamoja kisha kumkokota mfungwa namba 2203 kwenye chumba kilichoandikwa "INTERROGATION ROOM".
"Ni nini kimetokea?
"Inamaana huyu mwanamke kaabdilisha mpango bila hata kunitaarifu? Aliwaza mfungwa namab 2203 na kisha kuangalia vizuri mazingira aliyomo bila kujua yupo wapi kutokana na yeye kushindwa kutambua ni wapi alipo.
Baada ya dakika tano aliingia mwanaume mmoja kisha kukaa kwenye kiti kilichokuwa mbee ya mfubgwa namba 2203.
"Jina lako ni dravo anangisye? Aliuliza Yule mwanaume kisha kumtazama mfungwa namba 2203 kwa jicho la udadisi
Ukimya ulitawala baada ya mfungwa namba 2203 kutojibu swali aliloulizwa na mwanaume huyo.
"Au unataka nikuite mfungwa namba 2203? Huenda ni jina amabalo linafaa watu katili kama wewe". Aliongea mwanaume Yule
"ni nini haja ya kuniuliza jina langu wakati mna taarifa zangu zote zinazonihusu mimi? Aliongea mfungwa namaba 2203 huku akimwangalia mtuyule bila kuonesha wasi wasi wowote. Kwa jinsi alivyo tekwa na kuletwa sehemu ambayo hajui ni wapi mfungwa namba 2203 alijua tu kikundi hiki kina mafunzo ya hali ya juu pamoja na teknolojia ya kujua ni nini kinaendelea katika kila kona ya nchi hii.
"Kwakuwa hupendi kupoteza muda basi ngoja nisipoteze muda juu ya hili". Aliongea Yule mwanaume mweusi mwenye mwili uliojazia.
"Ni nani alikutuma kutekeleza mauaji ya waziri mkuu? Aliuliza bila kuonesha wasi wasi kisha kuegama kwenye kiti akisubili jibu kutoka kwa dravo ama mfungwa namba 2203.
"nahutaji kujua ni nani aliyekutuma!!! Aliongea kwa sauti kubwa na kumshtua mfungwa namba 2203 aliyekuwa mbali kimawazo akitafakali ni nini ajibu
"sina muda wa kupoteza juu ya hili".
"Naomba unupatie majibu wakati nakuuliza kiutaratibu".
"sipendi kuuliza maswali kinyume na utaratibu. Maana ni wengi wamepotea katika mikono hii nikitumia njia hiyo ya pili". Aliongea huku akionesha kutopendezwa na chaguo lake la pili.
"hakuna aliyenituma". Alijibu mfungwa namba 2203 kisha kukaa kimya
"kama hakuna aliyekutuma nitajie ulishirikiana na nani kufanya tukio hilo". Aliuliza tena mwanaume Yule huku akisimama na kusogea karibu na mfungwa 2203.
"nimelitekeleza mwenyewe bila msaad wa mtu yoyote". Alijibu mfungwa 2203 bila wasi wasi
"unadhani nani anaweza akaamini huo uongo, hata mtot mdogo huwezi kumdanganya kwa uongo kama huo". Aliongea Yule mwanaume na kisha kupiga simu upande wa pili.
Mlango wa chumba hicho ulifunguliwa na wanawake wawili waliovalia mavazi meusi huku wakiwa wameshika vifaa mbali mbali mikononi mwao.
"viwekeni mezani mje baada ya dakika kumi kutoa maiti. Andaeni pipa la tindikali ambalo tutaupoteza mwili wake kutoka katika uso wa dunia hii." Aliongea mwanaume Yule na wanawake wale kutoka nje baada ya kupata maelekezo hayo.
"unaweza badili mawazo yako , nna kupatia dakika tano za kuniambia ukweli. This is my last chance". Alisema mwanaume yule kisha kuanza kuvuta dawa kwa kutumia sindano na kimiminika chenye rangi ya bluu kuingia taratibu kwenye bomba hilo.
Dravo aliinama chini baada ya kuangalia anachokifanya mwanaume yule.
"Hawa watu ni wakina nani? Mbona mpango wetu pamoja na mwanamke yule hauendi sawa kama tulivokubaliana. Nilihitajika kuwa gerezani kwa wakati huu nikiwa nasubilia hukumu yangu ya mwisho, ili niweze pata nafasi ya kuweza kuwamaliza watu wale. Linda au umewatuma watu hawa kwa kuwa umebadili mpango?
"mmh…hapana hawezi badili mpango bila kumtuma mtu wa kuniambia mapema kuhusu mabadiliko yoyoyte". Hayo yote aliyawaza dravo ndani ya dakika chache na alishtuliwa baada ya kuisikia sauti ya mwanaume yule.
"Nadhani sasa utakuwa tayari kuniambia ulishirikiana na nani kutekeleza tukio hilo. Unaweza niambia ni nani aliyekusaidia kupata silaha yenye ubora kama ule. Risasi iliyotumika imetoka katika aina ya silaha mpya iliyotengenezwa nchini urusi "colt revolving snippling rifle." Alisema mwanaume yule kisha kuangalia mabadiliko yoyote katika nyuso ya kijana huyo aliyekuwa amefungwa na pingu zinazotumia teknolojia ya kielektoniki.
"Sina jibu lingine zaidi ya hilo nililokupatia mwanzo, niko tayari kwa chochote nimejikamatisha kwenye mikono ya serikali kwa sababu sina chochote cha kupoteza kwa sasa." Alisema dravo bila kuonesha hisia yoyote usoni mwake na kumshtua mwanaume yule ambaye alitarajia kuona wasi wasi kutokana na vitisho alivyovitoa lakini viligonga mwamba mbele ya mwanaume huyo.
"Hivyo kunitoa katika mikono ya serikali ni pamoja na kufanikisha kazi yangu ya kuonesha maovu aliyotenda waziri mkuu. Nadhani ninyi mnaweza kuwa vibaraka zake haiwezekani mtumie nguvu kubwa kunichukua mikononi mwa askari wa magereza na kunileta sehemu hii isiyojulikana." Aliongea dravo huku akitabasamu
"Nadhani ukweli uliotolewa ile siku ya tukio haukuweza kuwaingia akilini, mnadhani kwamba mpo sehemu sahihi kumbe sehemu mliyopo sio sahihi."
"Niko tayari kwa chochote ulichojiandaa kukifanya juu yangu. Sidhani kama mlinikamata ili mnihoji maswali hayo; mmenikamata ili muweze kulipa kisasi juu ya kuuawa kwa kiongozi wenu, mliyemtumikia bila kuuliza kwa nini anawapa amri hizo za kuwaua watu wasiokuwa na hatia, watu walioongea ukweli juu ya utekelezaji wake wa kazi kutokuwa sahihi." Aliongea dravo
"Kuwa makini kwa unachokisema ,sidhani kama unachokiongea umekifanyia tafiti. Sisi tumetekeleza mauaji hayo kwa kuwa watu wale walikuwa wanatishia amani ya nchi. Hivyo hatujafanya kosa lolote kuwaangamiza watu hao." Alisema mwanaume yule akisogea karibu ya dravo.
Vuta kuendelea kujisomea. Maoni yako ni muhimu sana nisichoke kuendelea kuandika.
Like it ? Add to library!
Have some idea about my story? Comment it and let me know.