"Retha utanikubali niwe mume wako?" Edrian hakujua nini kilimsukuma hata swali hili likamponyoka na kutoka mdomoni. Macho yake yalimwangalia Aretha ambaye ni wazi alishangaa, hakuwa na uhakika wa kile alichokisikia.
Macho yake akayaelekeza moja kwa moja kwa Edrian, akawa kama mtu aliyeshtuliwa na taarifa asizozitegemea. Akatoa mikono yake na kuikumbatia tumboni mwake, bado alitamani asikie mara ya pili, alihisi hakusikia vyema
"Rian, umeniuliza sawa au nimesikia vibaya"
"Ahmmm" Edrian akaitika kama aotaye ndoto, aligundua ni mapema mno kwa swali hili kutoka kwake. Alipoona macho ya Aretha yalikuwa katika uhitaji wa kusikia swali mara ya pili akaamua kulipa sura nyingine
"Sorry Retha, ninamaanisha una ndoto za kuolewa siku moja?"
Eeh. .aaah...na..ooh Rian kwa nini umeniuliza hili swali? Aretha akarudisha swali kwa Edrian.
"Why Retha aah! Aaaahm...I love you that's all"
Aretha akayarudisha macho pembeni baada ya kusikia ukiri wa Edrian kuhusu mapenzi yake kwake...
"Rian"
"Naam" akaitika Edrian ambaye hakuondoa uso wake kumwangalia Aretha. Aliona fahari kuyaangalia macho yake ambayo alipokaza kumuangalia aliyakwepesha kwa aibu. Kuna namna alijisikia raha kila mara Aretha alipohangaika kuyakimbia macho yake.
"Aah ndoto yangu ni kuwa na wewe, kama kuolewa kutanifanya niwe nawe nitaolewa"
Edrian hakujua nini afanye nini maana maneno yale yalikuwa matamu kiasi kwamba alimvuta Aretha kifuani kwake akisahau walikuwa kwenye gari muda ule.
"Asante Retha, Asante sana princess" maneno haya yakamtoka Edrian
"I love you" sauti ya chini ikasikika kutokea kifuani kwa Aretha.
Alipomwachia, akawasha gari na wakaondoka mahali pale kuelekea nyumbani kwao Aretha.
"Retha V, atakuletea watu wawili kwa ajili ya "make over" ya jumapili." Edrian akamwambia baada ya kusimama kwenye geti la nyumbani kwao Aretha.
"Asante Rian"
"Usisahau ushauri wa Beruya, endelea kuchagua picha unazoweza kuzielezea. Natamani ningekuja ili nisaidie lakini nina maandalizi ya mkutano wa bodi." Edrian akamwambia
"Hamna neno Rian, nitafanya vizuri katika kuchagua picha, nitafanya kama alivyonielekeza. Endelea na kazi bila shaka. I will do my best" Aretha akamhakikishia Edrian
"Sawa. Msalimie mama na Frans." Edrian akamuaga Aretha
Aretha akataka kushuka lakini kwa haraka alivyogeuka na kumbusu shavuni Edrian aliyeachia tabasamu kwa shtukizo la busu.
"I love you" aksema na kisha akashuka kwenye gari. Akafungua mlango wa nyuma na kutoa begi na mfuko uliobeba magauni yake na viatu.
Akatembea kuelekea getini akimuacha Edrian akimwangalia na tabasamu la furaha usoni kwake.
"Retha asante" akasema kwa sauti ya chini, akawasha gari na kuondoka.
*****************
Aretha akaingia ndani kwao kwa furaha nyingi, lakini akakutana na sura iliyojaa majonzi ya mama yake ambaye alishtushwa na uwepo wa binti yake mle ndani kwa ghafla. Akajaribu kuficha machozi yaliyoanza kulowanisha uso wake
"Mama kuna nini?" Akauliza Aretha huku akishusha mizigo yake karibia na mlango wa kuelekea vyumbani.
"Aahg..mh. .hamna kitu mwanangu, vipi leo mmewahi kurudi eeh!" Akajaribu kuweka sauti yake isikike vyema lakini ilikuwa rahisi kutambua alikuwa katika majonzi kwa muda
"Mama" akaita kwa hamaki kidogo
"Retha, acha kupiga kelele bwana, kuna nini kwenye hii mizigo binti yangu?" Akauliza japokuwa alifahamu kabisa kuwa Edrian alimpeleka kwenye manunuzi ya nguo kwa ajili ya onesho la jumapili. Edrian mwenyewe alimpigia simu wakati akimtaarifu kuhusu ratiba ya Aretha.
Mama tayari alisogea ilipokuwa mifupi na kuanza kuchungulia huku tabasamu likiumbika usoni pake na kuficha huzuni ambayo mwanzo ilionekana.
Aretha akiwa amesimama hakuelewa kwa nini mama yake hakutaka kuongelea kile kilichokuwa kikimsumbua.
"Mama kuna shi_"
"Shhh Retha, hebu twende tukaone unavyopendeza na hizi nguo" mama akasema na kunyanyua mifupi akapiga hatua kuelekea chumbani kwa Aretha.
Nyuma yake Aretha alifuata huku akitafakari nini kilimpata mama yake na hataki kukiongelea.
"Mama, Frans yuko wapi?" Akauliza mara walipofika chumbani kwa Aretha
"Retha wewe, Njoo upime nikuone!" Akajibu mama