1 CHAPTER ONE

STORY: HEAVENS CAN WAIT

Maamuzi niliyoyafanya siku ile sikuwahi kuyafanya siku yeyote kabla ya hapo, hata mimi nilishangaa kwa maamuzi niliyoyafanya siku hiyo, kila mtu akutegemea kama ningeweza kukisema kile ambacho niliweza kukisema, familia yangu ilihisi pengine ninachanganyikiwa kwa maamuzi yale, ukweli ni kwamba sikuwa na jinsi bali kufanya maamuzi yale. "Siwezi kuitoa hii mimba kwaajili ya kuilinda heshima ya familia yangu, ndio nimebakwa, ndio nimefanyiwa ukatili lakini ni kosa gani kiumbe hiki kilichoko tumboni kwangu kimefanya? Siwezi kuitoa mimba hii na haya ndio maamuzi yangu ya mwisho" Niliongea bila kujali ni yapi yangenikuta kwa kufanya maamuzi hayo, Zilikuwa zimebaki siku chache tu nifunge ndoa na mwanaume ambaye familia yangu ilikuwa imemchagua. Nilishika ujauzito baada ya kubakwa na mwanaume ambaye niliamini simfahamu kabisa na familia ilitaka niitoe mimba ile kwasababu nilikuwa ni mchumba wa mtu tayari kwa ndoa siku chache zijazo.

Baba na mama yangu hawakuwa tayari kabisa kukubaliana na maamuzi yangu, walijaribu kila njia kunishawishi hata kwakusingizia kuwa ile mimba ni ya kijana ambaye alitaka kunioa lakini juhudi zao ziligonga mwamba kwani sikuwa tayari kushirikiana nao katika huo mpango. Muda wote huo Lewis mwanaume ambaye alitakiwa kunioa hakuwa na taarifa yeyote kuhusu kinachoendelea bali familia yangu tuu, na kwaupande wa familia yake waliendelea na mipango ya harusi kwani ni siku chache tuu zimesalia ili mtoto wao wa kipekee kuweza kufunga pingu za maisha.

Familia ya Lewis ilikuwa ni familia ya watu wa hali ya juu yaani "First Class Family" mali kwao ilikuwa sio tatizo, Baba na Mama mzazi wa Lewis walimpenda sana kijana wao kwani ndiye mtoto pekee aliyebakia baada ya ndugu zake watatu wa kiume kufariki dunia baada ya nyumba yao kivamiwa miaka ishirini na tano iliyopita, wakati huo Lewis alikuwa na umri wa miaka sita tuu, Hivyo yeye tuu ndiye aliyesalimika, kwani wazazi hawakuwepo nyumbani watu wale wabaya walipoamua kuvamia, lengo lilikuwa kuwapoteza familia nzima lakini kwa bahati Baba na Mama Lewis hawakuwepo nyumbani usiku ule.

ITAENDELEA SEHEMU YA PILI...🙏❤

avataravatar