"No" jibu la Lyn lilifuata kwa haraka huku akimwangalia Ed ambaye aliposhusha glasi yake akaendelea
"Kwa nini hapana.... kuna sababu kuu kwa nini isiwe hivyo?" Ed akamuuliza huku mikunjo ikionekana usoni kwake. Lyn akamwangalia, akashusha pumzi, kwa sauti ya utulivu
"Hatuachani...sababu hatuwezi kuachana. Niambie hayo mambo mawili Edrian ambayo ni kizuizi" Lyn akaachia tabasamu ambalo ungeweza kujua ni feki, ndani yake alijaa ghadhabu. Hakuwahi kuachwa na tena kuambiwa na Edrian ghafla ilimfanya ndani ajisikie kufeli hatua kubwa.
Ed alibaki katika utulivu ule ule katika kuongea.." Ni vyema unataka kujua sababu, Kwanza siwezi kuwa na mahusiano ya amani nikijua baba yako ananifanyia ubaya kuangusha kampuni yangu. Lakini wewe unaweza kunizunguka na hata kunilaghai ili nifanye unachotaka. Sipendi kutawaliwa hasa kwenye mfumo huu wa uhusiano- Mapenzi."
"Hizo sio sababu, najua ni huyo binti.....nani vile... Retha eeeh" Lyn aliongea sasa bila mpangilio..
"Ed listen to me! I love you, mbona tulikuwa tu vizuri muda wote huo hadi a__"
"Hadi nilipojua ulinitega kwa dawa kwenye kinywaji changu, ulitaka kufanikisha nini Lyn mmh?" Ed akamuwahi kwa sauti ile ile ya taratibu
Macho ya Joselyn yalikaribia kuchomoka mahali pake aliposikia maneno ya Ed... "I don____"
"What eeeh, ulidhani sitafahamu Lyn?" Ed akamuinulia macho akimuangalia Lyn ambaye alipatwa na kigugumizi lakini akajiweka sawa na kumwambia
"Alright Ed, ni kweli niliweka dawa ili nikupate, nilifanya hivyo kwa msukumo wa mapenzi yangu kwako. Nilikosea nini hasa...mh. . Ni vibaya kumtamani mpenzi wako na kumtega umfurahie...eeeh..niambie Edrian?" Akaikunja mikono kifuani akimwangalia Ed
"Hivyo umefanya sababu ulitaka kunifurahia, bila ridhaa yangu, na siku ukinichukia utaniwekea nini ah...sio sumu?" Kabla Lyn hajajibu Ed akamuwahi..
"Ungeniamini ungesubiri niamue kukufurahisha na sio that one.You actually had guts to make me do things in your way! Lyn am sorry but let's part ways for now still we have respect for each other" akamaliza na kuinua glasi yake yenye mvinyo na kunywa
"Why Edrian! Am not stupid, i know you like that girl, unadhani sikukuona unavyomwangalia kwenye gari" Jazba sasa ilikuwa wazi kwenye sauti ya Lyn.
"Twende nikurudishe nyumbani Lyn, mzigo wako nitauleta." Akasimama Ed,
"I told you Ed, and am still repeating this, am not a fool. Uliniahidi na utaikamilisha ahadi yako. Thank you for a nice dinner" akachukua pochi yake na kuinuka tayari kufuatana na Ed. Wakatoka.
Wakati wakitoka walipofika kwenye eneo la wazi ambapo hakukuwa na watu wengi, Lyn akainama na kushika magoti akamuita kwa sauti dhaifu Edrian, naye alipogeuka nyuma kuona nini kinaendelea.. alishangaa
"Kuna shida gani Lyn m_____?" Kabla ya kumaliza sentensi yake Lyn alianguka,Ed akapiga hatua za haraka kuwahi kumuinua
Akamuita
"Lyn, wake up, what's happening" Lyn hakufumbua macho na alipomshika kwenye mshipa shingoni alishtuka na kuinuka huku baadhi ya watu waliosogea wakijaribu kumsaidia...
Akaelekea ilipo gari yake akasaidiwa kufungua mlango, na mmoja wa watu waliofutana nao, akamuweka kwenye kiti cha nyuma, bila kuchelewa akapokea pochi na simu yake kutoka kwa mhudumu ambaye alivishika baada ya kuwa vimeanguka. Akawasha gari na kuondoka.
Akawaza kumpeleka City hospital wakati huo akachukua simu na kumpigia Li akamuomba wakutane hapo. Akampigia Martinez, baba yake Lyn, ambaye akambadilishia njia kwa kuwa alitaka mwanae apelekwe Embassy Hospital. Akafanya hivyo kwa kuwa baba yake alisema ndio hospitali familia yake inapotibiwa. Alishangaa kuona Martinez akiwa na utulivu hata baada ya kusikia mwanae amezirai, alidhani angekutana na ghadhabu ya baba.
Alipofika Embassy Hospital getini akaelekezwa mlango wa eneo la matibabu ya haraka (ER) akaendesha kufuata maelekezo na alipofika tayari walikuwepo watu watatu wamesimama wakiwa na kitanda cha magurudumu pembeni..
Baada ya kuzima gari, tayari walishafungua mlango wa nyuma na kumtoa Lyn ambaye aliendelea kupoteza fahamu. Wakamweka kwenye kitanda na kusukuma huku mmoja kati yao akiendelea kumkagua...