"Mama" Ed akamuita mama yake mara alipoingia
"Eeeh sasa hivi umekuja kunisalimia baada ya kumshusha mgeni wangu"
"Mmmmm" Ed akaguna huku akiendelea kusimama kati kati ya sebule akimwangalia Lyn machoni ambaye alimrudishia tabasamu ambalo lilimaanisha "huwezi kunifanya chochote hapa"
Mama ambaye macho yake yalibaki kumuangalia mwanae aligundua hasira zilizomjaa mwanae
"Jana ulikuwa mgonjwa uliyezirai, leo umepona hata kutembelea wengine, ulikuwa kwenye maagizo?" Maneno haya yalipotoka kinywani kwa Ed ni kama radi ilipiga ghafla mle ndani. Ukimya ukatawala kabla ya Lyn aliyekuwa akitazamana na Ed machoni kujibu..
"Hakuna ubaya wowote kukaa na mama, nilijisikia vizuri mchana nikaona nije"
"Nafikiri umemaliza kukaa na mama, twende nyumbani ukapumzike tena" maneno ya Ed yalionesha kuwa ni mtu anayejaribu kudhibiti hasira zake.
"Ed, hebu acha kumkimbiza mwenzio" mama akaamua kuingilia kati..
"Mama am sorry tutaongea vizuri baadae, naomba niondoke nae" Ed akaongea huku akielekea alipokaa Lyn kumshika mkono, lakini Lyn akamuwahi na kuinuka akisogea alipokuwa mama na kumchutama hata mikono yake ikawa magotini kwa mama
"Mama asante kwa jioni nzuri uliyonipa, ngoja twende, tuna mengi ya kuzungumza baada ya hizi picha kuvuja. Muelewe Ed atakuwa amejisikia vibaya eeh" Akayarudisha macho kwa Ed ambaye alimwangalia kwa ukali japokuwa yeye aliendelea kuweka tabasamu lake la ujanja ujanja..
"Mwanangu asante kuja, karibu wakati mwingine"
Lyn akainuka na kuondoka akimpita Coletha ambaye alisimama hatua chache kutoka kwenye mlango akiwa na tabasamu fulani hivi ambalo lilionesha alifurahia yaliyokuwa yanaendelea. ..
"Edrian" mama akamuita Ed ambaye alianza kumfuata Lyn kwa nyuma kuelekea mlangoni. Akageuka kumuelekea mama yake ambaye alimpa ishara asogee karibu..
"Nimekulea kuwa na utu, usijisahau ukapambana na ujinga kwa kutumia hasira utaonekana nawe mjinga." Kwa sauti ya chini mama alimuonya kijana wake...
"Mmmm" Ed akaguna akamwangalia mama yake, akaona hakuna sababu ya kumwambia chochote kwanza. Akakubaliana na maneno aliyosema, akainama na kumbusu kwenye paji la uso
"Nitarudi" baada ya kusema hivi akageuka na kuondoka akimpita dada yake ambaye alimwangalia kwa huruma
"Stay here till tomorrow" akamwambia na kutoka nje
Lyn alisimama nje akiangalia gari gani alikuja nayo Ed maana aliona gari ya Li ikiwa imeegeshwa.
"Twende" sauti ya Ed ilimshtua kwa nyuma.
Akamfuata hadi gari ya Li ilipokuwa wakaingia kwenye gari, Ed akaondoa gari kutoka ndani na kuingia kwenye barabara kuu inayoelekea nyumbani kwao Joselyn.
"Ed, unaonaje ukipunguza mwendo ni hatari hiv___" kabla hajamaliza Ed aliongeza tena mwendo
"Okay okay... please Ed unajua huu mwendo unaweza kutupeleka paba___!
Ed akaongeza tena mwendo, sasa Lyn alianza kutetemeka kwa namna Ed alipishana na magari huku mwendo ukiwa mkali, akakata kuingia mtaa wa pili ambao haukuwa na magari mengi
"Ed please, stop the car, I don't want to die" Lyn akalalamika huku mikono yake ikiwa imeshika kwenye kiti alichokaa
"Vuum"
Ed akapunguza mwendo na kisha akafunga breki ghafla akamwangalia Lyn kwa macho makali kiasi cha kumtisha
"You don't want to die but you are playing with death Lyn"
Lyn akabaki amemuangalia machoni Ed.
"Nataka wewe na baba yako muache kucheza na maisha yangu..sitafanya chochote kuhusu habari ulizosambaza ila ulichofanya kitarudi kukuwinda"
"Ed, ni huyo Aretha eeeh?" Lyn akauliza huku akimuangalia kwa hasira
Kitabasamu cha upande kilionekana ghafla na kupotea usoni kwa Ed, "sio Aretha, ni wewe na hizo drama zako. Sikia hili ni onyo la mwisho. Mimi na wewe tumemalizana tayari. Live your life and let me live mine, umeelewa"
Lyn akacheka sana "sikia nisipokuwepo kwenye picha yako wala Aretha hatokuwepo"
"Oooh so unataka game na mimi eeeh"
Ed akamuuliza akimtazama machoni
Lyn akamuangalia bila woga "nikipoteza hakuna atakayemiliki nilichopoteza"
"Okay Lyn, usinilaumu mbeleni na onyo langu kwako, usijaribu kudhuru watu ninaowapenda including Aretha, you will read again my profile"
Alipomaliza akawasha gari na kuondoka na mwendo ule ule.