Maeneo ya fukwe ya bahari,kambi kubwa ilisimamishwa ya msafara wa kijana wa kwanza wa mfalme Hadas,Zolan.Alikuwa akirudi nyumbani kutoka kwenye ghafra falme jirani.Alikuwa akitegemewa kuwa mrithi wa kiti cha enzi cha baba yake baada tu ya kurejea
Akiwa zake chumbani anajiandaa kwa kulala,akahisi uwepo wa mtu karibu na maeneo yale.Hakuona mtu hata hivyo.
"Sijui kwanini nahisi kama kuna mtu."Akasema lakini hatimaye akaamua kwenda kuangalia nini au nani.Kwa mbali baada ya kuzunguka vya kutosha, akaona kitu ambacho kilikuwa kiking'aa kwa mbali karibu na pale.Zolan ikambidi asogee kujua ni kitu gani hasa.
Hakuamini kumuona mtu akiwa Kalala kwenye maji na mchanga baridi kama wa fukwe.
"Uko sawa?"Akauliza Zolan lakini hakujibiwa.Ikambidi amgeuze na hapo ndipo alipokutana na sura ya mwanamke mrembo sana.Alipomtaza vizuri akagundua kwamba kuna jeraha kifuani mwake yule mtu.
Haraka akambeba tayari kwa ajili ya kumpa huduma ya kwanza..
"Muite daktari haraka.!"Akaagiza na daktari akaja ambapo akampa matibabu ya awali Zebrana.
"Atakuwa sawa kweli huyu?"Zolan akauliza.
"Cha muhimu ni kwamba yupo hai.Atapona taratibu."Akasema daktari.Zolan akatabasamu na kumlipa pesa zake daktari kwa kazi nzuri.
"Hapana bwana,sikupaswa kulipwa.Hii ni kazi yangu."Akasema daktari.
"Hii ni furaha yangu kwako ndiyo maana nimekupa pesa."Zolan akasema na kumfanya daktari atabasamu.Akapokea pesa zake na kutoka taratibu akiahidi kurudi tena kumtazama Zebrana.