webnovel

WATU WAWILI

Derrick alipoingia ofisini aligundua moja kwa moja kuwa kaka yake hakuwa kwenye kawaida yake. Edrian alikuwa amesimama akiangalia nje kupitia kwenye dirisha la kioo lililokuwa mbele yake. Mandhari ya mji mchana ule haikuwa na mvuto wowote lakini macho yake yalitazama vioo vilivyopokea mng'ao kutoka katika mwangaza wa jua.

Akageuka taratibu na kumsalimu Derrick ambaye hakusubiri aambiwe nini kinaendelea akapanda na swali kwa kuwa yake

"Bro, nini kinaendelea?"

"Edrian akaketi taratibu, akashusha pumzi kwa uchovu akaendelea, "nahitaji kupata taarifa ya yule kijana ulimuona akiwa na Joselyn"

"Eeeh!" Derrick akashangaa, Edrian akamueleza kwa ufasaha kwa nini alihitaji kumfahamu na nini mpango wake.

"Bro umekuwa soft kweli kwa Lyn.. jioni nitaifanya kazi na majibu utayapata mapema."

"Soft aah" alirudia taratibu Ed.

"Ila bro usiwaze mchezo umepata wachezaji. Atapoteza tu"

"Hahahha D unaona kama navyoona" angalau uwepo wa D ulifanya uso wa Ed kurudisha hali yake ya awali.

"Na kitu kingine bro, kuna watu wawili tofauti wamekuwa wakiulizia kuhusu Aretha chuoni..Charlz kaniambia wanaonekana kutohusiana na___"

Edrian akasimama ghafla na kumkatisha mdogo wake, "D kwa nini hujaniambia taarifa muhimu hivi ta__"

"Bro, tulia kwanza, mbona bado taarifa yenyewe tunaifuatilia kujua ukweli wake. Watu wenyewe ni wanafunzi inaweza ikawa ni kawaida tu ku__"

D, usirahisishe, kama walikuwa hawamtafuti mwanzoni kwa nini waanze sasa hivi. Nipe namba ya Charlz" Ed akaonesha msisitizo wa kile alichotaka hadi Derrick hakuwa na namna ya kumkwepa. Akampatia namba huku akitabasamu

"Natumaini Aretha anastahili juhudi hizi" akaongea kwa sauti ya chini ambayo Ed hakuweza kusikia kwa kuwa alikuwa akimpigia Charlz.

Baada ya mazungumzo na kupewa taarifa kutoka kwa Charlz, Ed akaagana na mdogo wake kisha akaendelea na kazi. Mchana ulipita kwake bila kupata chakula cha mchana, japokuwa Loy alitaka kumuagizia lakini alikataa. Hakuwa na hamu ya kula bali alimudu kuiweka akili yake kwenye mambo ambayo wakati huo yalikuwa ya muhimu kwake. Alipomfikiria Aretha na hao watu wanaomuulizia alikosa kabisa utulivu.

Muda wa wafanyakazi wengine kutoka ulipowadia Ed hakuona sawa kuendelea kubaki ofisini. Akaagana na Allan ambaye naye alitoka ofisini, siku hii wote walitoka mapema.

Renatha ambaye alikutana nao kabla ya hawajaingia kwenye lifti maalum iliyowashusha mahali pa maegesho ya VIP, akajichomeka na kushuka nao.

Allan kwa kusoma ukimya ule wa Ed akajiongeza kwa kumuuliza Renatha wapi anaishi baada ya kuona dalili zote za binti huyu kutaka kupelekwa na Ed.

"Naishi mitaa ya Diamonds" akajibu mara tu walipotoka kwenye lifti huku akimwangalia Edrian ambaye alitembea pasipo kuwasubiri.

"Nitakusogeza" Allan akamjibu na kumfanya Renatha aliyekuwa akipiga hatua kumfuata Ed kusimama ghafla na macho yake yakamwangalia Ed aliyeingia kwenye gari akawasha na kuondoka..

"Asante Allan, nitachukua gari nje tu hapo" Renatha akajibu akijitahidi kujiweka sawa kutoka katika simanzi iliyompata kwa Ed kutomuuliza chochote

"Usijaribu kunifanya nikushawishi, tafadhali panda twende" Allan akamsihi huku alifungua mlango wa gari. Renatha akaingia. Allan akawasha gari na wakaondoka.

Kwa mbali alisimama Bon akiwaangalia.

Edrian aliendesha mpaka kwa Captain, mambo yalivyoonekana baada ya kupata mrejesho kutoka kwa 4D yalimfanya azidi kuazimu moyoni kupambana na Martinez na binti yake. Bado kichwani alijiuliza TM ni nani maana tangu gari ilipojaribu kuwagonga, hadi ikaelekea nyumbani kwao Aretha, mashaka yake yalikuwa wazi. Maadui alikuwa nao lakini alipata kazi kuwafahamu.

"Nadhani bro huyu Lyn atanyamaza tu ndani ya siku hizi mbili. Anza na ile video ya kule Dishan, ajue kuna kitu unacho ila hukitumii" Captain akamshauri Edrian.

Simu yake ikaita, alipoangalia Aretha ndiye alikuwa akipiga. .

"Retha" akaita mara baada ya kupokea. Mapigo yake ya moyo yalidunda haraka kwa wasi wasi

"Rian samahani, nilitaka kukujulisha kuwa natoka sasa hivi mkufunzi amepata dharura hatutaingia kweny____"

"Retha nisubiri nakuja kukuchukua" Ed akamkatisha Aretha kabla ya kumaliza.

Next chapter