webnovel

KWA NINI NIKUAMINI

"Uliipata wapi hiyo love bite Joselyn" ilikuwa sauti ya Ed ambaye alijitahidi kutoonesha hasira ambayo ilikuwa wazi katika mtetemo wa sauti yake.

Akiwa amekaa kwenye ubao wa kitanda, na macho yake yakimwangalia Joselyn ambaye alikuwa akitetemeka huku akifinyanga vidole vyake.

Dakika moja ilipita bila majibu kutoka kwa Joselyn

"Damn it, this is the last time am asking Joselyn, explain to me"

Aliuliza kwa dalili zote za kupoteza uvumilivu. Aliinuka na kumsogelea Joselyn ambae alirudi nyuma kwa uoga..

Akainama kufikia uso wa Joselyn

"Kwa vile huna cha kusema, it's over! Leave my house immediately before I hurt you."

Joselyn alipigwa na butwaa na kuamka kwenye usingizi wa mawazo aliokuwa nao, akarukia mkono wa Ed na kumshika akiwa amepiga magoti.

"No, usifanye hivyo Ed, babe am sorry haitatokea tena. Sikufanya chochote amini nakwambia."

Ed ambaye sasa alikuwa amesimama kwa kitendo cha kushikwa mkono na Joselyn.

Alimuangalia kwa macho makali hata kumfanya Joselyn auachie mkono aliokuwa ameushika

"Ed naomba unisikilize kweli sikufanya chochote ni mtu alinivamia na kutaka kunilazimisha lakini nilijinasua naomba uniamini"

Baada ya kimya kifupi kicheko chepesi kilisikika kutoka kwa Ed kisha akaendelea

"Kwa nini hukuniambia muda wote tuliokuwa tunachat wakati niko safari? And why should I believe you Joselyn?"

Joselyn alikamata mguu wa kulia wa Ed huku akilia

"Ungeniamini kama ningekwambia Ed? Kila mara umeamini mambo ambayo ndugu zako wanakuambia kuhusu mimi, hawanipendi najua, lakini kama ningekwambia ungeenda kuwauliza. Na kama wangekataa ungeniona muongo Ed"

Ed alikuna shingo yake kwa nyuma akifikiria aliyosema Joselyn kiasi yana ukweli maana alimkabidhi Joselyn kwa ndugu zake kabla ya kuelekea SA Country kwenye mkutano wa wafanyabiashara wa madini.

Aliamini ndugu zake watampa taarifa zote za Joselyn akiwa huko. Lakini hawakumwambia chochote na mwisho anashangaa kumkuta na alama katika shingo yake iliyoonesha wazi ni matokeo ya busu la kimahaba.

Akavuta pumzi ndefu, akamuangalia Joselyn kisha akasema

"Ni nani aliyekulazimisha?"

Joselyn aliposikia swali lile moyo wake ukaruka kwa furaha akainua uso wake na kumuangalia Ed akiendelea kutunza uso wa huzuni,

"Naomba usimfanye chochote Ed" akamsihi kwa sauti ya kubembeleza.

"Who is he? Speak Joselyn" aliunguruma Ed na kumfanya Joselyn ashtuke. Akainama na kuachia tabasamu la dharau kisha akasema

"Ni Derrick, but please usifanye chochote Ed..."

"Derrick mdogo wangu au unamuongelea nisiyemjua?"Aliuliza Ed huku moto wa hasira ulionekana dhahiri kwenye macho yake.

"Ed please, Derrick bado kijana naomba uone ni makosa katika ujana na hata...."

"Shut up Joselyn and answer me." Sauti ya Ed iliunguruma sasa na kumfanya Joselyn atetemeke maana huyu Ed anayemuona alimtisha. ..

"Ni shem Derrick ... Ed nakuomba sana...."

Kabla hajamaliza alishtuliwa na mguu uliomsukuma kando, na wakati huo Ed alikuwa amefika tayari mlangoni na kutoka huku akishuka ngazi kuelekea kwenye sebule kubwa iliyokuwa chini. Hatua zake ziliwafanya waliokaa sebuleni kushtuka na kabla hawajasema chochote Derrick alikuwa chini kwa kibao kimoja kutoka kwa Ed.

"Unawezaje kumgusa shemeji yako wewe mwanaharamu"

Kabla Derrick hajapata nafasi ya kumjibu mikono ya Ed ilikuwa imembana shingoni na kumfanya ashindwe kupumua. Alijaribu kufurukuta akashindwa. Ilikuwa ni zamu ya Coletha na Linus kumsihi kaka yao kumuachia Derrick.

"Kaka Ed nakuomba hebu muache kwanza Derrick tusikie nini amefanya?" Alisema Coletha huku akijaribu kushika mikono ya kaka yake ambae alipogeuka kumwangalia alitaharuki kwa ule wekundu uliokuwa kwenye macho kama miale ya moto.

Linus alimsogelea Ed na kumshika mikono kwa nguvu mpaka alipohakikisha Derrick anaweza kuhema vyema akamwambia

"Hebu mwachie bro, tuongee kwanza, huna sababu ya kutumia nguvu, kama Derrick kakosea nitamuadhibu mimi mwenyewe"

Ed alimwangalia Linus na kisha akaachia mikono yake kwenye shingo ya Derrick ambaye alishuka chini akihema huku Coletha akisogelea na kumkumbatia ndugu yake huku machozi yakimtoka alimpeleka lilipo kochi akae.

Ed akamgeukia Linus na kumwambia,

"Make sure simuoni hapa nitakaporudi jioni."

Aliondoka na kuelekea ghorofani akiwaacha ndugu zake wasijue nini kimetokea.

