"Eeeeh! Anaweza kuwa ni yeye? Li akahoji kwa mshtuko
"Bado sijang'amua lakini nina uhakika wa kitu kimoja, he is up to no good!"
"Vipi kuhusu Aretha anaelewa hivyo? Ulisema amenunua picha zake zote pamoja na chache za Beruya itakuwaje sasa?" Akauliza Li kwa hali ya kujali
"Nahitaji kupata namna ya kumfanya Aretha aone ukweli. Anyway, Mjinja amesema atawasilisha hati ya mauzo ya hisa kwa Martinez. Tunaanza kushughulika na shetani hivi karibuni"
"Hahahahaha shetani kweli aisee" Li akacheka kufuatia maneno aliyosema kaka yake.
********
"Hello bosi, Renatha anaomba kuonana nawe?" Sauti ya Loy kwenye simu ikipenya masikioni mwa Ed aliyeketi ofisini akibonyeza kompyuta yake akipitia ripoti na kutuma mrejesho wa barua pepe ambazo zilihitaji majibu kutoka kwake.
Akasugua taratibu paji la uso wake kisha akashusha pumzi na kumwambia Loy amruhusu aingie, ingawa alitamani ayatumie masaa yake vizuri ili baadae apate nafasi ya kumtembelea mama yake, asingeweza kumzuia mgeni huyu.
Edrian akainuka na kujinyoosha huku akiangalia mlangoni ambapo Renatha, aliingia. Akarudi kuketi kwenye kiti chake,
"Habari ya asubuhi bosi?" Renatha akasalimia
"Salama Renatha, nikusaidie nini?" Edrian akamuuliza huku akirudisha vidole vyake kubofya vitufe vya kompyuta taratibu
"Bosi, nimemaliza kuandika chapisho la kwanza la Tathmini, nikaona nikuletee katika nakala ili utoe maoni yako iwapo kuna mahali unahisi sijaandika vyema."
Edrian akainua kichwa chake na kumtazama, kisha akapokea karatasi kutoka mkononi kwa Renatha akaiweka pembeni,
"Kwa nini unanisaidia Renatha?"' akamuuliza kisha akaegama kichwa kwenye kiti akimuangalia machoni huyu dada
"Mr Simunge sikusaidii tu natimiza wajibu wangu" akajibu Renee akikaza macho yake kumwelekea Ed
Akazidi kumtazama Renatha, tabasamu lake la awali likizidi kupotea na sura ya kazi kuchukua nafasi
"Wajibu wako ni kuiambia wizara kile umekiona katika utendaji wetu, unachofanya kinaondoa maana ya wewe kuwa hapa. Ni kama mimi ndie niliyekuajiri."
Renatha akacheka kicheko chepesi kisha akamjibu "Ninachofanya mimi si kuchochea ubaya kuhusu SGC bali ni kuonesha kipi kinahitajika kuboreshwa ili utendaji wenu uwe na ufanisi"
"Ed akarudisha tabasamu, "Basi sawa, nashukuru Renatha. Nadhani baadae hutakuja kunidai kwa hizi favors unazonipa"
"Hahahha nitadai chakula cha jioni na bosi wangu" Renatha akasema wazi kile alitamani
"Ikiwa sitakubali?" Akauliza Ed akiinua nyusi zake juu
"Nitaendelea kujaribu mpaka ukubali" Renatha akasema huku akigeuka ili kuondoka
"Kwa nini 'dinner' na mimi?"akauliza Ed
Renatha akasimama tayari akiwa mlangoni, "Tufahamiane tu" akajibu na kuendelea kusimama pale
"Why over dinner?" Ed akauliza..
"Kufahamiana nje ya mzunguko wa kazi ndio kuna uzito zaidi. Umekubali Mr Simunge"
.
Ed akaachia tabasamu baada ya sura ya Renatha kuwa kama mtoto ambaye anaomba ruhusa kwenda kucheza..
"Hapana Renatha, sipendi 'favors'" Ed akarudisha macho kwenye kompyuta.
Renatha akatabasamu, "Sawa bosi, naamini ipo siku" akafungua mlango na kutoka.
Sura ya Renatha ikabadilika alipofunga mlango wa ofisini kwa Ed. Akakunja ngumi mikono yake akashusha pumzi kwa hasira kabla ya kupiga hatua kuondoka, akisahau kuwa pale aliposimama Loy alimuona kutokea ofisini kwake.
"Huyu amepatwa nini huko ndani, anadhani bosi ni asali kila siku aaah, acha yampate kiherehere kimuishe. Angeacha hizo nakala hapa yasingemkuta" akawaza Loy
Kumbe Allan pia alimuona Renatha alipotoka, akapiga hatua kumsogelea Loy
"Loy, Renatha alikuwa na shida gani kwa Bro?"
"Hahaha unasema mara zote mimi ninapenda umbea, sasa bosi wangu unaniuliza nini hiki" Loy akauliza huku akicheka
"Loy, unanijibu au nikuanzishie vita kwa Bro?" Akamtania
"Baaaasi, natania. Alipeleka nakala za Tathmini"
"Hivyo tu?" Akauliza Allah
"Ndio, kwani kuna nini bosi eeeh?" Loy akashangaa
"Basi sawa." Allan akaelekea mlangoni na kutoka
"Anamfuata Renatha au anaenda wapi bosi wangu. Ni nini kinaendelea kwa wawili hawa?" Akajiuliza Loy kisha akaendelea na kazi yake.
***********
Allan akapiga hatua mpaka ofisini kwa Beno, akagonga mlango.