Linus alisogea na kumshika Derrick bega, akamwambia

"Hili tulilitegemea, usijali ninajua huyo nyoka kashamjaza uovu kaka. Acha hasira zake ziishe nitazungumza nae bila shaka. Wala msimkasirikie." Alipomaliza Coletha alifuta machozi na kumshika mkono Derrick wakaondoka kuelekea chumbani kwa Derrick.

************************************

MBWEHA ALIYEVAA VAZI LA KONDOO

Baada ya Ed kuelekea sebuleni, Joselyn alifuta machozi na kuachia tabasamu kisha akasema

"Ngoja tuone kama utastahimili hasira ya kaka yako Derrick"

Akajiangalia kwenye kioo kilichokuwa kwenye kabati kubwa la nguo akaachia kicheko na kujitupia kitandani..

"No one messes with me, umejua siri yangu ndogo nitahakikisha unajuta kunifuatilia."

Aliposikia hatua kwenye ngazi, alishuka kitandani na kujikunyata pembeni ya kitanda huku kichwa akikiweka juu ya magoti. Aliendelea kuvuta mafua mepesi kuonesha ishara ya mtu anayelia, huku kwikwi za kilio zikufuatia..

Ed aliingia kwenye mlango ambao ulikuwa wazi kama alivyouacha na kuelekea alipokuwa Joselyn akamuinua alipokuwa na kumkumbatia. Uso wa Joselyn ulipotea kwenye kifua kipana cha Ed huku akiendelea kulia na kutoa sauti ya kwikwi ya hapa na pale.

"Am sorry Joselyn, please usiendelee kulia. He will leave this house." Alisema Ed kwa sauti yake tulivu huku akichezea nywele za Joselyn.

"Lakini, ataenda wapi Ed, ungemuacha tu" alisihi Joselyn

"Kwa nini nimuache Lyn, unadhani nitamuacha kwa kile amefanya?" Aliuliza huku akimsogeza mbele Joselyn ambae alikutana miale ya moto yenye ukali kwenye macho ya Ed.

"Hapana babe, ila jitahidi usimfukuze bila msaada, still he is your brother" alisema Joselyn kuonesha anamfikiria sana Derrick.

"Mmm!" Aliguna Ed kisha akamwachia Joselyn na kuingia bafuni.

Joselyn alitabasamu na kukaa kitandani kwa furaha kuwa mtego wake umenasa. Alijua hakuna namna Ed anaweza kubadili maamuzi ya kumfukuza mdogo wake Derrick. Akainua mkono na kushika ile alama iliyokuwa kwenye shingo yake, akacheka kwa sauti ya chini.

"Huniwezi Derrick"

Akaangalia kwenye mkoba wake akatoa simu yake na kuanza kutuma ujumbe huku akitabasamu. Baada ya dakika kumi Ed alitoka bafuni na kuelekea lilipo kabati lake la nguo. Akatoa shati ya mikono mifupi yenye miraba na suruali nyeusi ya kadeti, akaanza kunyoosha kwenye meza ya kunyoosha iliyokuwa pembeni.

Joselyn alibaki akiangalia mwili wa Ed huku aking'ata mdomo wake wa chini. Mwanaume huyu akiwa ndani ya taulo ilikuwa ni mateso tosha kwake kwa jinsi alivyojengeka misuli kuonesha alikuwa ni rafiki mzuri wa Gym. Akatamani kumsogelea lakini akakumbuka onyo alilopewa na Ed kuhusu kujitunza. Ed alimwambia hataki kumtumia kama mke kabla ya ndoa. Hivyo toka afahamiane nae aliwahi kufanya nae mapenzi mara moja na yeye mwenyewe akiwa ni sababu ya kushindwa kustahimili kwa Ed sababu alimuwekea dawa kwenye kinywaji chake.

Joselyn alishtuliwa kutoka katika dimbwi la mawazo na Ed ambae alikohoa akiwa amesimama mbele yake.

"Hey nataka kuvaa, kasafishe baby face yako bafuni umeiharibu na machozi" alimwambia na kumbusu kwenye paji la uso.

"Aah haya, I love you Ed" alisema Joselyn kisha akainuka na kumuacha Ed akitabasamu kwa maneno yale.

Baada ya kuwa amevaa vyema, alimalizia kwa kujipulizia manukato yake ya THEME na wakati huo Joselyn aliingia akitokea bafuni. Alijiweka vizuri na vipodozi vyake huku akijiangalia kwenye kioo.

"Umezipenda zawadi zangu?" Ed alimuuliza huku akiweka laptop yake kwenye begi lake.

"Asante babe! Nimezipenda sana." Alijibu Joselyn

"Usisahau kuzichukua" alimkumbusha na kisha akasimama ili kuondoka.

Joselyn alibeba mifuko miwili iliyokuwa na gauni nzuri mbili huku mfuko mwingine ukiwa na viatu.

Wakashuka pamoja hadi kwenye mlango wa kutokea ambapo walikutana na Linus.

"Nitaendesha mwenyewe, shughulikia suala la Derrick nikirudi nisimkute" Ed alimwambia Linus ambaye mara nyingi humuendesha kaka yake kumpeleka ofisini. Aliitikia na kugeuka huku macho yake yakikutana na ya Joselyn ambaye alitabasamu. Linus alipiga hatua kwa uchungu huku akiapia kulipiza kile alichofanyiwa mdogo wake Derrick.

"Just wait Joselyn. Just wait" alisema moyoni Linus.

Alielekea chumbani kwa Derrick, ili kuangalia nini cha kufanya ili kumsaidia mdogo wake. .

Alifungua mlango na kujiunga na ndugu zake waliokuwa wakiendelea kujadili mambo ambayo yanaendelea kwa kaka yao Edrian tangu alipokutana na Joselyn ambae ni binti wa moja ya watu maarufu kwa uuzaji wa madini ya dhahabu na almasi.

Next chapter